Meya Songoro: Tumeshindwa kupambana na Biashara ya Ukahaba, tutaomba ihalalishwe wasajiliwe

Hivi kwa akili ya kawaida serikali huwa inashindwa jambo? Hayo ni maneno yake binafsi, huenda na yeye ni mteja, nashauri 2025 apumzike awaachie kazi wanaoweza
Unaishi nchi gani? Umeme na maji kwako yanapatikana 24/7/365?
 
yaani Songoro kama baba wa familia anarudi nyumbani jioni anatazama taarifa ya Habari kwenye tv, wanarusha Habari yake alafu wanae wanatazama alichoongea ni hiki! Mama Samia, CC ya chama chenu ifanye uamuzi kwa huyu mtu.
 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni amesema Wameshindwa kupambana na Biashara ya Ukahaba hivyo Wataomba Ihalalishwe na Wasajiliwe Kabisa

View attachment 2528343

Chanzo: Jambo TV
Ukahaba unaitwa biashara,dah,humanity can't be more immoral.Si afadhali kujifanya kama haupo,kuliko kuuhalalisha.Sasa ukikusanywa hela halafu ukaitumia,si unaletea nchi laana.Hiyo ni hela chafu jamani.Yaani watu wamekuwa waovu kiasi kwamba hawajui uovu ni upi na wema ni upi.Very sad indeed.
 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni amesema Wameshindwa kupambana na Biashara ya Ukahaba hivyo Wataomba Ihalalishwe na Wasajiliwe Kabisa

View attachment 2528343

Chanzo: Jambo TV
Huyo ajiuzulu. Bila shaka kesho atakuja na kusema wameshindwa mashoga nao wasajiliwe.
Kuna. Maovu yalikuepo tangu kuumbwa dunia na binadamu wanachotakiwa ni kukataa. Meya kama huyo hawezi kwa sababu mwenyewe ni muovu.
Hawezi tu kusema wizi, ulaji rushwa, uzembe vimeshindikana kwa hivyo viruhusiwe.
Kauli ya huyu meya ni dhihirisho tunao viongozi waovu kiasi gani.
Huyu ajiuzulu mara moja.
 
Jamii yetu haijafika huko mnakolazimisha tuende. Eboo. Bongo kuna ukahaba au maigizo tu !!?
Wawezeshe kwa mitaji hao wanawake unaoita makahaba kama utawaona huko
Mkuu
Tanzania karibia miji yote Sasa Ukahaba umekubuhu.

Nenda Shinyanga, rudi Mtwara, potelea Sumbawanga na Mpanda, Arusha, Moshi, Songea achana na miji mikubwa huko ndio mamaaaa.

Kifupi ni bora itafutwe namna ya kuregulate kuliko hali mbaya tulioko Sasa.
 
Pombe ni halali?sigara ni halali? Na mbona wanakusanya kodi nyingi tu,uhalali na uharamu wa kitu ni mitazamo binafs tu ya jamii husika,
Kwa sheria zetu kunywa pombe au kuvuta sigaraTanzania sio kosa,ila Ukahaba ni kosa Kisheria,na kwa mtizamo na utamaduni wa wetu halikubaliki.

Ndio maana nikasema kama ni Maoni yake binafsi apeleke maoni kwenye katiba mpya
 
yaani Songoro kama baba wa familia anarudi nyumbani jioni anatazama taarifa ya Habari kwenye tv, wanarusha Habari yake alafu wanae wanatazama alichoongea ni hiki! Mama Samia, CC ya chama chenu ifanye uamuzi kwa huyu mtu.
Huyu ni wa kuondolewa haraka,hafai
 
Namna ya kukabiliana na tatizo ni kutoa mitaji kwa vijana wajiajiri,Lowassa alishasema miaka kama 10 iliyopita kwamba ukosefu wa ajira kwa vijana ni Bomu linalosubiri kulipuka,ndio haya sasa matokeo.

Wengi wanaingia huko sio kwa kupenda,ni shida ndio inawalazimisha
 
Kweli we ni Weed!
 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni amesema Wameshindwa kupambana na Biashara ya Ukahaba hivyo Wataomba Ihalalishwe na Wasajiliwe Kabisa

View attachment 2528343

Chanzo: Jambo TV
Jamaa yangu anayake je kuna kosa jipya duniani? Mauaji,madawa ya kulevya na makosa yote ikiwemo linaloibuka sasa hivi la ushoga mm pamoja na kuyakemea bado yanaendelea kwa dhana yake tuyaridhie sbb haikomi?

Sina la kumsemea huyu zaidi anatueleza kachoka

Anasema magereza,police na mahakama kunasiku zitafungwa
 
Sasa watu wanaojiuza wanavijiwe vyao mnatangaza kama mmewashindwa je mtawaweza majambazi,wahalifu wa mtandaoni nk mtawaweza? Maana hao hawajulikani maficho hao
Ingekua enzi hizo angeenda kwa pilato kufafanua kauli yake

Angeitwa na polepole akafafanulie watanzania
 
Umetaja dini gani eti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…