Mfahamu "Mkandala Rufufu" mzee wa kukotola

Mfahamu "Mkandala Rufufu" mzee wa kukotola

Utaskia Lufufuuuu afu anamalizia Nkorombo Wajeba

Mzee wa mfumfulizo kwny six comando
Shankomela-kupiga sarakasi
Kinumbu au viazi ndio mabomu
Kumiminia mwanyu kupiga risasi
Afu alikua mtu akikabwa unaskia puupuuu eti ushuz 😂
Mguu wa Bata/ wakuku- bastora
Kupata Kanyamazongo- kizunguzungu

Jamaaa yangu hiyo ilikuwa Lugha ya kihaya....ww umetupiga Chai la kufa mtuuu
#Sio mfufulizo ni mpulutulizo mana yake kitanzi
#Kanyabazongo ni kizungu zungu.
#Sio nkorombo wabeje ni lukoma abambeija
#Sio kumimina mwanyu ni kumimina Mwani(Mwani kahawa)....nk-nk-nk-nk
 
Haya ni baadhi ya maneno yake ninayotakumbuka enzi anatafsiri

" akamweka kwenye kanyampasila"

"Na picha letu linaisha hapa, sterling wetu anapanda gari Aina ya chai maharage na kutokomea zake kusikojulikana"

Rufufu alikuwa anatafsiri picha Hadi kuna maneno ukisikia unajua kbs hii ni chai,Ila tulipokuwa na kujua kiingereza Kish atukazirudia zile picha tunakuja kugundua kwamba kweli zile tafsiri za rufufu zilikuwa ni chai😅😅
Akaenda kujisongobeka kwenye gari aina ya mfukunyu Mfukunyuuu ni magari yanayobeba silaha nzito nzito......#Ngoja nikasubale kwanza
 
Zamani pale kimara kituo cha polisi kulikuwa kuna ukumbi tunaangalia ssna hizi muvi za lufufu mkandala daaah kitambo sana
 
Kila adui akipigwa teke la uku utasikia “akampiga kwenye paakuchu!!” [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sasa anavyoisema hiyo “paakuchu” lazima banda zima mcheke [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna Adui Mmoja kwenye Tiger Cage ya Don Yen Lufufu alkua anamwita Mpika chips manzese baunsa flan mfupi
 
Katika Maadui ambao alkuwa anampatia sana ni Carlos Bill Drago alvyokuwa anamuigiza anavyoongea kiteja
Hii muvi ni ya kitambo ila niliipenda sana!

Bill drago ni yule jamaa aliyechomwa kisu kwenye kikao kwa kesi ya usaliti.

Carlos ni yule kipara mwenye nywele zilizomwagika mgongoni.

Ramon cota ndiye huyo teja unayemzungumzia..
 
Anaitwa Kapteni Gaspa Derrick Mkandala Lufufu, halafu mbele hapo kuna maneno ya kihaya alipenda kuyaweka Mnaokumbuka vyema Mtatukumbusha.

Baada ya kustaafu kazi ya Jeshi Lufufu aliamua kuanza kutafsiri picha (Movie) za kizungu nk. kwa Kiswahili, jina lake likawa maarufu hapa Nchini Tanzania huku akiwa mtu wa kwanza kabisa kuingiza maneno ya kiswahili kwenye mikanda ya video VHS.

Huyu muasisi wa MaDj wote unaowaona wanatamba hivi sasa alifariki Mwaka 2015 na kuzikwa Moshi Mkoani Kilimanjaro. Baba yake alikuwa Mchaga na mama yake alikuwa Mhaya.

Alikuwa akinogesha movie kwa maneno yake ambayo hatuyajui maana yake mpaka leo ila wapenzi watazamaji walimwelewa.

"Eeeee Tujuane wale wote wa vibanda umiza kipindi kileee tulio kuwa tukirudi tunafikia kwenye kichapo na maji ya baridi juu. watoto wa getini mtupishe kidogo "

Unaikumbuka muvi ipi kutoka kwa huyu mkali....View attachment 2242541
Fundi
 
"Naitwa captain Gaspar Derrick Mkandala a.k.a Rufufuuuuu"

Jamaa alikuwa mwongo sana Ila alijua kucheza na maneno Hadi muvi unaiona tamu

Lkn kwangu DJ Mark Mzee wa acheche production namkubali zaidi
Muongo sana...utoke kwa wasomi utaishije mjini bila maneno maneno mengi? 😂 😂 😂 😂
 
Anaitwa Kapteni Gaspa Derrick Mkandala Lufufu, halafu mbele hapo kuna maneno ya kihaya alipenda kuyaweka Mnaokumbuka vyema Mtatukumbusha.

Baada ya kustaafu kazi ya Jeshi Lufufu aliamua kuanza kutafsiri picha (Movie) za kizungu nk. kwa Kiswahili, jina lake likawa maarufu hapa Nchini Tanzania huku akiwa mtu wa kwanza kabisa kuingiza maneno ya kiswahili kwenye mikanda ya video VHS.

Huyu muasisi wa MaDj wote unaowaona wanatamba hivi sasa alifariki Mwaka 2015 na kuzikwa Moshi Mkoani Kilimanjaro. Baba yake alikuwa Mchaga na mama yake alikuwa Mhaya.

Alikuwa akinogesha movie kwa maneno yake ambayo hatuyajui maana yake mpaka leo ila wapenzi watazamaji walimwelewa.

"Eeeee Tujuane wale wote wa vibanda umiza kipindi kileee tulio kuwa tukirudi tunafikia kwenye kichapo na maji ya baridi juu. watoto wa getini mtupishe kidogo "

Unaikumbuka muvi ipi kutoka kwa huyu mkali....View attachment 2242541
Hayo maneno unayoyasema ni Mkandara lufulu "lukoma abambeija" maneno mengi aliyokuwa akitumia yalikuwa ni ya kihaya mfano

Nyugunyu ni nyonga
Kanyampasila ni sehemu iliyobana mfano cell au mahabusu
Akakoimoza ni akakimbia
Dawa aina ya ntale ye ilungu dawa inayopatikana porini sana
Bunduki aina ya ebitoke binura yaani ndizi tamu

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom