Hapo kwenye suala la siasa safi na chafu ndio tatizo linapoanzia, tumeshaona mara nyingi wakisema hawataki siasa za matusi huku aakigoma kuyataja hayo matusi yenyewe, au ni nani mwenye kipimo cha tusi ni lipi, na lipi sio tusi.
Hapo ndipo nilipopatilia shaka mpaka nikaweka neno "kukomoana" naamini hili jambo lipo tu kwenye vichwa vya watawala, kwao popote anapoingia mpinzani hata kwenye hoja ya msingi lazima watafute vikwazo, kule bungeni kuna hoja nyingi za maana huwa zunapigwa teke na CCM kisa tu zimetolewa na wapinzani.
Hiyo ndio sababu yangu kuhofia madai ya wafanyabiashara nayo kuja kupigwa teke mbele ya safari, kwasababu tu ya msukumo unaotoka upande wa upinzani kwa sasa, japo wengine kwenu mnaliona jambo la kawaida kwasababu athari zake zinaweza zisiwaumize nyie kwa namna yoyote.