Habari wanajf,,, kama ulikuwa hujui kigoma kuna operation inayoendelea ya kutokomeza wachawi na imeruhusiwa na serikali,,
Hii ni operation inaendeshwa na watu kutoka kingo na niger pia sumbawanga (KAMCHAPE) hawa watu wako vizuri yaani wanafukua uchawi popote pale ulipo..... Iko hivi...👇👇👇👇👇
Hawa KAMCHAPE wanakuja kijijini hapo wanaomba ruhusa then mnawchangia 5000Tshs...
Wanapita kila nyumba kwa nyumba na huwezi kimbia kama ww ni mchawi,,, kwa mfano kijiji fulani cha uvinza a.k.a mlela village, kuna mchawi alijaribu kukimbia nyumba yake yaani alisafiri kabisa akaondoka lakini walimkuta amekaa nyumbani ndani kwake yaani kama kamwagiwa maji vile...
Na moja kitu ambacho wachawi walikuwa wakifanya walikuwa wanatoa madude yao ndani wanakuletea ndani kwako lakini KAMCHAPE akifika atajua hayo madude yametoka wapi na nani kayaleta...
Hawa jamaa wako vizuri kwa mfano kuna jamaa fulani mchawi alikutwa na madude yake katika hayo madude kuna kisu yule KAMCHAPE akasema hiko kisu kimeuwa watu mia moja 100 daaah watu walilia sana,,,,
Lakini pia KAMCHAPE wakishambulia kwako na kukuta na uchawi wanakunyoa na kunywesha dawa yao ambayo wanasema huwezi kuwa tena mchawi katika maisha yako yote,,,,,
Changamoto wanayokutana nayo KAMCHAPE ni pale watendaji wanapokataa kuruhusu hii operation katika sehemu yake kwa mfano kijiji cha mlela village wilaya ya uvinza mtendaji aligoma kusaini.... Ilikuwa ni fujo mtendaji alipigwa na kuchomewa nyumba yake na vitu vyake na wanakijiji wake wenye hasira kali ambao wamechoshwa na uchawi kijiji hicho,,,,, mpaka sasa operation imeisha sasa inaendelea katika vijiji vingine,,,,
Kiufupi hicho kijiji kilikuwa na wachawi... Kuna mchawi mmoja mpaka alifikia kujiita Mungu wa pili maarufu kama marehemu mzee Adamu, huyo mzee alikuwa nuksi kamuulize nyerere ile fimbo yake ilivyoibiwa kigoma,,, hilo tukio lilifanywa na baba yake mzee adamu,,,, huyo mzee alipofariki watu wakishangilia siku nzima usiku kucha nakumbuka hadi home tulichinja kitimoto kusheherekea na alikuwa nuksi upande wake,,,, mashamba yake watu walienda kuvuna mazao,,,,,
Hii operation ni babu kubwa nawapongeza sana wlioruhusu hii operation kufanyika kigoma,,,, aisee kigoma kuna uchawi ni balaa....
WATU HUACHA KAZI ILI KWENDA KUANGALIA WACHAWI WANAVYOTUMBULIWA KIUFUPI NI FURAHA KWETU TUNAINJOY SANA KAMCHAPE FANYA KAZI......