Mfahamu mtu asiyejuikana (The man with no identity)

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
mvongo.jpg

Huyu jamaa kwenye picha amekuwa akishikiliwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali huko Ontario, Canada.

Huyu jamaa alikamatwa huko Toronto mwaka 2013 kwa tuhuma za kutapeli kiasi cha dola laki nne. Jamaa alidai kwamba jina lake ni Herman Emmanuel Fankem, raia wa Ufaransa anayeishi Montreal. Hata hivyo baada ya vyombo vya usalama vya Canada kuwasiliana na vyombo vya usalama vya Ufaransa, iligundulika kwamba passport aliyokuwa anatumia ni fake na hawakuwa na rekodi yoyote ya kuonyesha kuwa ni raia wao au ametokea Ufaransa.

Uchunguzi zaidi uliendelea katika mataifa 11 lakini hakuna taarifa yoyote ya kueleweka iliyoweza kusaidia kutambua huyu jamaa ni nani hasa. Ila walichogundua ni kwamba kwa kipindi cha miaka kadhaa jamaa alikuwa akisafiri nchi mbalimbali tena kwa majina tofauti tofauti.

Jambo la kushangaza ni kwamba jamaa amegoma kabisa kutoa ushirikiano, na amekuwa mkali sana dhidi ya maafisa wa usalama na gereza kwa kugoma kujibu maswali yao yanayohusiana na wasifu wake au historia yake ya nyuma.

Kwakuwa wameshindwa kujua yeye ni nani na ametokea wapi, mamlaka ya uhamiaji ya Canada imeshindwa kumuondoa nchini humo kwasababu hawajui wamrudishe wapi, hivyo wameamua wamuache gerezani.

Mwaka 2019, aliitwa mahakamani lakini bado alionesha kiburi na kuwatukana hapo mahakamani. Jamaa alirudishwa gerezani. Anazungumza kifaransa kizuri sana.

Mimi ninahisi jamaa ni Mcameroon, maana wanazungumza Kifaransa na wengi hupenda kwenda Ufaransa, na pia kutokana na kukamatwa kwasababu ya kutapeli dola laki nne kwa mambo ya Faymanian ndiyo michezo yao. Huenda ametokea Bafoussam huko.
 
Nimekuja mbio nikifikiri ni wale watu wasiojulikana wa Tanzania kutoka kitengo pendwa kinachofanya uharamia, utekaji, uuaji,utesaji na unyanyasaji wa Watanzania wenzao!

62327194.jpg
 
Watuwasiojulikana kwa wenzentu wanapiga deal Kama hizi lakini kwetu ni kutesana
 
Wameonesha uzembe sana... Kwetu unaongea ukweli mpaka unaisha, Then unaanza kuongea chochote kitakachosaidia upelelezi usitishwe!
Kweli kabisa,kule wanambembeleza,inatakiwa wafanye mbinu zozote mpaka jamaa aseme yeye ni wawapi.
 
View attachment 1649792

Huyu jamaa kwenye picha amekuwa akishikiliwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali huko Ontario, Canada.

Huyu jamaa alikamatwa huko Toronto mwaka 2013 kwa tuhuma za kutapeli kiasi cha dola laki nne. Jamaa alidai kwamba jina lake ni Herman Emmanuel Fankem, raia wa Ufaransa anayeishi Montreal. Hata hivyo baada ya vyombo vya usalama vya Canada kuwasiliana na vyombo vya usalama vya Ufaransa, iligundulika kwamba passport aliyokuwa anatumia ni fake na hawakuwa na rekodi yoyote ya kuonyesha kuwa ni raia wao au ametokea Ufaransa.

Uchunguzi zaidi uliendelea katika mataifa 11 lakini hakuna taarifa yoyote ya kueleweka iliyoweza kusaidia kutambua huyu jamaa ni nani hasa. Ila walichogundua ni kwamba kwa kipindi cha miaka kadhaa jamaa alikuwa akisafiri nchi mbalimbali tena kwa majina tofauti tofauti.

Jambo la kushangaza ni kwamba jamaa amegoma kabisa kutoa ushirikiano, na amekuwa mkali sana dhidi ya maafisa wa usalama na gereza kwa kugoma kujibu maswali yao yanayohusiana na wasifu wake au historia yake ya nyuma.

Kwakuwa wameshindwa kujua yeye ni nani na ametokea wapi, mamlaka ya uhamiaji ya Canada imeshindwa kumuondoa nchini humo kwasababu hawajui wamrudishe wapi, hivyo wameamua wamuache gerezani.

Mwaka 2019, aliitwa mahakamani lakini bado alionesha kiburi na kuwatukana hapo mahakamani. Jamaa alirudishwa gerezani. Anazungumza kifaransa kizuri sana.

Mimi ninahisi jamaa ni Mcameroon, maana wanazungumza Kifaransa na wengi hupenda kwenda Ufaransa, na pia kutokana na kukamatwa kwasababu ya kutapeli dola laki nne kwa mambo ya Faymanian ndiyo michezo yao. Huenda ametokea Bafoussam huko.
Hii sura naifahamu kabisa, hao wakanada waniite niende nikawaambie jamaa ni naniili wampeleke anapostahili
 
Mi nilijua waliomteka ROMA na kumtwanga risasi LISU
 
Back
Top Bottom