Messi akishinda tena Ballon Dior itakuwa ni yale ya upendeleo, mapenzi na favouritism

Messi akishinda tena Ballon Dior itakuwa ni yale ya upendeleo, mapenzi na favouritism

Wewe ndiyo umesema kutoka na moyo wako,ila hamna sehemu iliyo andikwa kwamba ukishinda UEFA basi ww unastahili Ballon Dor na ndio maana nikakuomba takwimu na reference.

Halafu kombe la dunia ni mchakato wa mda mrefu,sio tukio la mwezi mmoja,timu hazi chaguliwi bali zinapambana au ushajiuliza kwa nini Halaand timu yake haikushiriki?

Maana kwa jinsi mnavyo ongea hizo timu 32 kama zimepewa nafasi za upendeleo kushiriki kombe la dunia.

kwanini Iniesta hakushinda Baloon Doir 2010?
Kwanini Manuel Neur hakushinda Baloon Dior 2014?
Kwanini Griezmann hakushinda Ballon Dior 2018?
Na kwanini Messi ashinde 2023?
 
Ucl ndio kila kitu kakwambia nani ?

hivi washabiki wa Pessi leo munalipinga hili? Wakati Messi alipokua ashinda hizo Ballon Dior kwa kupitia champion League sio ndio nyie muliokua mukimwaga radhi miataani?
 
Tap ins goals ndio unasema top performer huu mpira wa LiveScore inabidi muachane nao
Mchezaji ambaye hawezi kumpiga chenga hata mchezaji mmoja unataka awe mchezaji bora wa dunia
Hiyo ni dunia ya wapi ?
Kwenye nyakati muhimu haonekani
Hahahaha
Acha kuangalia mpira LiveScore

80% ya magoli ya Messi na Ronaldo ni Tap ins pia kwanini leo iwe tatizo kwa Halland?
 
Mwaka wa kombe la dunia aliyechukua kikombe mara nyingi ukiacha 2018 huwa lazima huyo atoe mchezaji wa Ballon D’or!

Sio kweli mkuu.
2010 - Messi
2014 - ROnaldo
2018 - Modric

Mara nyingi ipi unayokusudia wewe? Au millennium iliyopita?
 
nikuwa unapoteza kumbukumbu ama unazirusha? Modric alishinda Champion League pia kwenye ule msimu
Varane alishinda Champions League na World Cup.

Modric alimflip Varane kwa performance yake WC ambapo alikuwa MVP. Champions League Ronaldo alifanya vizuri kumzidi Luca. Unajitoaje ufahamu kindezi hivi?
 
Varane alishinda Champions League na World Cup.

Modric alimflip Varane kwa performance yake WC ambapo alikuwa MVP. Champions League Ronaldo alifanya vizuri kumzidi Luca. Unajitoaje ufahamu kindezi hivi?

Lakini Modric alikuwa ndio second best performer wa Club kwenye Champion League. Au kuna sheria inayosema kila Club haihitaji kuwa na nominee zaidi y a mmoja?
 
Lakini Modric alikuwa ndio second best performer wa Club kwenye Champion League. Au kuna sheria inayosema kila Club haihitaji kuwa na nominee zaidi y a mmoja?
Kumbe hakuwa best ila second best. Kama ni hivyo alishindaje ubora wa dunia ikiwa WC haikusaidia?
 
Kumbe hakuwa best ila second best. Kama ni hivyo alishindaje ubora wa dunia ikiwa WC haikusaidia?

Kwasababu alikua ana extra max ndani ya WOrld Cup, kitu ambacho Ronaldo hakuwa nacho.

Tatizo la kijana wenu Messi Champion League ameishia round of 16 hicho ndicho kinachomuumbua.
 
Messi apewe mwakani dunia iachane na huyu mtu. Labda huenda tukashuhudia vipaji vipya vikishindanishwa sio kijana anaibuka anakutana na mzee kwamba ndo mshindani wake.

Mashabiki tunahitaji burudani mpya, ushindani mpya, vita mpya.
Wewe na kina Nani..??haya muungane mkampe mnayemtaka
 
Hivi kwanini watu tunabishana nani anastahili wakati mshindi anapatikana kwa kupigiwa kura?

Labda mimi ndio sijui

Lakini kama ni vigezo hapo kutakua na mjadala

Kelvin De Bruney aliulizwa kati ya Halaand na Messi nani anastahili
Kelvin akajibu ni Halaand
Akaulizwa lakini Messi kabeba kombe la dunia
Kelvin akajibu Hata Iniesta alibeba kombe la dunia lakini Messi akashinda
Akaulizwa lakini Messi alikua mfungaji bora alifunga magoli mengi kwa msimu
Kelvin akajibu hata Halaand kafunga magoli mengi kwa msimu

Nadhani tuheshimu maamuzi ya KURA hata kama yana utata
 
Back
Top Bottom