Messi Vs Pele

Messi Vs Pele

Higuan yule mshenzi sana alinifanya nimchukie mno

Ila kwa mchango wa messi kwenye mpira dunia hii hata asingebeba kombe la Dunia bado ndiye angekuwa mchezaji bora wa wakati wote
Kama ni World cup hata Messi 3 angekuwa nazo timu ilikuwa haijitambui tu eg 2014 ile fainal Argentina alishindwa mwenyewe kisa ujinga wa other strikers huwezi kumlaumu Messi hapo
 
Kama ni World cup hata Messi 3 angekuwa nazo timu ilikuwa haijitambui tu eg 2014 ile fainal Argentina alishindwa mwenyewe kisa ujinga wa other strikers huwezi kumlaumu Messi hapo
Kwahio hio timu ambayo haijitambui ilimsaidia kufika fainali ?

Na aliye-miss chance ya kufunga goli alikuwa nani ? Pacha wake Messi ?
 
Mkuu mbona unakuwa mvivu ? Ulishawahi kujiuliza na kufanya Research kwanini Pele hakwenda Juventus, Real n.k. Tafuta sababu alafu utaelewa...

Ila kama watu wenye uwezo wa kuchambua ngoja tupime like for like..., yaani makombe / mashindano aliyocheza Pele na ambayo kacheza Messi (like for like) ambayo ni World Cup.., Hapo Stats zipo vipi naomba unijibu...
kati ya Messi na Ronaldo kwako wewe nani ni bora zaidi a complete footballer ?
 
Mimi nijipinge nimekuwa kichaa? Acha dharau mara moja

Nilikuwa najibu hoja yako kuwa vilabu vya bocce juniors na rivar plate ni bora kuliko vya uropa ndio nikakuambia km ni bora mbona hawaonekani kuchukua ubingwa wa klabu wa Dunia?

Sasa umejileta mwenyewe kwa kusingiziq ulaya kulikuwa na ubaguzi mbona wachezaji wengi weusi walikuwa wanacheza au yeye pele alikuwa mchezaji wa njano ndio akakataliwa?
Okay kwahio cup competition haina maana ? Sawa.... ngoja nifuate logic yako ili uone kwamba hata wewe mwenyewe hujui unaongea nini au unasimamia nini ?

Hivi unashindwa hata kufanya research kidogo ndugu yangu.... unaongelea kwamba Europe ndio kuna mpira kipindi cha Pele wangapi walikuwa wanatoka kwao kucheza Europe ? Na kipindi hicho ambacho Brazil ilikuwa inachukua makombe huku na kule wale wachezaji walikuwa wanacheza timu gani ? Pili unajua 1961 pele alifanywa nyara ya Serikali ili asichukuliwe ?

Unajua mambo ya ubaguzi ? Eusebio alikuwa the Best Footballer in Europe mara kadhaa ila unajua walivyokutana na timu ya Pele ilkuwaje ? Kuna kombe lilikuwa linaitwa Intercontinental Cup na hili zilicheza timu za Ulaya na South America... unajua ilikuwaje kipindi cha Pele ?

Having already won the World Cup with Brazil, he became a world champion at club level as Santos defeated Benfica to win the Intercontinental Cup in 1962, repeating the feat the following year against AC Milan. In addition to two Intercontinental Cups, Pele's Santos won the shortlived Intercontinental Supercup in 1968.



Club Bingwa ya dunia ilianza lini ? Mkuu cheki hapo continental cup ambayo ilikuwa ni European and South American Cup kipindi cha Pele...

Pia nimekwambia hata wewe mwenyewe unajipinga..., hapo juu umesema world cup (cup competition sio kipimo) sasa club bingwa ni nini ?
 
Mtu anakuja kukuambia eti "enzi hizo mpira ulikua mgumu". Hebu tuheshimiane asee!


Kipindi ambacho akina Maradona walichukua ndoo kwa goli lililofungwa kwa mkono ndio mpira ulikua mgumu? Kipindi ambacho hakuna VAR, wala idadi kubwa ya mashindano ndio mpira ulikua mgumu? Acheni porojo.

Huu ndio wakati bora kabisa wa mchezo wa mpira, kwa sababu probability ya kufanya udanganyifu ni ndogo sana. Teknolojia imeweka mambo mengi sawa, yani hata ukizidi nywele tu watu wanajua hiyo ni offside, na hupewi goli.

Huwezi kufunga goli kwa mkono katika zama hizi za V.A.R alafu likahesabika!

