Mfahamu mtunzi mahiri was nyimbo za kikatoliki marehemu John Stephano Mgandu

Mfahamu mtunzi mahiri was nyimbo za kikatoliki marehemu John Stephano Mgandu

Kuna jamaa tulisoma naye alikuwa anajua Nota na kucheza piano balaaaaaa.Jamaa wakasema huyu akienda Kwa Mgandu ataambiwa aanze upya kujifunza
 
Huyo mwenye nyekundu mwondoe, katika list aliyoitaja na watunzi wanaotunga nyimbo zenye adabu na zinazofuata sheria na vipengele vyote vya muziki. Huyo na mpiga kinanda aitwaye mkude, waliibukia huko arusha kwa kuanza kutunga manyimbo na uimbaji wa staccato (matamshi ya kukatakata maneno) , nyimbo zisizo kamilika unakuta ni chord 3 au 2 zinajirudia , mapambio. Hawa waliungana na mpiga kinada aitwaye mkude ambaye ndiye mwanzilishi wa masebene katika kanisa, na baadaye mtunzi maarufu wa kizazi kipya aitwaye mukasa akajiunga na ndio ikawa turning point ya kuharibika na kupotea muziki wa akina mgandu na sasa huwaambii vijana kuhusu masebene, kila mpiga kinanda hana time na kujifunza bugert bali ni hizo chord 3 tuu, ........basi mengine nitaeleza siku nyingine
Nadhani muziki wa Mgandu ndio Bora kabisa na ndio utambulisho wa Nyimbo za Liturjia za Katoliki
 
Hii ndo thread bora kabisa kwangu kwa mwaka huu 2018.
Asante mtoa post kwa kutumegea mambo ya muhimu kuhusu historia ya nguli wa muziki wa kikatoliki Tanzania.
Binafsi n mpenzi mkubwa wa nyimbo za kikatoliki za zamani,ila naona kuna changamoto kidogo muziki wetu haupewi promo ya kutosha ktk vituo vya radio na Tv kubwa,natamani wakatoliki tungekuwa na vyombo vyetu vikubwa vinavosikika nchi nzima ili uinjiilishaji kwa njia ya nyimbo na muziki mtakatifu usonge mbele.
 
John Mgandu alikuwa wa daraja la kipekee kwenye muziki wa kikatoliki. Wengine kwenye kundi hilo nawaweka akina Fr Gregory Kayeta, Fr Malema Lui Mwanampepo, Guido Matui, IP Nganga, Joseph Makoye, Felician Albert Nyundo, Melkiory Syote.
Kuna kundi lililoibuka baada yao likijifunza kwao, linajumuisha akina Thobias Daudi Nsato. Baadae wakaja akina Charles Saasita katika kiwango hicho. Bahati mbaya wengi niliowataja ni marehemu.

Utunzi wa segere, midundiko, na mengine ya hovyohovyo kanisani kwa sasa ni janga la kitaifa linalohitajika kukemewa kwa nguvu.
 
