Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Labda ungeandika kifungu kabisa kurahisisha halafu nikujibu

Kumbukumbu la torati 3:11
11 (Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani

Biblia hapa inasema ogu ni mrefai aliyesalia sasa naomba unisaidie kama wanefili (warefai) wote walifariki kwenye gharika je mfalme ogu alitokea wapi???

Tuanzia hapo kwanza
 
Naona umeshinda!.
Sema wengine wamebaki Na maswali yale yale ya mwanzo!...
 
Kiongozi usijaribu kubishana Na watu!.
Mbona hapo juu nishatoa hitimisho!.
Mpango wa Mungu Huwa Na kusudi maalumu!.
Nimesema hapo juu kuwa Mungu alimwacha OG Na waamor for reasons!...
Nakubaliana na hitimisho lako 100% ila kuna watu wanakataa kabisa kuwa Mungu hawezi muacha mnefili nyuma kama ilikuwa nia yake kuwaangamiza kwenye gharika ndio maana nikajenga hoja hapo kuwa mbona Mungu aliapa kuwafuta wacanaan wote ila mwisho wa siku aliwaacha wengine hakuwaua na aliwakataza hata waisrael wasiawaue??

Kama aliweza kuwaacha hao wacanaan ilihali alishaapa kuwamaliza kivp watu wakatae kuwa Mungu asingeweza kumuacha mfalme ogu??
 
Hahahahaa!..
Upo vizuri naona!.
Mjadala umekwisha anzisha mwingine!.
Hawa waliobaki wataleta ubishi wa kitoto!..
Mkuu leta maada ingine
 
Hahahahaa!..
Upo vizuri naona!.
Mjadala umekwisha anzisha mwingine!.
Hawa waliobaki wataleta ubishi wa kitoto!..
Mkuu leta maada ingine
Nmeshaipost mkuu ila kama kawa JF intelligence wanashikilia nyuzi kwa siku kadhaa ndio wanaiachia
 
Sahihi jana nimepost Uzi but naona Bado upo pending!..
Itabidi ni freeze Uzi wangu ili wako utembee
Hata wangu utakuta unaachiwa jumatatu huko dah yaani hawa mods mkuu wanaudhi sana na hizi kelele hata hawajali kabisa sijui kwanini
 
mkuu ...
aliyesalia katika mabaki ya warefai wapi?
1:Kumbukumbu 2:20 (Nchi hiyo nayo yadhaniwa kuwa ni nchi ya Warefai, hapo kale Warefai walikaa humo; lakini Waamoni huwaita Wazamzumi;
21 nao ni watu wengi, wakubwa, warefu, kama Waanaki; lakini Bwana aliwaangamiza mbele yao; wakawafuata wakakaa badala yao;

au
2:Waliobaki baada ya waamori kuchukua eneo hilo kutoka kwa waamoni.

au
kubaki katika gharika?
 
Uzao wa wanefili haukua wa wanadamu japokuwa anaki nao haukua hivyo Tangu mwanzo shetani alijiingiza ndani ya kiumbe ili afanikishe kile alicholenga ndani ya jamii hiyo
Mfano biblia inasema habari ya majitu kabla wakati wa nuhu na baada ya nuhu
Katika Mwanzo 6:1-4 unaona watu wanatajwa kama wana wa Mungu hao wana Mungu walizaa na binti za wanadamu yaani watu wa Mungu ukielewa hapa Utaona uasi na dhambi
zikawa nyingi Mungu aliteketeza wore hakuna kilichosalia isipokuwa baada ya gharika kulitokea nimrodi huyu alikuwa ni mtu hodari ambaye inaonyesha alikuwa na nguvu uyu naye ni mzao wa kushi lakini alizaa hao waamori wafilisti na wengine wengi tu ambao ni watu wakubwa mwanzo 10:9,,, utagundua hayo majitu yalitokea uzao upi linganisha hayo makabila na hayo yaliyotajwa hapo kwa Ogu

