De Lima ni mshambuliaji mahiri aliyecheza na kuwa na mafanikio makubwa sana katika ligi mbalimbali na bora kabisa duniani akililetea Taifa lake heshima kubwa sana sawasawa la alivyofanya katika vilabu mbalimbali alikosukuma kandanda. CR7, mbali na kufanya vizuri akiwa England hajaacha kusukumiza mpira nyavuni akiwa na RMA na kwa bahati sana ametoa mchango mkubwa kwa Taifa lake akiwa mchezaji wa kawaida na pia akiwa nahodha. Hii imemfanya kuchaguliwa na kutunukiwa heshima kubwa ulaya na duniani kuonyesha ubora wake juu kabisa ya wachezaji wengine wakiwemo akina kichuya, tambwe n.k. Messi ameanza na probably atastaafu akiwa na Barca na soka lake muda wote linatazamwa sambamba klabu yake hiyo, so simply messi ni barca na barca ni messi tangu alivyoanza kuwa vibrant baada ya akina Gaucho kutoka kwenye timu hiyo. Bado hajafanikiwa sana kama hao wawili niliowataja na naamini ukiuliza deni kubwa alilonalo atataja ni la kutoibeba Argentina. Magwiji wengi wamefanya hivyo katika nchi zao. Samatta, Zidane, Gaucho, Maradona, Buffon, Maldini (Baba na Mtoto) and the list goes on.
Basically kwa nafasi zao ndani ya uwanja hawawezi kufanana kwa lolote kwa hiyo mchango ndo utawabeba na reflection ni mafanikio ya jumla.