Mfahamu 'Kamchape' mkamata wachawi na shughuli zake kwa ujumla kutokea hapa Mkoani Kigoma

Hii ni hatari, hivi mkoa upi ni hatari sana kwa uchawi yaani wachawi wa huko ni wale wameshindikana kabisa kwenye haya mambo? Cc Mshana Jr
 
Hii ni hatari, hivi mkoa upi ni hatari sana kwa uchawi yaani wachawi wa huko ni wale wameshindikana kabisa kwenye haya mambo? Cc Mshana Jr
Hii ni ngumu kujibu ila naona wachawi wa ukweli wako Dar kwasababu Dar ndo mpango mzima. Kuna vita nyingi sana za kiroho huko Kkoo. Mikoa ambayo ni brands kali za uchawi ni Kigoma, Rukwa na Tanga. Tanga ni kama imepoteza mwelekeo kwenye tasnia ya uchawi. Sisikii kabisa matukio. Sumbawanga bado matukio yapo.. kuna jamaa yangu aliamka kakuta mdomo umepinda mazima.
 
WAKRISTO wameongezeka Tanga Ndiyo Maana uchawi umepungua
 
Ukiniuliza mimi nitasema mhusika wa kozi inabidi awe genius.

Anapitishwa kwenye kozi ya kuamua uhai wa watu kwa wiki zisizozidi 3 na anaelekezwa kuchanganya madude mengi mengi na hatarajiwi kukosea na yote anayakumbuka.

Darasani unafundishwa points za kwanini Wakoloni walikuja Afrika na unazunguka nazo for months only to forget them once you are in exam room
 
Ni elimua ya vitendo zaidi sio rahisi kusahau
 
Nimejifunza kitu,Kuna tukio liliwahi kutokea miaka mingi imepita, Mtaani alikuja huyo wakuitwa kamchape ipo nyumba jirani aliingia akatoa vitu live live bila chenga bahati mbaya mwenye nyumba hakuwepo nadhani alikuwa kwenye pilika walikuwa mabinti tu.
Sasa ndugu Kigoma Region Tanzania embu tuweke sawa nywele alimnyolea wapi na kuchanja utosi au walikuja kumalizana kivyao.
 
Hicho huwa ni kiapo cha kafara asimpo mfanyia hivyo basi muhusika huweza kurudia katika kazi yake kama kawaida.
 
Sasa asipofanikiwa kurudi inamaanisha amekufa ama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…