Meya Songoro: Tumeshindwa kupambana na Biashara ya Ukahaba, tutaomba ihalalishwe wasajiliwe

Meya Songoro: Tumeshindwa kupambana na Biashara ya Ukahaba, tutaomba ihalalishwe wasajiliwe

FEBRUARY 22 , 2023 BARAZA ROBO YA PILI MANISPAA YA KINONDONI DAR ES SALAAM TANZANIA


Aomba waziri Dr. Dorothy Gwajima aingilie kati asema meya Manispaa ya Kinondoni Mh. Songoro Mnyonge kwani mambo ni mazito mtaani.
Source : KMC OnlineTV
 
Kukusanya kodi kwenye chanzo kipya sio lazima uwe umekosa hela.

Fikiri upya na uweke siasa pembeni, Meya yuko sahihi sana ila mkwamo utakuja kwenye ule utamaduni wetu wa ustaarabu na hatukuwahi kufanya jambo kama hili.

Mambo ya Serikali kuishiea au kutoishiwa hayana maana hapa.
Huwezi kukusanya kodi kwenye chanzo haramu,hilo hata yeye anajua,anakuwaje yuko sahihi wakati anajua utamaduni na ustaarabu wa Tanzania hauruhusu na yeye ni Kiongozi? kusema Serikali imeshindwa kudhibiti kwahio iruhusu huo ni uhuja,kesho watasema serikali imeshindwa kudhibiti ujambazi kwahio tuwaruhusu?

Kama ni maoni yake binafsi sawa,ndio maana tunasema katiba mpya muhimu ili apeleke maoni yake yafikiriwe
 
Hiyo ni too primitive
Ikifikia hatua Serikali ikahitaji kukusanya kodi itatafutwa namna ya kuchaji kodi digitally na watoza kodi watajifunza kwenye nchi ambazo tayari zinatekeleza hili jambo.


Hela ya hapo ni nje nje alaf ni uhakika sana[emoji23][emoji23]
Ndo kwanza tunapambana na kurasimisha wafanyabiashara rasmi kidigitali wasiweze kukwepa kodi, malaya tutawaweza vp? Unathibitisha vp kuwa hapa anatoa huduma kwa mpenzi na hapa anauza? Labda utenge maeneo rasmi ya kuwauza na kwa watz tulivyo wanafiki hutaona mteja hata mmona ila watauziana, serikali itakutana na condom tu zilishatumika.

Halafu wakifika mauzo ya m100 na zaidi wanaungwa VAT?
 
Serikali si washikaji wenzetu.
Swala dogo sana kukomesha ukahaba kwanza kuna njia mbili hapa naziona.
Nchi iongozwe kwa misingi ya dini ya kiislamu.

Au wafunge bar, casino,club, saloon zenye huduma ya massage nadhani hapa watakuwa wamefika hata asilimia 70.

Serikali haiwezi kusema imeshindwa kuthibiti ukahaba ilo nakataa kabisa sema kwakuwa wanunuzi nao wako serikalini inakuwa ngumu sana kuwa na mikakati thabiti.

📌 Jiulize hao makahaba pindi wanapokamatwa mbona wanaonga pesa na wanatolewa. Afu kufanya kazi ya ukahaba ni upungufu wa MAARIFA afu akili chenga.

📌 Wasichana wanatoka mikoani kuja dar kufanya shughuri za ukahaba mwingine anakuja kujificha bar kwa ni mhudumu wa bar kumbe anauza sangara.

Wanakataa kuuza karanga wanaona wauze miili yao .
 
Serikali si washikaji wenzetu.
Swala dogo sana kukomesha ukahaba kwanza kuna njia mbili hapa naziona.
Nchi iongozwe kwa misingi ya dini ya kiislamu.
Halafu wakristo wahame nchi? Wazo la kishamba sana. Hayo mawazo mengine sawa.
 
Tuwe wa kweli tuache kudanganya a kujivika vitu ambavyo hatuvifwati
Hii nchi mpaka Leo tunajiita wa jamaa tunafuata Sera ya jamaa na kujitegemea ni uongo tuwe wa kweli sisi ni mabepari Tena tusioeleweka
Tunajidai tuna utamaduni wetu. Ni uongo kwa Sasa hatuna utamaduni wowote hata atujielewi ni utamaduni gani Tena tunao kila mtu na lwake
Hata ukiiangalia tuna KATIBA na sheria, zetu tulizojiwekea kama nchi lakini zinavunjwa kivyovyote ili mradi maisha yanasonga
Ni mbaya iwapo itaharalishwa lakini Hakuna namna kama wapo wanajiuza na wapo mipaka yote tunawaona na wengine SASA TUNAENDA KUGONGA mipaka 50?!!hii biashara tunaiona imeshindikana vipi kuzuia mipaka yote hip?!?
Tusidanganyane hii biashara imeruhusiwa ila kwa siri waache wafanye kazi kihalali walipe kodi na Wawe na maeneo yao maalumu, wasitawanyike ovyo ovyo majira Hakuna,
Malaya wapo Enzi na Enzi
 
P
Hivi kwa akili ya kawaida serikali huwa inashindwa jambo? Hayo ni maneno yake binafsi, huenda na yeye ni mteja, nashauri 2025 apumzike awaachie kazi wanaoweza
Mkuu,Serikali ni Binadamu sio Mungu,hata Serikali za mataifa makubwa kuna mambo mengi tu bado wanahangaika nayo na hakuna dalili ya kuyamaliza,

Mambo kama Ugaidi,wizi,mauaji...bado vinaisumbua Dunia.
 
Back
Top Bottom