Messi Vs Pele

Messi atwae WC 3 ndo ataongea lugha 1 na Pele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Huu ndo ukweli
 
Huyu nimemwona ni shabiki wa CR7 aka HATER [emoji23]
Hivi watu mnadhani kabla ya CR7 na Messi watu walikuwa wanacheza karata na hawachezi mpira ?

Hivi unajua pale nyumbani tu kwa Ronaldo kuna a Jamaa aliyezaliwa Msumbiji hajamzidi record yake ya magoli katika timu ya Taifa ? The guy know as Eusebio (The Black Panther) ?

Au unadhani mpira ulizaliwa kipindi wewe umeanza kuuangalia ?
 
Pele ilifika hatua raisi akamdeclare as national treasurer, ndio maana hakuuzwa kwenda ulaya.. Alikuwa ni kama pembe za ndovu au meno ya simba.

Pele kacheza kipindi kigumu jamani, tafuteni video zake watu wanachapa kisawa sawa, hakuna redcard
 
Ubora wa mchezaji unapimwa kwa social media ? unadhani hii ni Big Brother ? Leta dissections ya vitu sio nani ana wapenzi wengi ? Mambo gani yamefanyika na wakati gani....

Soma post ya mwanzo Maradona Messi wanaweza kutumika kama playmaker tengeneza teams around them ila tukija kwenye playmaker tamchukua Andre Pirlo Maestro... tukija kwenye clinical finishers Messi anaachwa mbali, dribbling Pele hakuwa nyuma ila kuna kina garrincha huenda angecheza kama winger angepiga chenga Pele was a complete athlete ambaye walishasema ange-excel kwenye any sport ambayo angefanya...., Na chenga za leo haupigwi buti huwezi linganisha na Chenga kipindi cha kupigwa ndaruga na refa anapeta..., Mpira umekuwa ukibadilika na kuwa a non contact sport...

Siongeli vitu kwa mapenzi ya mtu naongelea vitu kama mpenda kandanda na mfuatiliaji wa mambo na sio nani ana followers wengi au nikupe votting inayompa Ruud Gullit kwamba ndio the Best Player ?
 
Pele ilifika hatua raisi akamdeclare as national treasury, ndio maana hakuuzwa kwenda ulaya.. Alikuwa ni kama pembe za ndovu au meno ya simba.

Pele kacheza kipindi kigumu jamani, tafuteni video zake watu wanachapa kisawa sawa, hakuna redca
Messi ana goli la mkono, thierry Henry ana assist ya mkono
 
Pele ilifika hatua raisi akamdeclare as national treasury, ndio maana hakuuzwa kwenda ulaya.. Alikuwa ni kama pembe za ndovu au meno ya simba.

Pele kacheza kipindi kigumu jamani, tafuteni video zake watu wanachapa kisawa sawa, hakuna redcard
Hayo ni mambo ya kisiasa, hata Messi serikali yao ikiamua kucheza politics inaweza kumtangaza ni hazina ya Taifa. Si tunasikia wanataka kuweka sura yake kwenye pesa?
 
Hizi habari za skills wachezaji wengi wanafanya. Mpaka wachezaji wanaocheza vilabu vya kawaida.
Kwa hiyo hoja za skills na dribling achana nazo.

Niambieni ni kitu gani Pele alifanya Messi hakukifanya.
Seriously ?

Ngoja nikupe stats ambao wote wamecheza...

Pele alicheza world cup nne tu ( I repeat NNE) na katika hizo nne 1958 akiwa na miaka 17 aliingia na kufunga(record ambayo haijavunjwa na hapo mechi za mwanzo alikuwa bench- unajua tena kuwa rangi nyeusi wakati huo) kijana aliwasaidia Brazil kuchukua kombe na Goli lake fainali angainst Sweden la kwanza kati ya mawili ili-involve kumdash mchezaji wa kwanza (left for dead) wa pili kupigwa kanzu na kufunga bao...

