Hakuna kauli ya moja kwa moja kuwa alizaliwa tarehe hiyo.
KUNA KHILAAF juu ya tarehe ya kuzaliwa Mtume Wa Allah.
Mimi naona muislamu anaefanya maulidi asinyanyue mdomo wake kuponda crissmass kabisa kwa sababu na hawa wanamshereheea mtukufu wao kama ambavyo wana maulidi wanamsherehekea Mtume Muhammad.
Sikubaliani na itikadi ya kikristo lakini pia sikubaliani na waislamu ambao wanawananga wakristo kuhusu krismass alafu wao wanafanya maulidi.
Lakini pia kusherehekea krismass sio kumshirikisha Mungu ikiwa kama huamini yale yanayoaminiwa na hao wenye krismass.
Huku ni kuwasaidia watu katika uovu na sio kila uovu ni kufru,ikiwa utaamini kama wanavyoamini wakristo basi naam hiyo ni kufru kwa mujibu wa UISLAMU.
JA WALE waislamu wanaoponda sherehe za mwaka mpya wakati huo huo wanataka watu washerehekee sherehe za mwaka mpya wa kiislamu,huu pia sio uoni mzuri.
Hii terehe mpya na ile ya kiislamu ni mpya kama kusherehekea zisjerehekewe zote na kama kukatazwa zikatazwe zote.
Ndio maana mimi naona kuwa maulidi,krismass,mwaka mya wa kidunia na kiislamu hizi sherehe zote hazina maana kwangu mimi hata hizo za waislamu walizojitungia hazina mpango wowote.