Mfahamu "Mkandala Rufufu" mzee wa kukotola

Mfahamu "Mkandala Rufufu" mzee wa kukotola

alikuwa akinikosha akiigiza sauti ya kike, amkumbuka kwenye movie la titanic
 
alikuwa anafanya makosa sema nchi yetu huwa haifuatilii mambo ya hati miliki za kisanii
Huwezi tafsiri kitabu au picha ya senema yeyote bila idhini ya mtunzi.
 
Anaitwa Kapteni Gaspa derki Mkandala lufufu, halafu mbele hapo kuna maneno ya kihaya alipenda kuyaweka Mnaokumbuka vyema Mtatukumbusha.

Baada ya kustaafu kazi ya Jeshi Lufufu aliamua kuanza kutafsiri picha (Movie) za kizungu nk. kwa Kiswahili, jina lake likawa maarufu hapa Nchini Tanzania huku akiwa mtu wa kwanza kabisa kuingiza maneno ya kiswahili kwenye mikanda ya video VHS.

Huyu muasisi wa MaDj wote unaowaona wanatamba hivi sasa alifariki Mwaka 2015 na kuzikwa Moshi Mkoani Kilimanjaro. Baba yake alikuwa Mchaga na mama yake alikuwa Mhaya.

Alikuwa akinogesha movie kwa maneno yake ambayo hatuyajui maana yake mpaka leo ila wapenzi watazamaji walimwelewa.

"Eeeee Tujuane wale wote wa vibanda umiza kipindi kileee tulio kuwa tukirudi tunafikia kwenye kichapo na maji ya baridi juu. watoto wa getini mtupishe kidogo "

Unaikumbuka muvi ipi kutoka kwa huyu mkali....View attachment 2242541
Akapigwa mpaka akasumbagila[emoji1787][emoji1787][emoji1787] nilikuwa napenda akiigiza sauti ya mwanamke au ya mtoto huyu jamaa ni legendary
 
Nikiwa mdogo niliangalia movie zake ila sijawahi kuzipenda maana maneno aliyokua anayatumia sikuwahi kuyapenda bila sababu niliona maneno ya hovyo tu ila nilikua naangalia hivyo hivyo maana ni stage ya ukuaji ambayo ilikua lazima niipitie

Badae nilikuja kumpenda sana Dj Afro wa Kenya hadi leo namkubali sana
Kama hukumuelewa Rufufu ata shule ulikuwa mzito[emoji1787][emoji1787]
 
Enzi hizo miaka ya 90 nilikuwa nakaa mbagala kwa mangaya, ni jirani na kwa limonga justin wa limonga ambaye nadhani ndio alikuwa mfadhili wa lufufu.
Jamaa alikuwa charming sana nakumbukuka alikuwa akipita pale mtaani tulikuwa tunamshangalia lufufu...lufufu amevaa kofia ya cowboy.
Ananunua machungwa tunakula, na sehemu alipokuwa akitasfiri hzio movie ni mbagala hapo hapo kwa limonga. Ilikuwa raha sana maana ukiwa na shiling 20 unaangalia trailer na movie moja matata ya anord la jini hahahaha..way back
Pale Kona la kwenda magenge ishilini, upande wa kulia ni kwa limonga, mbele Kuna baa ya mamboto ukiendelea mbele ni kwa serenge dah , we mkali
 
Mtafute Dj Afro alafu ulete mrejesho
"Naitwa captain Gaspar Derrick Mkandala a.k.a Rufufuuuuu"

Jamaa alikuwa mwongo sana Ila alijua kucheza na maneno Hadi muvi unaiona tamu

Lkn kwangu DJ Mark Mzee wa acheche production namkubali zaidi
 
Eeeeh kwa majina mi ni kaparo, hahahahahaaa.

Utacheka sana mpka usahau mbavu zako upate movie ya Jackie Chan imetiwa maneno na huyo dj.
Dj Afro amigos...

Mzee wa kulya mundu, makagari, saitung'i...

Kitambo sana niliwahi tazama muvi za huyu Mkenya,,,,,ni Comedy sana..
 
Majambaka jaz band halafu mkubwa wa bendi alikua na pua kubwa Kama engine ya boti
 
"Naitwa captain Gaspar Derrick Mkandala a.k.a Rufufuuuuu"

Jamaa alikuwa mwongo sana Ila alijua kucheza na maneno Hadi muvi unaiona tamu

Lkn kwangu DJ Mark Mzee wa acheche production namkubali zaidi
Dj Mark ndio mkali wao kwangu
 
Pale Kona la kwenda magenge ishilini, upande wa kulia ni kwa limonga, mbele Kuna baa ya mamboto ukiendelea mbele ni kwa serenge dah , we mkali

Hahaha mm nilikuwa nakaa mitaa ya kwa manganya magengeni kulikuwa na baa ya fusi jirani yetu...kwahiyo ile kona ya magenge 20 nilikuwa sifiki napita njia ile ya makaburini katikati zamani sana
 
Wapeeeeenzi watazamaji ndugu zangu wapendwaa

Kwa mara nyingine tena mkandala lufufu library iliyoopo Yombo kwa limboa inawaletea movie kali kabisa ya deadly pray

Imetafsiriwa na captain Gasper Mkandala lufufuuuuuu wako mabameja
Umempatia sanaa
 
Back
Top Bottom