Meya wa Jiji la Dar kuzindua kinachoitwa 'Chawa wa Mama'

huwa nadhani huu ukumbi ni maalumu kwa mambo ya msingi. kumbe hata kwa mambo ya kipumbavu namna hii!!
 
Kwakweli hii inadhihirisha ni jinsi gani tupo mbele ya ujinga kuliko ujinga wenyewe

Usishangae sana kaka hiyo ni version mpya ya wale buku 7 wa awamu ya 5

MAMBUZI WANA MBINU NYINGI ZA KUTAFUTA SHAMBA LENYE MAJANI LAINI

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Yaani Meya wa Jiji mama anakosa ubunifu kiasi hiki? Huyu ni zao la Elimu duni CCM waliwekeza.
Haiwezakani kabisa Meya na ndevu zake anaenda kuzindua kampeni ya kijinga hata mwanangu wa darasa la pili hawezi kuwaza kijinga namna hii, No wonder jiji limejaa uchafu kila kona, kumbe tuna Meya kiazi namna hii
 
Mi naombea wazindue hao machawa ili CCM ife rasmi,na tarehe 21 Chadema wawapige vilivyo kwenye uzinduzi wa Kampeni,huku mtaani mambo ni magumu sana hakuna wa kusema wala kutenda,Leo watu wanajikusanya ili kuwa machawa wa Samia.

Sasa acha wazinduliwe hao machawa,najua ndio hao watakuwa wanamtetea mama yao akipigwa Spana na upinzani, Kwanza machawa akili zao zinaendeshwa na matumbo,badala ya kujibu hoja wao watakuja na vioja ndio hapo anguko la Samia na CCM litakapoanzia,enzi za kuzomewa mtaani zinawarudia.
 

Bila shaka mwenyekiti wao atakuwa ni sitivu nyerere
 
Umeandika kwa hisia za juu Kama mlima Kilimanjaro
 
Upuz mtupu,waingie barabarani wakafanye usafi huko nako ni kutawaonesha wanamuunga mkono
Rais

Ova
kuunga mkono ni kitu tofauti , hawa ni chawa , yaani wanataka kula mgongoni mwa mama
 
Ujinga mtupu! Tayari hayo ni matabaka katika chama na serikali. Wengine wataonekana wa hovyo. Kuna walimu viherehere waliwahi kutaka kuunda jukwaa la walimu wazalendo enzi za JPM Bashiru amawapiga marufuku kuwa wanataka kuleta mgawanyiko. Mama naona anakumbatia sumu itamuua
 
Hao chawa unakuta wananuka madeni kila mahali kutokana na ugumu wa maisha.

Nauli ya kufikia eneo la tikio wamekopa.

Maji waliyotumia kuoga wamechota kwa jirani.

Ukosefu wa ufahamu ni tatizo kubwa sana kwa sasa ingawa Mbwembwe kibao.
Huo ndo mtaji wa chama cha mambuzi
 
Chawa ni parasite, anaishi kwa kificho.
Hebu jaribu kufikirisha akili, tafuteni jina lingine.
Naamini chama kina watu smart..
 
Hii topic sidhani kama inamuhusu Mwendakuzimu lakini hata yeye alikuwa na chawa wengi sana ila kwa majina tofauti, wengine wapo humu JF wanapambana kulinda 'legacy' yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…