1962 akacheza mechi mbili ya kwanza against Mexico akafunga bao la pili pamoja na kupigwa kiatu cha kutosha, mechi ya pili na wa-Czech akapigwa kiatu mpaka akashindwa kucheza mechi nyingine....

1966 waingereza na figisu zao alipigwa kiatu game ya kwanza cha kutosha against portugal wakammaliza kabisa hadi akasema ana-retire mpira kutokana na kwamba alikuwa target ya watu kumuondoa (kipindi hicho chote hakuna red/yellow cards)

1970 FIFA waka-introduce Yellow / Red Card Pele akarudi na kuchukua ndoo nyingine....

Messi kacheza world cup mechi nyingi zaidi katika world cup anazidiwa na mtu mmoja tu hapa duniani..., na katika hizo ingawa ameshiriki fainali mara mbili ameshinda moja...


Kwahio hapo unaweza kuona nani ni clinical na when push comes to shove who bottles it..., na katika hizo mechi alizocheza kuna ku-miss matuta

Ndio ikaja point yangu kuu kipindi hiki striker / anaweza kucheza mechi nyingi zaidi kipindi hiki ni rahisi kuliko kipindi cha kina Pele (Football imekuwa non contact sport) yaani mtu anapiga vyenga unamuangalia na kumpuliza puliza zamani yeye na mpira angejikuta kwenye chaki...
 
Unakataa nguvu za social media wakati sasa hivi tunawalinganisha hapa jukwaani. Kwani hizo debate za messi na cr7 nani mkali zinafanyika wapi. Uwanjani?

Kwanza mjadala mnahamisha. Messi hajawahi kulinganishwa na pele. Pele alilinganishwa na maradona thats why wakapigiwa kura kwenye ile ya kumpata mchezaji bora wa karne.
Hii ya kumfananisha Pele na Messi inakuja baada nyie mashabiki wa cr7 kuona sasa hamna namna. Ndio mnakimbilia kuanzisha mijadada kama hii kujifariji.

Messi top ya wote waliowahi kucheza soka dunia hii.
 
Hayo ni mambo ya kisiasa, hata Messi serikali yao ikiamua kucheza politics inaweza kumtangaza ni hazina ya Taifa. Si tunasikia wanataka kuweka sura yake kwenye pesa?
Fuatilia mambo kabla haujasema, Kipindi Pele yupo Peak Brazil kulikuwa na fukutu la Kisiasa kwa sababu Pele aliunganisha watu na Timu zote za ulaya zilikuwa zinamtaka Pele Rais wa kipindi hicho akapeleka hoja haraka haraka Bungeni ili Pele asiondoke na watu waendelee kumfaidi na sio kufuatilia Siasa za nchi....

Pele alikuwa na impact kwa watu wengi bila Joao Havelange kutembea na Pele mpaka Africa huenda asingepata kura na kuwa Rais pekee wa Fifa ambae hatoki bara la Ulaya na ulaya wangeendelea kufanyia figisu mataifa mengine..., Pele alifika Nigeria kwenye exhibition match na walivyosikia the King atakuwa anacheza wakapatana waache kupigana kwa masaa 24 ili wakamwangalie the King...
 
Kama ungekuwa mtihani na mimi ni mwalimu wako ningekupa alama 0. Sababu swali nililokuuliza umetoa majibu ya ajabu.

Swali linauliza, Pele kafanya nini ambacho Messi ameshindwa kukifanya? Umekuja na maelezo ya ajabu.

Mfano. Lissu aliuliza ni kitu gani ambacho Magufuli alifanya Nyerere alishindwa kukifanya kwenye eneo la maendeleo.
 
