Mfahamu T.O Kihombo 2006 aliyepata Degree yake ya Kwanza baada ya Miaka 11

Mtu anayesema Pure Math ni rahisi ama ni muongo ama hajaielewa, pengine kwa kuisoma kwa level ndogo sana.

Hizo Physics na Chemistry kimsingi ni derivatives za Pure Maths.

Unaweza kusoma Pure Maths bila Chemistry wala Physics. Lakini ukisoma Chemistry na Physics utakutana na concepts za maths. Huwezi kusoma bila maths.

Ukisoma historia za ma genius wa kweli kama kina Srinivasan Ramanujan (kama hujamjua tafuta movie au kitabu "The Man Who Knew Infinity", the book is better than the movie, the movie is good too) utaona mtu ni genius wa kweli mpaka inabidi tujiulize alikuwa na ubongo wa aina gani, lakini yuko very humble.

Srinivasa Ramanujan - Wikipedia
Fact hesabu ndo baba lao
 
Ila system ya kudisco ipo Tanzania peke yake yani mtu afaulu miaka 3 afeli semester moja eti ufute matokeo yote aanze upya bora sikusoma any degree hapo Tanzania ni upumbavu wa Hali ya mwisho
Upo sahihi kabsa mkuu, system ya chuo ukizingua kabisa kabsa unapewa Discontinued.
 
Sasa unataka apite tu kisa alipata 1.3?
Hivi wewe unaakili kichwani yani mtu afaulu miaka yote 3 akifeli semester moja ya mwaka WA 4 ndo anafutiwa matokeo yote Hivi Kuna ujinga kama huo Dunia ipi kwanini wasimwambie arudie mwaka au afanye transfer. Elimu ya Tanzania ni upumbavu mtu. Hivi kufeli semester moja kunafutaje matokeo ya semester za zamani ulizofaulu
 
Imepita miaka takribani 12 sasa, tangia Tanzania ilipapata kumshuhudia mwanafunzi alishindikana katika maswala ya Elimu hapa namzungumzia,Tanzania One (2006) Elias Kihombo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2006 akitokea shule ya sekondari Tosamaganga wengi wanapenda kuiita Tosa Boy's

Mwaka 2006, Necta ilimtangaza mwanafunzi Elias Kihombo kutoka Tosamaganga Secondary School kuwa ndo kipanga wa mwaka huo akiwapita wanafunzi wenye akili zaidi waliovuma toka shule kongwe na special schools kama kibaha, ilboru, mzumbe, kilakala, Tabora boys etc ukweli ni kwamba Elias Kihombo hakuwa maarufu kwa kipindi hiko na wengi walisikia tu story zake haswa kwa wanafunzi wa Mzumbe Boys ambao Mara nyingi walipata kumuona katika mazingira yao.

Kumbuka kwamba Elias Kihombo hakupewa Priority kubwa sana ya kuwa T.O wa Advance Level kutokana pia na matokeo yake ya Kidato cha Nne (4) kuonekana kuwa ya kawaida sana, Kihombo alifanikiwa kupata Division One (1.14) akiwa na Physics-A Chemisrty-A Biology na Mathematics-B, Ndipo mwaka huo 2003 alipata kuchaguliwa Tanga Technical school iliyopo mkoa wa Tanga (tetesi), lakini baadae aliamua kurudi tena katika shule yake ya zamani yaani Tosamaganga secondary kuendelea na masomo yake ya Advance level. Alimaliza hapo hapo akifanikiwa kuwa mwanafunzi wa kwanza toka Tosamaganga kwa Advance Level kuwa mwanafunzi bora kitaifa, Alifanikiwa kupata maksi za juu sana na kupata Division One (1.3)
Physics-A
Chemistry-A
Advanced Mathematics-A

October 2006 Alichaguliwa kujiunga na University of Dar Es Salaam (UDSM) akiwa kama T.O kusoma Bachelor of Science In Telecommunication Engineering (4years) na tetesi zinasema alifanikiwa kupata ufadhili wa masomo yake chini ya kampuni ya Airtel.
Siku zilienda na alikuwa karibu kumaliza Elimu yake ya chuo kikuu, huku akipata madili mengi ya kufundisha Tuition maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam na shule nyingi za sekondari ndani ya Tanzania hasa shule za Advance.

Lakini baada ya Miaka 4 kupita ikiwa miezi michache tu imebaki ya kumaliza chuo Tanzania One Kihombo alidisco chuo na hivyo kumfanya asifanikiwe kupata degree yake ya kwanza mwaka huo 2010, lakini wengi wanasema hakupaswa kudisco chuo lakini ndivyo ambavyo Hatima yake ilipoishia hapo. (tetesi [emoji6] [emoji6]).

Moja kati ya maneno ambayo wengi wanamnukuu aliyopata kuyasema ndani ya Miaka hiyo, alisema "Duniani walionipita kwa akili ni watu wawili tuu wa kwanza Mola, wa pili ni Mzungu" hapa ndipo hatima yake inavyosemekana ikafungwa na wakuu wake lakini wengine wanasema vingine.

