Meya afika kwenye madanguro Mwananyamala, Wadada wanaojiuza wakimbia

Meya afika kwenye madanguro Mwananyamala, Wadada wanaojiuza wakimbia

Bora hao wanaofuata mbele, pigeni vita ushoga!
Kufuatia ongezeko la madanguro katika maeneo ya Kinondoni, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge amefika kwenye maeneo ya kunapodaiwa kufanyika kwa biashara ya kuuza mwili maeneo ya Mwananyamala na kuahidi kuchukua hatua dhidi ya wamiliki wa nyumba zinazotumiwa katika biashara hiyo.

Amesema: “Ukiacha danguro hili la Mwananyamala Mianzini kuna sehemu nyingine kama Tandale Uwanja wa Fisi na kuna Msasani Mikorosini na taarifa zinasema yapo mengi.

“Watendaji wetu wamepewa kazi ya kuhakikisha wanapata idadi kamili ya madanguro katika Kata zetu 20 na Mitaa 126.”

Ameongeza kuwa watawaita wenye nyumba wote kujieleza kwa nini wamegeuza nyumba zao kuwa madanguro, na kuwa biashara ya kujiuza inaanzia 2,000 hadi 10,000.

“Mipango mingi hairuhusu kinachofanyika, jambo hili siwezi kulifanya peke yangu, lazima Serikali Kuu iingilie, sheria lazima ifuatwe, hatuwezi kuacha jamii iendelee kuangamia.

“Tunasema tupambane na maradhi hasa magonjwa ya ngono kwa hali hii,” amesema Meya na kuongeza:

“Zipo taarifa zisizo rasmi hawa watu (dada poa) wanajipanga na kutoa fedha kwenye baadhi ya mamlaka zinazotakiwa kuzuia hii biashara, hatuwezo kuona Watoto wetu wanakua huku wanaangalia hiki kinaendelea, wataacha kusoma na kuamini hii ndio biashara stahiki.”

Amesisitiza kuwa wenye nyumba wanatakiwa kujitokeza na ambao hawatajitokeza nyumba itataifishwa na Serikali.

Naye Diwani wa Kata ya Makumbusho, Mohamed Mohamed amesema wameita wenye nyumba kuwauliza sababu za nyumba zao kuhusika katika biashara hiyo, lakini wakadai kuwa wale ni wateja wao wa kawaida na kuhusu wanachokifanya ndani hawawezi kuwaingilia.

Dada mmoja ambaye alijifungia ndani na kusikika sauti tu alisema “Watoto wenu wanakula, wa kwangu je, mnataka wale wapi?”

Nao baadhi ya Wateja waliohojiwa walisema kuna changamoto kadhaa wanazokutana nazo ni kufanyiwa fujo, kuibiwa vitu vyao na kushambuliwa hasa kama ukiwa si mwenyeji wa eneo husika.

Chanzo: ITV & Global TV
 
Bora hao wanaofuata mbele, pigeni vita ushoga!
Safi kabisa.
Wangekamata Ile misengeh ya kitambaa cheupe ningewapongeza. Wanaogopa Ile midume wanaonea wanawake kwasababu hawajui karate.
 
Akili yako na ya huyo mteja Ni mbovu.
Kwani bar ukiwa huna pesa unahudumiwa?
Relax man don't take everything serious especially here in jf
"hili nalo mkalitizame" ni kauli pendwa ya mheshimiwa Hangaya ume comment kwa kukurupuka.
 
Huyo Meya kakosa kazi za kufanya.
 
Kama anataka jela zijae Kwa kesi za ubakaji afunge hayo madanguro ataona
 
Naye RC wa dar kaamua kumuunga mkono mega🤣🤣🤣🤣🪑
 
Back
Top Bottom