Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,298
- 7,612
Anaitwa Kapteni Gaspa Derrick Mkandala Lufufu, halafu mbele hapo kuna maneno ya kihaya alipenda kuyaweka Mnaokumbuka vyema Mtatukumbusha.
Baada ya kustaafu kazi ya Jeshi Lufufu aliamua kuanza kutafsiri picha (Movie) za kizungu nk. kwa Kiswahili, jina lake likawa maarufu hapa Nchini Tanzania huku akiwa mtu wa kwanza kabisa kuingiza maneno ya kiswahili kwenye mikanda ya video VHS.
Huyu muasisi wa MaDj wote unaowaona wanatamba hivi sasa alifariki Mwaka 2015 na kuzikwa Moshi Mkoani Kilimanjaro. Baba yake alikuwa Mchaga na mama yake alikuwa Mhaya.
Alikuwa akinogesha movie kwa maneno yake ambayo hatuyajui maana yake mpaka leo ila wapenzi watazamaji walimwelewa.
"Eeeee Tujuane wale wote wa vibanda umiza kipindi kileee tulio kuwa tukirudi tunafikia kwenye kichapo na maji ya baridi juu. watoto wa getini mtupishe kidogo "
Unaikumbuka muvi ipi kutoka kwa huyu mkali....