elmagnifico
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 8,261
- 9,733
Kama ambavyo ukitaja majina ya wanasayansi wakubwa huwezi kukosa kumtaja Newton, hivyo hivyo huwezi kutaja waandishi wa vitabu vya lugha ya Kingereza bila kumtaja William Shakespear.
Huyu ni mwandishi wa michezo ya kuigiza ambaye anashika namba moja katika waandishi wa Kingereza kutokana na uwezo mkubwa aliyokuwa nao katika kazi zake.
Uwezo huo umefanya kuwepo kwa mabishani baina ya wanazuoni baadhi wakipinga ya kwamba Shakespear hakuwa na uwezo wala elimu ya kuandika hizo kazi zinazodaiwa kuwa aliandika yeye.
Ukisoma vitabu vya shakespear kama Julius ceaser, Romeo and Julieth, The merchant of Venice, Hamlet, Macbeth, Othello, The tempest, King Lear, Twelfth Night na kazi zake nyingine nyingi, utagundua huyu mwandishi alikuwa amebobea katika sheria, biasha, saikolojia, utwala, elimu ya tiba na mfumo wa mwili, elimu ya jeshi, lugha ya Kingereza, uchumi, siasa, ametembea sana sehemu mbalimbali duniani na nyanja nyingine.
Jambo hili huleta utata kwakuwa Shakespear hakuwa amesoma sana alikuwa na elimu ya kawaida na kazi yake ikiwa ufundi seremala.
Uwezo huo ndiyo unaowafanya wanazuoni wengi kuhisi ya kwamba siyo yeye aliyeandika kazi hizo bali kuna watu kadhaa ambao walikuwa katika utawala ndiyo waliandika hizo kazi kwa kutumia jina la Shakespear ili wasijulikane.
Katika kazi zake Shakespear alitumia maneno ya Kingereza 31,534 ambapo 14,376 aliyatumia mara moja tu na maneno 846 aliyatumia kwa kuyarudia zaidi ya mara 100.
Inakisiwa Shakespear alikuwa anajua maneno ya Kingereza yapatayo 66,534 wakati mtumiaji wa kawaida wa kingereza anajua kati ya maneno 10,000-20,000.
Na zaidi ni kwamba alitengeneza maneno mapya 1,653 ambayo yanatumika kwenye lugha ya Kingereza.
VITU AMBAVYO WANAZUONI WANAKUBARIANA KUHUSU SHAKESPEAR
William Shakespear alizaliwa Stratfor-upon-Avon, akahamia London alipoanza kujihusisha na kazi ya uigizaji kabla ya kurudi Stratford na kuishi hapo mpaka mwaka 1616 umauti ulipomchukua.
Lakini kupata kumbukumbuku za maisha yake imekuwa vigumu tu ni habari chache zenye ushahidi kama ndoa yake na Anne Hathaway, na vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wao watatu.
Kutokana na kukosekana kwa nakala zozote za maana inayomhusu kunaleta maswali mengi na watu kujiuliza inawezekanaje mtu aliyeonekana kuwa na uelewa mkubwa wa mambo mengi na uwezo mkubwa ambaye kazi alizoandika zinaonekana na ziko wazi ila yeye hakuna nakala zozote za maana zinazomhusu?
Mwandishi T.J Looney yeye anadai ya kwamba anahisi aliyeandika kazi za Shakespear ni Edward de Vere wa Oxford.
Vere alikuwa ana elimu kubwa na alikuwa kasomea sheria, pia alikuwa amesafiri sana na sehemu nyingi alizoaafiri ndizo zinazotajwa kwenye kazi za Shakespear.
Inadaiwa kwamba aliamua kuficha uhalisia wake kwakuwa kazi zake nyingi zilihusisha siasa, jambo ambalo alihisi linaweza kumletea matatizo iwapo atajiweka wazi kama mwandishi.
Lakini hakuba ushahidi wowote ambao unaweza kumuunga Vere na kazi za Shakespear hivyo basi bado Shakespears mwenyewe anabakinkuwa ndiye mwandishi.
Kwa wale ambao wamebahatika kusoma vitabu vya huyu bwana watakubariana na mimi kwamba, huyu jamaa alikuwa ni mwandishi wa kipekee aliyewahi kutokea.