Mfahamu "Mkandala Rufufu" mzee wa kukotola

Mi siyo muangaliaji wa muvi,ila jina la Lufufu,ni maarufu sanasana kwani huwa nasikia watu wanaoingiziwa muvi,wanamtaja sana.
 
Mtu mzima unaanzaje kuangalia movie iliotafsiriwa kwa kuingiza sauti? Hizo movie huwa naona hazina tofauti na katuni za watoto za akina Kibena.
Mimi hapa ndipo uwa namkumbuka marehemu baba yangu. Alituwezesha kutokuwa na hitaji la kwenda kwenye vibanda kuangalia video na hata hawa akina Mkandala and the like nimekuja kuwajua kupitia hapa JF kwamba wapo au walikuwepo wakitafsiri muvi. Hata hivyo natambua kuangalia muvi za aina hii kunakuwa na raha yake kwa rika husika.
 
Pole sana mkuu yan ninyi ndo wale watoto wa tumbo kubwa na miili ya mkate 😂😂 hamkupata bahati hata ya kwenda kwa jiran kupata mambo ambayo kwa utoto wetu yalikuwa mzuri sanaaa.
But background ndo zinatu shape
 
Wapeeeeenzi watazamaji ndugu zangu wapendwaa

Kwa mara nyingine tena mkandala lufufu library iliyoopo Yombo kwa limboa inawaletea movie kali kabisa ya deadly pray

Imetafsiriwa na captain Gasper Mkandala lufufuuuuuu wako
Watu wengi hawajawahi kujua kama comando kipenzi inaitwa deadly prey huyu rufufu alikua hatarii sana.
 
Sir Name ya kihaya mukandala kama yule prog mukandala wewe zombi unamuita mhaya very pathetic

Hata hayo maneno aliyonuwa ananigesha kama kumiminawani (kumwaga kahawa) kanyampasira (kijambio )na nk huyu alikuwa mhaya typical hata ongea yake wewe bwashee unamuita mchaga upate sifa za kipumbavu

USSR
 
Enzi hizo miaka ya 90 nilikuwa nakaa mbagala kwa mangaya, ni jirani na kwa limonga justin wa limonga ambaye nadhani ndio alikuwa mfadhili wa lufufu.
Jamaa alikuwa charming sana nakumbukuka alikuwa akipita pale mtaani tulikuwa tunamshangalia lufufu...lufufu amevaa kofia ya cowboy.
Ananunua machungwa tunakula, na sehemu alipokuwa akitasfiri hzio movie ni mbagala hapo hapo kwa limonga. Ilikuwa raha sana maana ukiwa na shiling 20 unaangalia trailer na movie moja matata ya anord la jini hahahaha..way back
 
Hapana mkuu lufufu alikuwa ni mchaga kabisa na mama mhaya Huyu mzee mie pia nina mfahamu vzr sn ila yeye alikulia upande wa mama ambaye ni mhaya so alipoanza kazi zake akaona atumie maneno ya kihaya kwenye kuchombeza movie zake, ila lufufu ni mchaga baba na mama mhaya
 
Nikiwa mdogo niliangalia movie zake ila sijawahi kuzipenda maana maneno aliyokua anayatumia sikuwahi kuyapenda bila sababu niliona maneno ya hovyo tu ila nilikua naangalia hivyo hivyo maana ni stage ya ukuaji ambayo ilikua lazima niipitie

Badae nilikuja kumpenda sana Dj Afro wa Kenya hadi leo namkubali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…