MGANDU%2Bcopy.jpeg

MTUNZI MAHIRI WA NYIMBO ZA KIKATOLIKI MAREHEMU JOHN STEPHANO MGANDUkwa wale wapenzi/walimu au wanafunzi wa Muziki wa kikatoliki baasi jina la JOHN MGANDU sio geni, kwa ufupi.. Alikua Mmoja kati ya watunzi ambao walijitahidi kutumia karama zao katika kuwasaidia waamini kusali vizuri kwa njia ya uimbaji ni Mwalimu John Stephano Mgandu.Yeye alizaliwa Oktoba 8, 1940 kijijini Busondo, katika Parokia ya Ndala-Nzega, mkoani Tabora. Alipata elimu katika Shule ya Msingi Puge (1951-1953), kisha Seminari ya Lububu (1954 – 1955), baadaye Seminari ya Itaga (1956 – 1959) na Seminariya Kipalapala1964. Mwaka 1960 hadi 1970 alikuwa katika Chuo cha Ualimu cha Chang’ombe. Elimu ya muziki aliipata katika Chuo Kikuu cha Toronto nchini Canada ambako alisomea Shahada ya Muziki (Bsc – Music) 1972 – 1976, na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es salaam akisomea Shahada ya Uzamili (MA – Music) 1987. Amewahi kufanya kazi katika maeneo mbalimbali pamoja na Benki ya NBC tawi la Masdo (1968), Shule ya Sekondari ya Kibasila (1970), Shule ya Sekondari ya Mirambo (1971), Shule ya Sekondari ya wavulana Tabora (1976 – 1978), Taasisi ya Elimu (1978 – 1980) na kisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika Idara ya Sanaa na maonyesho (Julai 1980 – Julai 2008) Alifunga ndoa na Elizabeth Kulwa Binti Constatino Ngelegi, na kupata watoto wawili, wa kiume na wa kike. Licha ya kuwa mtunzi, Mwalimu Mgandu alikuwa mpiga kinanda, filimbi na ala nyingine nyingi. Pia alikuwa mwalimu na muongozaji wa muziki na kwaya mbalimbali. Ikumbukwe kuwa mwaka 2002 Mwalimu Mgandu alishinda tuzo ya kuwa Mpiga Kinanda Bora Tanzania (Tanzania Kilimanjaro Music Awards). AlifarikiJulai 10 mwaka 2008. *Baadhi ya Nyimbo alizotunga*Bahati Nzuri Kwetu - John Mgandu Bwana aliniambia - John Mgandu Bwana Amefufuka - John Mgandu Bwana amejaa huruma - John Mgandu Bwana Asema Tazama - John Mgandu Bwana mfalme - John Mgandu Bwana Ndiye Mchungaji Wangu - John Mgandu Bwana ni Nani Atakayekaa - John Mgandu Bwana Ni Nani Atakayekaa (corrected) - JohnMgandu Bwana Ni Nuru Yangu - John MganduD ----- Dondokeni enyi mbingu - John MganduE ----- Ee Bwana Fadhili Zako - John Mgandu Ee Bwana Kumbuka Rehema Zako - John Mgandu Ee Bwana nakuinulia nafsi yangu - John Mgandu Ee Bwana Nimekuita - John Mgandu Ee Bwana Nimekuita - John Mgandu Ee Bwana Twakuomba - John Mgandu Ee Bwana Ulimwengu Wote - John Mgandu Ee Bwana Ulimwengu Wote - John Mgandu Ee Bwana Ulitafakari Agano - John Mgandu Ee Bwana Unihukumu - John Mgandu Ee Bwana Usikie (Mwanzo J2 11B) - John Mgandu Ee Bwana Utege Sikio - John Mgandu EeBwana, Wewe Ndiwe Mwenye Haki - John Mgandu Ee Mungunchi yote itakusujudia - John Mgandu Ee Mungu Nimekuita Kwa Maana Utaitika - John Mgandu Ee Mungu Wangu - John Mgandu Ee Mungu Wangu Mfalme - John Mgandu Ee MunguWangu Nitakutafuta - John Mgandu Ekaristi Takatifu - John Mgandu Enendeni Duniani Kote - John MganduF ----- Fadhili za Bwana - John Mgandu Furahi Yerusalemu - John MganduH ----- Hawa Ndio Wale - John Mgandu Heri Taifa - John Mgandu Heri Taifa - John Mgandu Heri Walio Maskini Wa Roho - John Mgandu Hosana Mwana Wa Daudi - John MganduI ----- Ingekuwa Heri Leo - John MganduK ----- Kaa Nasi Bwana - John Mgandu Kabila Langu - John Mgandu Kanisa la Kitume - John Mgandu Kikondoo Cha Mungu - John Mgandu Kristu Alijinyenyekeza- John Mgandu Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa - John Mgandu Kwako Bwana - John MganduL ----- Leo Amezaliwa - John Mgandu Leo Tumefunga Ndoa - John MganduM ----- Malaika wa Bwana - John Mgandu Maombi Yangu Yafike - John Mgandu Maombi Yangu Yafike-2 - John Mgandu Mawazo ninayowawazia ninyi - John Mgandu Mawazo Ninayowawazia Ninyi - John Mgandu Mbele ya Miungu - John Mgandu Mimi Ndimi Mchungaji Mwema - John Mgandu Misa No.2 Utusamehe Makosa Yetu - John Mgandu Mpigie Mungu Kelele - John Mgandu Mshukuruni Bwana - John Mgandu Msifanye Mioyo Yenu Iwe Migumu - John Mgandu Msifanye Mioyo Yenu Migumu - John Mgandu Msisumbuke - John Mgandu Msisumbukie Maisha Yenu - John Mgandu Msisumbukie Maisha Yenu - John Mgandu Mtoto Yesu Yuko Pangoni - John Mgandu Mtu Akinitumikia - John Mgandu Mtu Hataishi Kwa Mkate - John Mgandu Mtumikieni Bwana - John Mgandu Mungu Awabarikie - John Mgandu Mungu Awabarikie - John Mgandu Mungu UnihifadhiMimi - John Mgandu Mungu Wangu Mbona Umeniacha - John Mgandu Mwenye Heri Bakhita - John Mgandu Mwimbieni Bwana - John Mgandu Mwimbieni Bwana Wimbo Mpya - John MganduN ----- Nakwenda kwa Baba - John Mgandu Nalifurahi Waliponiambia - John Mgandu
 
Mwenye wimbo unaoitwa "hapa we msafiri simama " audio yake tafadhar naomba aniwekee hapa.. Ntashukuru sana.. Muwe na jpili njema
 
Back
Top Bottom