Mfahamu Amou Hadji, Binadamu mchafu zaidi Duniani

Mfahamu Amou Hadji, Binadamu mchafu zaidi Duniani

Msamiati

R I P
Joined
Mar 6, 2011
Posts
1,063
Reaction score
700
Amou Haji Mzee wa zaidi ya miaka 75, Raia wa Iran, ndio Binadamu anayeshikiria rekodi ya kuwa Mwanaume mchafu zaidi duniani. Haji amekuwa na matatizo ya kisaikolojia kwa kujengewa imani tangu utotoni mwake kuwa, kitendo cha kusafisha mwili wake kitamsababishia maradhi.

Haji Hakubaliani kabisa na kunywa maji safi, na anachukia kabisa apoletewa habari za kuoga. Uchafu huu haujaishia tu kwenye usafi wa mwili wake, bali umeenda mbali zaidi kwa mzee huyu kuamua kuishi ndani ya shimo.

Chakula cha Haji ni Nyama zilizo oza lakini pia anatumia sigara zinazotengenezwa kwa vinyesi vya wanyama. Kitendo cha binadamu mchafu zaidi kuwa Mwanaume, kinafanya wanaume tuzidi kumulikwa zaidi kwenye swala la usafi wa miili yetu, mavazi na ushiriki wetu katika usafi wa mazingira.


1.jpg

2.jpeg
3.jpg
4.jpeg
 
75 years..... takwimu zinasema kaumwa mara ngapi? kama afya yake ni bomba hongera yake
 
Iran!?Atakuwa alifunzwa kuwa akiwa msafi atafanana na "Wamarikani"!Bado nacheeeka....!
 
yani bacteria hawawezi mdhuru aiseee loh.. sipati picha maeneo yale loh
 
Sawa fanya utafiti utuletee mtu mwingine ambaye hajaoga miaka 60 kama huyu ili tusiseme huyu ni mtu mchafu zaidi dukani
 
filthiest...75...and still kicking....
 
Back
Top Bottom