Nakwambia Rais wa wakati huo kisiasa alikuwa na hali mbaya, ili kujipa kiki kwa wananchi akafanya move hiyo maana Wabrazili wanapenda mpira sana na walimkubali Pele. Lakini hayo ni mambo internal ya nchi, ni kama sisi tulivyowahi kumuweka kwenye Stempu Jellah Mtagwa baada ya Tanzania kufuzu kucheza kombe la AFCON mwaka 1980
 
We hujawahi kusikia kuwa Fifa ilimgeuza pele kuwa chombo chao cha propaganda? Hizi shutuma zisemwa sana.
 
We jamaa una matatizo kweli unajibiwa vizuri tena Kwa evidence unaleta mambo ambayo hayaeleweki kweny maelezo ya jamaa kitu Gani hujaelewa umeulza amefanya kitu Gani Pele ila Messi hajafanya unapewa majibu ya maswali Yako bado unagwaya wew sio mtu wa mpira achana na mpira kafundishe vitenzi wanafunzi wako
 
Unakataa nguvu za social media wakati sasa hivi tunawalinganisha hapa jukwaani. Kwani hizo debate za messi na cr7 nani mkali zinafanyika wapi. Uwanjani?
Wanaoongelea mpira sababu ya social media waache waendelee kuongea ukisoma post yangu ya mwanzo kabisa nimesema football is a game of opinions na hilo sikatai mimi ukiniambia wachezaji wakali duniani naweza kumtaja Andre Pirlo, the guy has footballing brain..., wala sitashangaa watu wanaopenda entertainers, au waliompenda OCD kutokana na uchezaji wake wa akili au Samli Ayoub kutokana na Ustaarabu wake wakati ni beki..., its all about Opinions wala haikatazwi.... Na wakati watu walikuwa wanaangalia Galacticos kina Zidanne na Roberto Carlos mimi nilikuwa naangalia umuhimu wa Makelele bila yeye timu inakosa balance wakati wengine wanafanya fancy stuff yeye anaprovide safety...
Kama unafuata mchezaji bora kwa kura kama za urais hio ni prerogative yenu, lazima kizazi ambacho kipo current kichagua mtu ambaye yupo current sababu ndio wamemuona na kukua nae; ila footballing people tunakwenda deep..., Sasa baada ya kuja Kwamba Messi ni bora kwa miaka yote ndio likaja swali Pele vipi ? Ooh Pele kipindi kile kulikuwa hakuna sheria, mara kulikuwa offside (hizi zote ni story za kwenye Gahawa..., Na mimi kama mpenzi wa soka ninasaidia kuchambua makapi kwenye ukweli hayo mengine ya mapenzi ya fulani au nani ninawaachia nyie na social media zenu
 
We hujawahi kusikia kuwa Fifa ilimgeuza pele kuwa chombo chao cha propaganda? Hizi shutuma zisemwa sana.
Kwahio ?

Nashukuru uwepo wa Pele na kumsaidia Havelange kuwa Rais wa FIFA, hii FIFA imekuwa bora leo kuliko asingekuwepo Havelange, Ulaya walikuwa wanajivutia kwao hata kupata mwakilishi kutoka Africa kila mwaka ni baada ya Africa kugomea worldcup 1966, Havelange na baadae Blatter walisaidia sana kwa kukipa kila Chama cha Mpira Kura, no matter hata kama kinatokea Africa na hivyo kupunguza ubinafsi wa ulaya...

Kwangu mimi FIFA has done wonders kwenye Mpira, kwahio kama hutaki FIFA ifanyiwe Propaganda unataka nani afanyiwe UEFA ?!!

Stars wana following kubwa kwahio kila mtu /watu / kampuni na bidhaa zinawatumia that's life.. iwe mwanasiasa au Adidas au Nike au Pepsi; sipo huko kuangalia extra curricular activities za hawa watu outside soccer bali ni kuweka ukweli kwenye ukweli na uongo kwenye uongo (nadhani hili la kwamba zamani kulikuwa hakuna offside tumeshalifunga na kwamba zamani kwa striker kucheza mpira ilikuwa rahisi ni mtu tu asiyeshirikisha akili yake na mdomo wake ndio anaweza kutamka hayo maneno)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…