Mfahamu Mateso, mtu mwema wa Msasani aliyeuawa kwenye tukio la ujambazi Mikocheni jirani na Coca-Cola

Mfahamu Mateso, mtu mwema wa Msasani aliyeuawa kwenye tukio la ujambazi Mikocheni jirani na Coca-Cola

Heci

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Posts
3,591
Reaction score
6,114
Mateso au Meshach, mkazi wa Msasani mtaa wa Mikoroshoni, unashuka pale General Tyre, ulizia kwa John muuzà duka ambalo pia ni genge na bar.

Kiji bar cha John kinakesha 24/7, Msasani ikilala, kwa John pako live.

Kwenye kijiwe hiki ndio watendakazi wote wa Msasani hunywa wakikosa wateja viwanja. Pia kama umeibiwa na MTENDAKAZI wa mitaa ya Msasani, we nenda kwa John, mbona faster tu unampata mwizi wako. Awe ni Zabibu, Mourine,, Mwantumu, Mwmvita, Irene au MTENDAKAZI yoyote Yule, hapa ndio fungulia keba.

Mateso alikuwa ni MNYIHA WA MBOZI, Kijiji kimoja na Ester Mwampashe, mama Eliza mke wa Willy. Mateso alikuwa bonge la giant, handsome, mpole, mwenye haiba na kada maatufu wa CHADEMA.

Kuanzia Namanga hadi Msasani mwisho alijulikana Kama meneja wa bandari, hamna aliyemshitukia kuwa anapiga kazi za hatari.

Kuna kipindi inasemekana kuwa jamaa alijiteka, kumbe kuna wachina alikuwa anapiga nao dili, wale wachina wakampa begi limejaa pesa , wakamuuliza jamaa, huu mzigo wetu unaweza kutupelekea benki? Jamaa akajibu, “bila hofu”. Wachina wakamkabidhi jamaa begi, kumbe wamefanya ujanja, wamebasilisha begi, alilopewa sio Lile la kwanza, hili chini lilikuwa na makaratasi, juu hela kidogo.

Jamaa akatokomea nalo na Kisha kutangaza kuwa ametekwa, alipokaa na kutulia akagundua kuwa kumbe chini Kuna magazeti.

Mateso alikuwa mtu mwema akisaidia watu na chama pia. Siku moja kabla ya kuuawa kwake, alimuaga mkewe kuwa ana Safari, mke akamuandalia nguo kwenye lasket. Jamaa akaondoka.

Kumbe MATESO alikuwa amechora mchoro na mlinzi wa ghala la GSM Mikocheni jirani na Coca-Cola, akamshikisha mil 1.5 akamueleza na muda atakaokuja na crew Yake. Mateso akakubaliana na mlinzi kuwa watakaofika wakina MATESO watamfunga mlinzi makamba na kumlisha dawa za kulevya ambazo zitamlaza kwa siku mbili. Mlinzi alikubali, lakini akaenda Polisi kutoa taarifa.

Mateso alimtuma kijana aitwaye Mashaka, aende Biafra kukodi Noah, akalamba elfu 40 kwa kazi hiyo.

Usiku MATESO akiwa na wenzake sita Ndani ya Noah, bunduki moja na mitungi miwili ya gesi kwa ajili ya kuvunjia wakawa wanaelekea eneo la kazi.

Jirani na ghala la GSM, kulikuwa na Vitz inabadilishwa tairi. Kina MATESO walipofika, wakashuka na vitendea kazi vyao. Mara kutoka upande ilipoegeshwa ile Vitz, ikapigwa risasi hewani.

Kina MATESO wakajibu, kumbe nyuma yao Kuna difender nne ziko full loaded zinakuja. Jamaa wakamiminiwa risasi za kutosha, akabakizwa MATESO peke yake. Polisi wakamchukua na kwenda kufanya naye mahojiano. MATESO akauliwa kesho Yake.

Ilichukua zaidi ya siku kumi na nne kupatikana kwa mwili wa MATESO. Mateso alisafirishwa na kwenda kuzikwa kwao MBOZI.

MATESO ndio walewale, TUMUGOJE, TUMULESHE? Maana Yake, tumuue au tumuache?

Karibuni Msasani makazi rasmi ya Malaya, matajiri, majambazi, mateja na vibaka.
 
Mateso simjui hanijui..ila anaonekana alikua anafanya ujambazi local sana, na wa kizamani mno. 1.5 kwa mlinzi wa GSM its a peanut. Vitz wakati wa tukio ni wake up call!

Mateso kafa inaonekana kataja vibaka tu hakuna jambazi mwelewa atafanya kazi na mtu wa kariba ya mateso....

All in all, anifurahisha kuwa mtu wa watu na kada wa CHADEMA Ilikua inamuondolea suspicions. Pia inaonekana alikua family man.

Wangemueleza sku hz watu hawaibi na magari, its too risk. Kungekua na piki piki baadhi wangepona nd live to tell the Tale but now, Dead Men tell no Tale.

RIP Mateso, only GOD can judge you!
 
Mateso simjui hanijui..ila anaonekana alikua anafanya ujambazi local sana...na wa kizamani mno...1.5 kwa mlinzi wa GSM its a peanut..vitz wakati wa tukio ni wake up call...!

Mateso kafa inaonekana kataja vibaka tu hakuna jambazi mwelewa atafanya kazi na mtu wa kariba ya mateso....

all in all...kanifurahisha kuwa mtu wa watu na kada wa CHADEMA Ilikua inamuondolea suspicions..pia inaonekana alikua family man.

wangemueleza sku hz...watu hawaibi na magari...its too risk kungekua na piki piki baadhi wangepona...and live to tell the Tale but now...Dead Men tell no Tale.

RIP Mateso...only GOD can judge you!
Nomaaaaa hakujiongeza

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Mateso hyu ndio ana ghala la kusafirisha mizigo kwenda Mbeya na iring pale Mnazi mmoja lumunba?

Kwa maelezo yako kama yy maana nae ni wa MB.
 
Back
Top Bottom