Meya afika kwenye madanguro Mwananyamala, Wadada wanaojiuza wakimbia

Meya afika kwenye madanguro Mwananyamala, Wadada wanaojiuza wakimbia

Biashara ya ngono haiwezi kuisha kamwe, Meya atafute kazi nyingine za kufanya ili kulisaidia Jiji.
 
Wacheni kujisumbua kwa kuwasumbua wanao uza miili yao. Mnajua sheria zinasemaje? Kulingana na sheria za adhabu (penal code) adhabu ya mtu anayeendesha danguro haizidi Tsh 500 za kitanzania.

Bwana wetu mpendwa Yesu Kristo alipoulizwa na wanafunzi wake kwa nini hawachukulii hatua watu kama hawa alisema... 'Acheni magugu na ngano vimee pamoja'...
 
Kufuatia ongezeko la madanguro katika maeneo ya Kinondoni, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge amefika kwenye maeneo ya kunapodaiwa kufanyika kwa biashara ya kuuza mwili maeneo ya Mwananyamala na kuahidi kuchukua hatua dhidi ya wamiliki wa nyumba zinazotumiwa katika biashara hiyo.

Amesema: “Ukiacha danguro hili la Mwananyamala Mianzini kuna sehemu nyingine kama Tandale Uwanja wa Fisi na kuna Msasani Mikorosini na taarifa zinasema yapo mengi.

“Watendaji wetu wamepewa kazi ya kuhakikisha wanapata idadi kamili ya madanguro katika Kata zetu 20 na Mitaa 126.”

Ameongeza kuwa watawaita wenye nyumba wote kujieleza kwa nini wamegeuza nyumba zao kuwa madanguro, na kuwa biashara ya kujiuza inaanzia 2,000 hadi 10,000.

“Mipango mingi hairuhusu kinachofanyika, jambo hili siwezi kulifanya peke yangu, lazima Serikali Kuu iingilie, sheria lazima ifuatwe, hatuwezi kuacha jamii iendelee kuangamia.

“Tunasema tupambane na maradhi hasa magonjwa ya ngono kwa hali hii,” amesema Meya na kuongeza:

“Zipo taarifa zisizo rasmi hawa watu (dada poa) wanajipanga na kutoa fedha kwenye baadhi ya mamlaka zinazotakiwa kuzuia hii biashara, hatuwezo kuona Watoto wetu wanakua huku wanaangalia hiki kinaendelea, wataacha kusoma na kuamini hii ndio biashara stahiki.”

Amesisitiza kuwa wenye nyumba wanatakiwa kujitokeza na ambao hawatajitokeza nyumba itataifishwa na Serikali.

Naye Diwani wa Kata ya Makumbusho, Mohamed Mohamed amesema wameita wenye nyumba kuwauliza sababu za nyumba zao kuhusika katika biashara hiyo, lakini wakadai kuwa wale ni wateja wao wa kawaida na kuhusu wanachokifanya ndani hawawezi kuwaingilia.

Dada mmoja ambaye alijifungia ndani na kusikika sauti tu alisema “Watoto wenu wanakula, wa kwangu je, mnataka wale wapi?”

Nao baadhi ya Wateja waliohojiwa walisema kuna changamoto kadhaa wanazokutana nazo ni kufanyiwa fujo, kuibiwa vitu vyao na kushambuliwa hasa kama ukiwa si mwenyeji wa eneo husika.

Chanzo: ITV & Global TV
Itataifishwa kwa sheria gani?? Hebu fatilia mambo ya maana kama migogoro ya ardhi.usafi hususani wa matope mazito machafu madimbwini yanayopelekea kinondoni inanuka .mifumo mibovu ya vyoo.kuondoa makazi m'abonden.Haya mambo ya kufatilia watu wazima kutiana ni kutafuta kiki
 
Wacheni kujisumbua kwa kuwasumbua wanao uza miili yao. Mnajua sheria zinasemaje? Kulingana na sheria za adhabu (penal code) adhabu ya mtu anayeendesha danguro haizidi Tsh 500 za kitanzania.
Bwana wetu mpendwa Yesu Kristo alipoulizwa na wanafunzi wake kwa nini hawachukulii hatua watu kama hawa alisema... 'Acheni magugu na ngano vimee pamoja'...
Lete hicho kifungu.
 
Yakifungwa CCM Itapoteza wapiga kura wengi maana wengi wao ndo wateja wao halafu kuna hii kitu ya ubakaji..lile jiji linawashamba wengi na madomo zege lazima yaingie mtaani kusaka watoto kwa nguvu...macheni ikifungwa kula K ya 2000 na kitanda safii labda awe mkeo 🤣🤣🤣
 
Kuna vingi vya kufatilia maendeleo ya wananchi cha ajabu wanafatilia vitu vidogo tu hvyo... hao madada kwanza wanasaidia vitendo vya ubakaji visiwepo.. alafu pia ni starehe za watu ya nn kuwaingilia watu starehe zao
 
Aache kupoteza muda na kuumiza kichwa kwa vitu ambavyo kamwe hawezi kuvizuia...ni suala ambalo liko nje ya uwezo wake....inahitajika jamii nzima na serikali yote kuingilia kati.Mizizi ya hili tatizo iko mbali sana....kuanzia masuala ya kiuchumi na malezi..

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Watu wa daressalam ni wapuuzi sana wananunua malaya wachafu
Mbona unatujumlisha watu wa Dar wote ilhali hii biashara ni world-wide? Na kama ni uchafu mbona hata wewe ni mchafu kama unabisha tia kidole njia yako ya haja kubwa halafu nusa usikie kama kuna harufu ya udi.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mwenyewe anaishi maeneo ya pale meridian (masai club) asivunge itakua kawapitia tu.
Ukipita buibui guest house unashuka chini, kajenga bwawanii ... sjui kibali pale alikipate cha ujenzi
Sema wakati wa mvua anaipataga tabu sana

Ova
 
Back
Top Bottom