Mfahamu Carlos the Jackal: Gaidi tishio zaidi kuwahi kutokea duniani

Asante mkuu kwa elimu nzuri uliyotupa....kingine kumbe tezi dume haichagui rais wala gaidi,maskini wala fukara aisee na mie ngoja nikacheck kabla haijanitokea duh.
 
Kwa maoni yangu aliharibu pale akipoamua kubadili dini
Hizi dini ndugu yangu zina mambo mengi sana na ukizifuatilia sana unaweza kuja changanyikiwa. Umeshawahi kujiuliza kwanini wamarekani weusi wengi hubadili dini na kuwa waislamu wakati walizaliwa na kukulia katika ukristo? Ulishawahi kujiuliza kwanini mzee Fidel Castro haamini katika dini?
 
H
Ndo yule wa kwenye novel ya "The Day of the Jackal"?

Hapana, yule wa kwenye novel alikuwa ni mwingereza jina lake la mwanzo nimelisahau lakini la pili ni Cathlope. He was a professional asassin i.e anafanya mauuaji kwa kulipwa, hakuwa na itikadi za siasa za magharibi wala mashariki.
 
Alitalikiana Na mke wake mwaka 1997 akiwa Gerezani French, ila mwaka 2001 alimuoa Mwanamke mwingine akiwa Gerezani ambaye alikua ni Lawyer wake!
 
Kuna story mtaani kuwa aliwahi ingia kwa malkia eliza, akala vyombo kisha akatokomea kupitia tundu la choo,, maana alimkuta malkia yuko bafuni anaoga. Hii ilikuwa ni kweli au chai tu?
Chai tu hii.
 

Muonekano wa Carlos the jackal sasa hivi..


-Alifanikiwa kuzaa watoto wawili wa kike, 1. Elba Rosa Ramirez 2. Sonia Marine Oriola
-Huyu Elba Rosa yupo ujerumani katika mji wa Neu Ulm
-Hakuna ambae imesikika amefata nyendo za baba yake
-Mke wake alifariki mwaka jana 2015
-Mke wake wa sasa ni aliekuwa mwanasheria wake Isabella Countant Peyre
 
Hawa wote nilishawasikia kasoro MICHAEL SAVIMBI.
 
Kuna story wakati nakuwa niliisikia kwenye vibanda umiza,eti huyu bwana Carlos alishawahi kuingia kwa Queen wa UK,wakati anatoka ndiyo wakajua alikuwa ni yeye??Ni kweli?
 
Unapomuongelea Carlos usiwasahau pia vikundi alivyoshirikiana navyo katika ujasusi wa dunia enzi hizo kama Red Brigades cha Italy, Japanese Red Army ilokua chini ya Fusako Shigenobu na Kozo Okamoto pamaoja na Baader- Meinhoff cha West Germany kilichohusika na kuteka ndege ya Lifthansa hadi Mogadishu., vikundi hivyo vyote vilikua vinawapigania wapalestina kudai nchi yao toka kwa wazayuni, kutetea maxims, Maoism na communism.
 

mkuu pia nadhan unakumbuka Mandela kwa mabeberu pale SA alikua gaidi kwa wenzake alikua mwanaharakati na at last wakampa na Nobel Prize

ni kama udikteta, Gadafi, Mugabe, Asad, Sadam, Chaves, Castro, Kim Jon Un etc hawa kwa wamagharibi ni madikteta lakini kwao ni watawala bora na wanapendwa

ni katika kuhalalisha jambo basi majina kama gaidi au dikteta hutumika, usishangae mjomba Magu akiwabana wazungu ktk maslahi yao wasipumue ukaambiwa ni Dikteta anatumbua tu majipu bila kufata sheria, tukashawishiwa kuingia mtaani kumpinga yeye na chama chake kinachotawala tokea uhuru wapate mwanya kuweka watu wao watunze maslahi yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…