Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,154
- 31,246
Huyu jamaa kwenye picha amekuwa akishikiliwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali huko Ontario, Canada.
Huyu jamaa alikamatwa huko Toronto mwaka 2013 kwa tuhuma za kutapeli kiasi cha dola laki nne. Jamaa alidai kwamba jina lake ni Herman Emmanuel Fankem, raia wa Ufaransa anayeishi Montreal. Hata hivyo baada ya vyombo vya usalama vya Canada kuwasiliana na vyombo vya usalama vya Ufaransa, iligundulika kwamba passport aliyokuwa anatumia ni fake na hawakuwa na rekodi yoyote ya kuonyesha kuwa ni raia wao au ametokea Ufaransa.
Uchunguzi zaidi uliendelea katika mataifa 11 lakini hakuna taarifa yoyote ya kueleweka iliyoweza kusaidia kutambua huyu jamaa ni nani hasa. Ila walichogundua ni kwamba kwa kipindi cha miaka kadhaa jamaa alikuwa akisafiri nchi mbalimbali tena kwa majina tofauti tofauti.
Jambo la kushangaza ni kwamba jamaa amegoma kabisa kutoa ushirikiano, na amekuwa mkali sana dhidi ya maafisa wa usalama na gereza kwa kugoma kujibu maswali yao yanayohusiana na wasifu wake au historia yake ya nyuma.
Kwakuwa wameshindwa kujua yeye ni nani na ametokea wapi, mamlaka ya uhamiaji ya Canada imeshindwa kumuondoa nchini humo kwasababu hawajui wamrudishe wapi, hivyo wameamua wamuache gerezani.
Mwaka 2019, aliitwa mahakamani lakini bado alionesha kiburi na kuwatukana hapo mahakamani. Jamaa alirudishwa gerezani. Anazungumza kifaransa kizuri sana.
Mimi ninahisi jamaa ni Mcameroon, maana wanazungumza Kifaransa na wengi hupenda kwenda Ufaransa, na pia kutokana na kukamatwa kwasababu ya kutapeli dola laki nne kwa mambo ya Faymanian ndiyo michezo yao. Huenda ametokea Bafoussam huko.