Mfahamu mtunzi mahiri was nyimbo za kikatoliki marehemu John Stephano Mgandu

Mfahamu mtunzi mahiri was nyimbo za kikatoliki marehemu John Stephano Mgandu

Kwa kweli sina shaka na utunzi wa nyimbo mbalimbali za John Mgandu na mimi ni mmojawapo wa wapenzi wa tunzi zake. Pamoja na weatunzi wengine uliowainisha mwangalie na mtunzi mwingine mahiri kutoka Jimbo la mbeya Fr. Gregory F. Kayeta (Marehemu) na yeye kazi zake za utunzi zinaishi kwa maana na yeye alifata sana Liturujia. Asante kwa uandishi mzuri juu ya John Mgandu maana mimi wasifu wake sikuwa naufahamu vyema zaidi ya kusikia kuwa alikuwa professor pale Chuo Kikuu cha DSM akifundisha muziki.
 
John Mgandu alikuwa wa daraja la kipekee kwenye muziki wa kikatoliki. Wengine kwenye kundi hilo nawaweka akina Fr Gregory Kayeta, Fr Malema Lui Mwanampepo, Guido Matui, IP Nganga, Joseph Makoye, Felician Albert Nyundo, Melkiory Syote.
Kuna kundi lililoibuka baada yao likijifunza kwao, linajumuisha akina Thobias Daudi Nsato. Baadae wakaja akina Charles Saasita katika kiwango hicho. Bahati mbaya wengi niliowataja ni marehemu.

Utunzi wa segere, midundiko, na mengine ya hovyohovyo kanisani kwa sasa ni janga la kitaifa linalohitajika kukemewa kwa nguvu.
Sahihi kabisa!
 
Daah Hakika alikua ni mtaalamu sana, playlist yangu ina nyimbo zake kadhaa ambazo zote zinakufanya utamani na uzidi kumpenda Mungu.🙏
 
Back
Top Bottom