swali je kwamba unakubali kuna katazo la kutoshorikiana na makafiri katika sikukuu zao?
Hakuna katazo la kwamba usishirikiane na makafiri zinapofika sikukuu zao.
Amri imekuja kwamba usijifananishe nao,na kujifananisha ni kufanya kama ambavyo wao wanafanya.
Lakini kushirikiana ni tofauti.
Mfano leo ama jana sisi waislamu wauza maduka tufunge,michele tusiuze,nyma tusiuze ati kwa sababu tukiuza vitu hivi wataenda kupika na hapo itakuwa tumejifananisha nao.huu ufahamu sio sahihi.
Kwa hiyo kwa kuweka sawa tu ni kuwa kuna tofauti ya kwamba kushirikiana nao na kujifananisha nao,na amri zimekuja hivyo.
Kujifananisha na mtu ni kuiga mambo yake na pia kufuata mila yake yaani unafata matendo yake.
Sasa katika kushirikiana ni jambo pana sana ambalo halitakiwi kutafsiriwa kwa mujibu wa wewe bali litafsiriwe kwa mujibu wa huyo anayefanya.
Mathala ndugu yangu jana ameuza nguo kuwauzia wakristo na anawajua,ameuza mchele na sukari na nyama kuwauzia wakrsito na anajua kwamba hawa kesho wanaenda kula sikukuu,hii kaifiyyah hutakiwi kumhukumu kwamba eti KAJIFANANISHA NAO AMA KAWASAIDIA KATIKA SIKUKUU ZAO,bali hapo itarudi katika nia ya huyo unayemtuhumu,kama alikusudia kweli kushiriki katika hilo naam ni shida lakini kama yeye hajakusudia basi hutakiwi kumhukumu hivyo.
Jibu kama ndio nielekeze ni aina gani ya ushirikiano au jambo gani ambalo ukilifanya utakuwa ndio umeshirikana nao siku hiyo ya hizo sikuu zao?
Ushirikiano ambao utakuwa umenuia kuwasaidia na kujifananisha nao katika sikukuu zao.
Lakini ikiwa haujakusudia kushirikiana nao kisikukuu na kujifananisha nao basi hilo haliitwi ushirikiano.
Mimi krismass naweza kuvaa nguo zangu nzuri tu nikatoka nje alafu wewe unikataze nisivae vizuri ati kwa kuwa leo wakristo wanavaa vizuri hivyo mimi nisijifananishe nao ?
Kwani mimi nimekusudia kujifananisha nao ama nimekusudia mambo yangu tuu jamani.
إن ما الأعمال بالنيات
"Hakika matendo yanahukumiwa kwa nia ya mtu"
Na matendo hayo yanayohukumiwa kwa nia ya mtu ni yale yenye sura ya kujuzu isiyokuwa ya haramu,sio unazini unasema nilikuwa na nia nzuri laa,sio unaiba unasema nilikuwa na nia nzuri laaa.
Bali yale matendo ambayo dhaahir yake yanaonekana hayana uharamu kuyafanya,mfano mtu unaenda kusali sio haramu kusali lakini unasali kwa sababu unataka kuwaibia waislamu,wewe utapata dhambi kwa nia yako na wala sio kwa matendo yako.
Hivyo wewe muislamu siku ya krismass na wewe ukapika wali wako pale safi umeamua kupika alafu Mungu akakuchome moto wakati haukukusudia kuiadhimisha siku hiyo ?
Hii itakuwa Tunamfanya Mungu kwamba hayajui yale ya nafsi zetu kwamba ili akuhukumu basi anaangalia wengine wanafanyaje alafu anakuja kwako wewe kukuhukumu kwa mujibu wa alivyowaona wengine.No No.
Allah anahukumu kwa mtu mmoja mmoja na ndio maana jambo la nia Anayelijua ni Allah pekee na sio mimi na wewe tukaangalia matendo ya nje tukahukumu.
Nimejibu kwa urefu utanisamehe lakini nimeona niandike haya pengine ukapata jambo
Kama jibu hapana naomba dalili ya kuruhusu kushirikiana na makafiri katika sherehe zao
Nilishajibu kuwa ushirikiano ambao utakuwa umeutilia nia ya kusapoti sikukuu zao na kujifananisha nao basi huo ndio ushirikiano ambao umekatazwa.
Kwa hiyo huo ushirikiano utaambatana na NIA ya Mfanyaji na wala sio utakavyoona wewe kwa dhaahir yako.
Siku ya sikukuu sio kwamba ni siku special saaaana kwa Allah kwamba eti siku hiyo asiangalie nia ya Mtu badala yake aangalie je anajifananisha vipi na wengine .,sivyo hivyo ndugu.