Watu wanacheza ligi ina mechi 30, wanapiga sijui Carrabao cup, wanapiga FA cup, wanapiga UEFA na wengine EUROPA. Hapo bado michezo ya kimataifa inawasubiri, na kote huko teknolojia ipo kuhakikisha hakuna udanganyifu. Hakuna kitu utaniambia kuhusu mpira wa zamani nikakuelewa!

Messi is the GOAT. That's what the numbers say. And last time I checked, numbers didn't lie!
 
Mnaosema eti Pele ana Worldcup tatu. Mwaka 1962 Pele aliumia kwenye Mechi ya pili na kushindwa kumalizia tournament,
Sasa aliumia ulitaka acheze na maumivu ? na hizo mechi mbili alifanya nini ?
Mechi ya Kwanza na Mexico nani alifunga goli la Pili ?

Na unajua kwamba 1966 angeweza kuchukua tena lakini ni kwamba alipigwa kiatu hadi akaamua kujiuzulu ? Je unajua bila FIFA ku- introduce red / yellow cards Brazil wangegoma kucheza 1970 ?


akina Garincha wakaibeba timu mpaka kutwaa ndoo halafu unakuja hapa kumsifu kwa Worldcup Tatu?.
Kwamba goli alilofunga dhidi ya Mexico ulifunga wewe ? Ofcourse 1962 world cup belonged to Garrincha mchawi wa chenga....
Messi katwaa Copa America, Pele hajawahi kutwaa Copa America!.

Messi amekuwa mchezaji bora wa mashindano ya Worldcup mbili, ya mwaka 2014 na 2022 , Pele amekuwa mchezaji bora wa Worldcup ya mwaka 1970 tu.
Kwamba 1958 youngest World Cup Player alikuwa nani ?
 
Kwahio unadhani watu na akili zao wanatafuta stats za kina Pele kwa kutumia Instagram ya Pele ? Yaani FIFA Officially verified Stats ni Insta ya Pele ?

Hii nishajibu mara kibao hata kwenye Post hapo juu acheni kudanganyana Offside rule imeanza tangia 1800's na pia haikuwa marginally onside bali lazima awepo jamaa kabisa mbele yako achana na sasa kwamba upo nae sambamba
Messi ndo mchezaji Bora wa muda wote wewe endelea kuamini unavyo amini sikuzuii ila kwangu Messi ndo mchezaji bora
 
Sasa mbona hapo anachezewa rafu na refa anasimamisha mpira kuonesha ni faulo? Tafuteni vigezo ndugu zangu otherwise Messi ni bora kuliko huyo pele.
Hata uelewa unao mkuu ? Kipindi anaanza kulikuwa hakuna red/ yellow wala substitution na rafu nyingi refa anapeta.
Ngoja niseme jambo la uongo kwako ,
Umesema enzi hizo asist zilikuwa hazihesabiwi ila umetuandikia kwamba Pele ana 0.83 za asist huku Messi akiwa na 0.79
Huu ni uongo maana kama takwimu hazikuchukuliwa wewe umezitoa wapi?
Narudia uelewa wako unatia mashaka nimesema kipindi cha pele assists zilikuwa haziwi recorded kwahio inabidi watu warudi kutazama mechi ambazo zilikuwa televised (sio zote) kwahio hii stats ni ngumu kuipata sababu hatuna kina opta index wanaochukua kila takwimu Kwahio hizo sio official upande wa Pele
Kuna kipengele cha Offside ambacho umekisemea mi naona cha wakati wa Pele kilikuwa soft maana enzi za sasa ambazo Messi kafunga sana hata tshirt ikizidi tu tayari ni offside that means Messi kafunga magoli huku wachezaji wengi ikilazimika awapite kwanza ndo akafunge.
Again uelewa wako mkuu kipindi kile hakuna marginally offside yaani achana na shati yaani hata kama defender anakuweka onside kwa nusu mwili bado ni offside na zamani kabisa haikuwa mmoja tu bali wawili kwahio kila wakati kulikuwa na defender mbele yako ambae haogopi kwamba ana-kuplay onside....
Huyu Pele anaweza kuwa alikuwa bora sana ila Messi kamfunika kwa vingi sana kiuchezaji.
vipi ?
 
Messi ndo mchezaji Bora wa muda wote wewe endelea kuamini unavyo amini sikuzuii ila kwangu Messi ndo mchezaji bora
Hapa hatupo kuridhishana mimi na wewe bali ni kuweka data / facts za nini ni nini ? na vipi na wapi ?
 
Back
Top Bottom