Sasa matusi ya nini yahkee? Mimi kwa mfano ni mkristo. Simusapoti Israel kwa sababu ya ukristo wangu, la hasha. Israel wengi bado wanaheshimu uyahudi wao, dini kongwe kuliko Ukristo na Uislam.
Namsapoti Israel kwa sababu ya historia. Historia inatuambia Jerusalem ni jiji lililojengwa na waebrania=Israel=wayahudi. Umejengwa kwanza na Daud, lkn Suleiman akafanya kazi kubwa zaidi. Hata majina ya miji hiyo, yanasadifu uzayuni kuliko upalestina. Hiyo tu ni ishara tosha kuwa ni miji mikongwe ya wazayuni au waebrania.
Wote tunafahamu kupitia historia kuwa, Isaak na Ismail wote ni watoto wa Ibrahimu ambaye ni mrithi wa ahadi za Mungu. Tofauti iliyopo kati ya Ishumael=baba wa wapalestine na Isack=baba wa waebrania, ni kuwa mmoja alikuwa na mchanganyiko wa damu yaani Ebrania+Egypt wakati Isaak alikuwa pure Israel au myahudi.
Tofauti nyingine ni kuwa, Isack ni mtoto wa ahadi, wa kurithi mahali pa Ibrahimu, lakini Ishumael alifukuzwa na kuwa mkimbizi mbele ya ndugu yake Isack. Pengine hata kuoa alioa kwa warabu kuliko kwa waebrania.
History inatuambia pia, Israel walipokosa, walinyang'anywa nchi na vyote viijazavyo, wakachukua wengine, lkn historia hiyohiyo inasema ipo siku huyu aliyefukuzwa atarudi kwake, aendeleze maisha hapo.
Utata uliopo, umekimbia miaka mingi iliyopita, unarudi unakuta watu wamejimilikisha eneo lako. Je kudai eneo ambalo ni mali yako, ni kosa?
Wewe umejenga mji wako huko, baadae ukakimbilia mjini wengine wakauendeleza. Baadae maisha yamekupiga, unaamua kurudi kwenye mji wako, unakuta watu wameendeleza lkn unakumbuka hakika nyumba uliyoiacha ulivyo ijenga. Je kudai mali yako hiyo ni kosa?
Kama Palestine wanadai wao ndo walioubuni mji huo, iweje ukose majina ya kipalestina au kiarabu lakini uwe na majina ya kiyahudi?
The best solution ni kuwafanya watoto wa Ibrahimu kukaa pamoja kama familia, lakini kitendo cha Palestine kuwaona Israel hawastahili wakati wao ni mazao ya kuchepuka tu, wanajidanganya.
Vitisho vyao havitaiyumbisha Israel, na siku zote wameonesha hivyo. Tangu mwaka 1948, wameonesha wana uwezo kuliko Palestine. Cha msingi wakae wayamalize kama watoto wa baba mmoja siyo kujifanya wajuaji.