Messi Vs Pele

Afadhali wewe umeona Mkuu....

Hapa naona nitakesha yaani ni kama tunashindana ni nani anatoa post nyingi majibu unayotoa yaani kama watu hawaoni kule juu nimeweka kwamba sio kweli zamani kulikuwa hakuna offside ila unakuta post ya 30 mtu anarudia yaleyale; hapa bora kwanza nikafanye mengine takuja baada ya siku kadhaa na kuanza kujibu majibu ya jumla jumla...

Yaani ni bora watu wanaobishania vitu subjective na kila mtu anaweka point yake... ila huku mtu anabisha kabisa kwamba nyeusi ni nyeupe.... ukimwambia kwanini ni nyeusi anaenda kwenye mambo mengine ili mradi basi tu tunapotezeana muda
 
Samahani naomba uniambie , Je,zama za Pele kucheza walikuwa wanaingia uwanjani wanacheza tu filimbi ilipigwa mpira ukitoka nje ya field of play tu na wakati wa kuanzisha na kumaliza mechi? Maana unajaribu kutuaminisha kwamba Pele alikuwa anacgezewa rafu refa anapeta ina maana unataka kutuaminisha wakati wa pele mtu akichezewa rafu hapakuwa na hatua yoyote inayochukuliwa.
 
Tukubaliane, kutokubalia.
Kwa hiyo hapa tunalinganisha nini? Ubora wa mchezaji au umuhimu wa mchezaji? Sababu chenga zote pele anazopiga, messi anaweza pia kupiga. Kifupi kila kitu ambacho pele alikuwa akifanya Messi anaweza.

Kwa maelezo yako nilivyoelewa kwenye hii post ninayoQuote, ni kama unazungumzia mchezaaji muhimu. Ndio maana unahangaika kumtaja Mzee Pirlo na makele. Bada kama ndivyo, Messi ni bora na pia ni mchezaji muhimu kwenye timu.
 
Its like comparing God to Jesus! Its very confusing and conflicting. But the fact being there is only ONE GOD
 
Nisaidie wewe unayejua soka. Ni jambo gani uwanjani pele alilifanya wakati akicheza ambalo Leonel Messi hawezi au ameshindwa kufanya anapokuwa uwanjani. Kama hilo jambo wote wanaliweza nani analifanya kwa ufanisi zaidi. Swali mbona rahisi sana!
 
Wewe ukizuiliwa kwenda shule huko kijijini kwenu , unaweza kusema ndicho kigezo cha wewe kutokuwa na maendeleo na hivyo usipimwe na wale waliokwenda shule?

Namaanisha Pele apimwe kwenye world stage hizi habari za ohh alikuwa nyara haziwezi kubadili ukweli.
Ninachoweza kusema ni kwamba huenda alicheza zama za ushindani kidogo na hivyo fighting yake ilibaki ni ya kutoshindana na yeyote , hata wewe hapo bila ushindani wa karibu utambwelambwela na kuamini unachokifanya ni kikubwa zaidi kumbe ungekuwa na mpinzani wa karibu ungefanya zaidi ya hicho ulichofanya matokeo yake ukilinganishwa kwa takwimu na wenzako unaonekana ulikuwa bora zama zako zama zote unaonekana wa kawaida tu.
Ukitaka kuamini hili fikiria kama Ronaldo angefikisha mafanikio aliyonayo individually bila Messi kuwa karibu yake anamkimbiza.
Siku zote spidi yako huongezeka zaidi iwapo kuna kinachokukimbiza unataka kisikufikie.

Fikiria tu bila Ronaldo Messi angekuwa na Ballon Dior ngapi , huenda angekuwa nazo 15 au angekuwa nazo 2 tu
 
Kama ni rahisi kufunga kwa kupiga chenga tu wewe umeshindwa nini kumfunika Messi?