Elias hakutaka kwenda chuo chochote kile na ndani ya Miaka hiyo mitatu baada ya kudisco chuo, yaani 2011,2012 na 2013 alikuwa anazunguka shule mbalimbali za sekondari Tanzania kupiga mapindi ya Physics na Chemistry na kwelii huyu jamaa alikuwa ni Invisible katika masomo hayo mawili, Japo Pure Mathematics alikuwa hafundishi kabisa kwasababu alikuwa anasema "Siwezi kufundisha Somo rahisi duniani kama Pure Mathematics, Mimi nafundisha Physics na Chemistry tu"

Ndipo baada ya Miaka mitatu kupita (3) T.O aliyetukuka zaidi katika vinywa vingi vya wanafunzi wa Tanzania, kutokana na ufundishaji wake na kuwaita wanafunzi wake Nyumbu na kuwa na Jeuri zaidi ya Akili zaidi ya watu wengine, alifanikiwa kurudi tena ndani ya University of Dar Es Salaam safari hii akiwa ameamua na amezamilia kuchagua kozi nyingine Mpya kabisa iliyoanzishwa mwaka huo 2013 hapohapo Udsm iliyoitwa (Bachelor of Science In Petroleum Engineering). Hii kozi ilikuwa inachukua wanafunzi 20 pekee Tanzania nzima tena wale waliosoma PCM tu (Physics, Chemistry na Advanced Mathematics) na waliopata Marks za juu kabisaa.

Baada ya Miaka 4 kupita, ndipo July 2017, T.O Elias Kihombo alifanikiwa kumaliza Degree yake ya kwanza (Bachelor of Science In Petroleum Engineering) na mnamo November 2017 Elias Kihombo alifanikiwa kutunukiwa Degree yake ya kwanza akiwa ndani ya University of Dar Es salaam baada ya Miaka 11 kupita.

Hapa imepita Miaka mingi tangia, 2006 Engineer Elias Kihombo alivyotangazwa kuwa Tanzania One lakini ilimchukua Miaka mingine 11 mpaka kutunukiwa Degree yake ya kwanza. Huyu ndiye The Best Of The Best, Eng Elias Kihombo Mwanafunzi aliyepata kutokea Tanzania na kuwaonesha wengine uwezo wakee katika nyanja nzima ya Elimu.

Wapo wengi wanaojiuliza Eng Elias Kihombo yupo wapi kwasasa, Lakini mpaka sasa Kihombo yupo chini ya Himaya ya Mkoa wa Geita Nyumbani kwa Mheshimiwa Rais John Joseph Pombe Magufuri, huku akiendeleza harakati zake na akiwa na vitabu vyake vingi alivyoviandika kuwasaidia vijana wa Tanzania ikiwa pamoja na Physics Books na Chemistry Books.

*We Always Live To Fight Another Day*

Written by Eng Evans Richard.View attachment 818214View attachment 818215View attachment 818222
Point of correction; he didnt graduate class of PE 2017. Fatilia vizuri.
 
huyo kijana kihombo haja graduate degree ya petroleum eng hakumaliza pia ilikua adisco tena but ana carry za kutosha. Jf hatupendi udaku period
 
Huyu jamaa akikufundisha ukaacha kuelewa inabidi umuone daktari. Binafsi namuelewa sana.

Aliwahi kuja kufundisha shuleni kwetu A level, siku moja akaomba tukusanye maswali yoote magumu (hata kutoka shule za jirani) ya physics kisha tumpatie ayatatue aka ahidi ikitokea akakosea swali hata moja basi atatupatia laki moja kwa kila swali atakalokosa, basi siku ikawadia (ijumaa fulani saa 2 kamili asubuhi) maswali kuntu yote yakafikishwa mbele yake.
Akaanza ku solve maswali yale ubaoni mpaka saa 5 inafika hakuwa kakosea swali hata moja, akaomba break kidogo ya saa moja kwaajili ya kupata chai na kupumzika kidogo, akarejea ubaoni saa 6 hadi saa 8 napo hakukuwa na swali lililomtatiza, tukapata break ya kwenda kula cha mchana, akarejea ulingoni saa 10 hadi saa 12 hakuna swali lilomchachafya pia na maswali yote yaliisha, kutokea hapo kila mwanafunzi aliamini uwezo wa huyu kijana.
 
Huyu ni kishoka! Kipofu anayejaribu kumwongoza kipofu mwenzake! Kupata division 1 ya pointi 3 hakumfanyi mtu kuwa mwalimu mzuri.
Binafsi nimewahi kufundishwa nae, jamaa anauelewa mzuri sana wa masomo tajwa, anafafanua kwa njia rahisi kabisa na ya kueleweka bila shaka hizo ni miongoni mwa sifa za mwalimu mzuri
 
Hivi ma TO huwa wanzdisco....mkuu umefeli kwa stori yako mbwembwe nyingi lakini mambo unayomsifia jamaa ni ya kawaida sana.
 
Back
Top Bottom