Mfahamu "Mkandala Rufufu" mzee wa kukotola

Mfahamu "Mkandala Rufufu" mzee wa kukotola

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Anaitwa Kapteni Gaspa Derrick Mkandala Lufufu, halafu mbele hapo kuna maneno ya kihaya alipenda kuyaweka Mnaokumbuka vyema Mtatukumbusha.

Baada ya kustaafu kazi ya Jeshi Lufufu aliamua kuanza kutafsiri picha (Movie) za kizungu nk. kwa Kiswahili, jina lake likawa maarufu hapa Nchini Tanzania huku akiwa mtu wa kwanza kabisa kuingiza maneno ya kiswahili kwenye mikanda ya video VHS.

Huyu muasisi wa MaDj wote unaowaona wanatamba hivi sasa alifariki Mwaka 2015 na kuzikwa Moshi Mkoani Kilimanjaro. Baba yake alikuwa Mchaga na mama yake alikuwa Mhaya.

Alikuwa akinogesha movie kwa maneno yake ambayo hatuyajui maana yake mpaka leo ila wapenzi watazamaji walimwelewa.

"Eeeee Tujuane wale wote wa vibanda umiza kipindi kileee tulio kuwa tukirudi tunafikia kwenye kichapo na maji ya baridi juu. watoto wa getini mtupishe kidogo "

Unaikumbuka muvi ipi kutoka kwa huyu mkali....
FB_IMG_1653757618440.jpg
 
Haya ni baadhi ya maneno yake ninayotakumbuka enzi anatafsiri

" akamweka kwenye kanyampasila"

"Na picha letu linaisha hapa, sterling wetu anapanda gari Aina ya chai maharage na kutokomea zake kusikojulikana"

Rufufu alikuwa anatafsiri picha Hadi kuna maneno ukisikia unajua kbs hii ni chai,Ila tulipokuwa na kujua kiingereza Kish atukazirudia zile picha tunakuja kugundua kwamba kweli zile tafsiri za rufufu zilikuwa ni chai😅😅
 
Haya ni baadhi ya maneno yake ninayotakumbuka enzi anatafsiri

" akamweka kwenye kanyampasila"

"Na picha letu linaisha hapa, sterling wetu anapanda gari Aina ya chai maharage na kutekomea zake kusikojulikana"

Rufufu alikuwa anatafsiri picha Hadi kuna maneno ukisikia unajua kbs hii ni chai,Ila tulipokuwa na kujua kiingereza Kish atukazirudia zile picha tunakuja kugundua kwamba kweli zile tafsiri za rufufu zilikuwa ni chai[emoji28][emoji28]
Nomaa
 
"Naitwa captain Gaspar Derrick Mkandala a.k.a Rufufuuuuu"

Jamaa alikuwa mwongo sn Ila alijua kucheza na maneno Hadi muvi unaiona tamu

Lkn kwangu DJ Mark Mzee wa acheche production namkubali zaidi
Kazi za DJ Macky ntazipata mtandaoni sehemu gani ? Nyingi zilizopo wanamuiga tu huku wakiwwka Title Ni yeye
 
Utasikia Lufufuuuu afu anamalizia Nkorombo Wajeba

Mzee wa mfumfulizo kwenye six comando
Shankomela-kupiga sarakasi
Kinumbu au viazi ndio mabomu
Kumiminia mwanyu kupiga risasi
Afu alikua mtu akikabwa unaskia puupuuu eti ushuz 😂
Mguu wa Bata/ wakuku- bastora
Kupata Kanyamazongo- kizunguzungu
 
Anaitwa.Kapteni Gaspa derki mkandala lufufu,, afu mbele Apo kuna maneno ya kihaya alipenda kuyaweka Mnaokumbuka Vyema Mtatukumbusha.

Baada ya kustaafu kazi ya Jeshi Lufufu aliamua kuanza kutafsiri picha (Movie) za kizungu nk. kwa kiswahili, jina lake likawa maarufu hapa nchini Tanzania huku akiwa mtu wa kwanza kabisa kuingiza maneno ya kiswahili kwenye mikanda ya video VHS.

Huyu muasisi wa MaDj wote unaowaona wanatamba hivi sasa alifariki Mwaka 2015 na kuzikwa Moshi Mkoani Kilimanjaro. Baba yake alikuwa mchaga na mama yake alikuwa mhaya.

Alikuwa akinogesha movie kwa maneno yake ambayo hatuyajui maana yake mpaka leo ila wapenzi watazamaji walimwelewa. [emoji2]

"""Eeeee Tujuane wale wote wa vibanda umiza kipindi kileee tulio kuwa tukirudi tunafikia kwenye kichapo na maji ya baridi juu. watoto wa getini mtupishe kidogo [emoji2][emoji2]"""

Unaikumbuka muvi ipi kutoka kwa huyu mkali....View attachment 2242541
Apumzike kwa amani
 
Back
Top Bottom