Hoja yako nzima imebaki kwenye ishu ya rafu tu hadi imekosa mvuto , unataka kutuambia huyo Pele ndo alikuwa anapigwa viatu wengine hawapigwi? Hivi leo unaweza kusema Ronaldinho alikuwa hapigwi viatu ndo maana alikuwa haumii mara kwa mara watu wakakuelewa?
Dembele alikuwa anaumia mara kwa mara hadi Barca wakasema wanafikiria kumwachia cos faida kwa timu hana unataka utuaminishe eti Dembele ni bora kuliko Ronaldo ndo maana alikuwa anaumizwa mara kwa mara?

Dembele kwa sasa ubora wake umerudi na majeruhi hakuna kwake unataka tuseme sasa hivi mabeki hawamchezei rafu?Kama Pele alikuwa anaumia mara kwa mara huenda kuna factor nyingine zilikuwa zinachGarinchaangia eg hakuwa mpiga chenga makini mbona hakuwa akiumizwa kama yeye wakati naye alikuwa hatari (Jibu linaweza kuwa Simple huenda Pele alikuwa na style ya kucheza ile ya Kibu D ) ya kujibamiza bila akili kwa wachezaji wenzake.Unapenda kula nini nayo yaweza kuwa sababu ya yeye kuwa rahisi kuumia maana vyakula navyo ni muhimu.

Dembele aliambiwa azingatie diet ambayo alikuwa haipendi ili aepuke majeraha rahisirahisi na akaambiwa na Messi kwamba kuna wakati wa kupiga chenga,wakati wa kudribble na wakati wa kutoa pasi si kila muda utake kudribble leo hii majeruhi yamemwepuka.

Hoja ya rafu haina mashiko hata kidogo
 
Vile vikosi ambavyo Pele alichezea kwenye kombe la dunia vilikuwa vimekamilika. Kwa hiyo hata kama Pele asingekuwemo vingetwaa ubingwa tu.

Chukilia mfano michuano ya meaka 1962, licha ya Pele kuumia katika mechi ya pili, lakini akina Garincha waliibeba timu mpaka ikafanikiwa kubeba ubingwa.

Halafu kitu kingine inabidi uelewe, Kubeba Worldcup ni team work. Sasa kama wewe kwenye kikosi ni bora sana ila kuna wenzio wanafungisha, hilo linakufanyaje usiwe bora?

Cha msingi angalia individual contributions katika kila gemu, usichukue mafanikio ya timu nzima na kumtwika mtu mmoja, au usitumie kuvurunda kwa timu ukamtwika mtu mmoja!.
 
Fact
 
Tanzania tupo ranking ya chini sana kisoka hiyo ni pamoja na uelewa wa soka Duniani...
Pele sio wa kufananishwa na Messi
Messi watu wake ni wakina CR 7
Gaucho na Zidane
Elexander kiungo wa Italy na wakina Xavi au Iniesta...
 
Tanzania tupo ranking ya chini sana kisoka hiyo ni pamoja na uelewa wa soka Duniani...
Pele sio wa kufananishwa na Messi
Messi watu wake ni wakina CR 7
Gaucho na Zidane
Elexander kiungo wa Italy na wakina Xavi au Iniesta...

Wewe ni mwanampira kweli au ni shabiki tu?
 
Nisaidie wewe unayejua soka. Ni jambo gani uwanjani pele alilifanya wakati akicheza ambalo Leonel Messi hawezi au ameshindwa kufanya anapokuwa uwanjani. Kama hilo jambo wote wanaliweza nani analifanya kwa ufanisi zaidi. Swali mbona rahisi sana!
Pele wakati anacheza mpira alifikisha Goli 1000 Messi wakati anacheza mpira kashindwa kufikisha Goli 1000 ana jumla ya Goli kama 700hivyo kitu ambacho Pele ameweza kufanya uwanjani ni kwamba Kafunga jumla ya Goli 1000 wakati Messi amefikisha Goli 700 plus
 
[emoji23]
Na Messi kachukua best world cup player of the tournament mara mbili ,Pele ana ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…