Ukisoma yuda 1:4. Utaona watu waliojiingiza kwa siri waibadilio neema kuwa ufisadi waozungumziwa hapa na mwandishi sio tu Leo katika kanisa bali hao majitu
Kwa kukamilisha uzao wao ogu haukuwa wa kawaida maana hawakuwa watu wa asili bali walitokana na malaika waasi na hukumu yao si sawa nawanadamu ukiniambia mabaki yaliosalia
Ni watu nane na katika hao kuna uwezekano wa kuwapata wanefili kirahisi mno
Soma
Hayo makabila kwanza uniambie yanavyo endana na ogu
 
Kabla ya gharika mkuu..... All in all hata kama ingekuwa baada ya gharika bado swali lingekuja whether og alikuwepo au hakuwepo kabla ya gharika je WANEFILI walirudije baada ya gharika??

Nafkiri ukinielewesha jinsi warefai walirudi baada ya gharika basi tunaweza fikia ukomo wa mjadala huu yaani tukiachana na OG ambaye biblia haisemi kama alivuka gharika JE WANEFILI walirudije baada ya gharika hadi almost immediately baada ya gharika walishakuwa na utawala wao soma mwanzo 14

Ukinielewesha hapa utakuwa umenisaidia kupata ukweli wa ogu kama naye alikuwepo hata kabla ya gharika au ni upotoshaji tu wa vitabu flani

Ahsante
 
Mkuu hii ni biblia mbona ndio nmeongelea kwenye hii post na hata mfalme Ogu pia biblia inamtaja so hatupo mbali sana na vitabu vya dini

Labda udadavue kipi kimekuchanganya ili wajuvi watiririke
Mkuu nimeusoma uzi wote taratiibu nimegundua biblia naisomaga juju muda mwingi tu,nikuulize we kwa uelewa wako mbn mi naona ule mstari katk kitabu cha mwanzo unao sema wana wa mungu walijitwalia mabinti wa binadamu wakazaa nao watoto ambao ndo walikuwa hodari kipindi hicho,sasa tatizo language hapa nilidhani mstari unaofuata unaosema nao wanefili walikuwako siku zile ninavyoelewaga Mimi ni kuwa wanefili walikuwako kabla ya wana wa mungu kujitwalia binti za wanadamu,kingine ni kuwa Nina bible Fulani hivi katika mstari wa wana wa mungu wametajwa kama "wana wa mungu wa kweli" sasa hapa neno wakweli linamuhusu Mungu au "wana" yaani Mungu wa kweli au hao wana wa Mungu ni wana wa kweli wa mungu? Pole nimeandika kwa uelewa wangu tu sijanakili kila neno katk mistari ya biblia.
 
Kiongozi usijaribu kubishana Na watu!.
Mbona hapo juu nishatoa hitimisho!.
Mpango wa Mungu Huwa Na kusudi maalumu!.
Nimesema hapo juu kuwa Mungu alimwacha OG Na waamor for reasons!...
Waamori ni uzao wa nimrodi unafikiri nimrodi alikuwa nani ni yale yale majitu soma mwanzo hakunahaja ya kukimbia mbele mwazo 10:8-20
Je nimrodi si alizaliwa na kushi mwana wa hamu mzao wa nuhu je nuhu hakuwa mabaki ya gharika au nini tena
 
Naongeza hivyo wanefili/warefai hawakujishikiza bali walizaliwa tena kwa nimrodi maana hawakuwa watu wa asili bali walitokana na kuingiliana kwa malaika wa shetani(wana WA Mungu) kwa maana hiyo Hoja yako pamoja na vifungu vyote hukuchimba hayo makabila yanayoelezwa hapo jamaa walikuwepo kutoka kwenye uzao wa nimrodi hakuna aliyejishikiza popote
Yaaani
Mwanzo waliosalia ni 8 tu na katika hao warefai walizaliwa
 
Waamori ni uzao wa nimrodi unafikiri nimrodi alikuwa nani ni yale yale majitu soma mwanzo hakunahaja ya kukimbia mbele mwazo 10:8-20
Je nimrodi si alizaliwa na kushi mwana wa hamu mzao wa nuhu je nuhu hakuwa mabaki ya gharika au nini tena
Mkuu ambacho nafkiri unaruka ni kwamba sisi hatubishi kuwa Og hakuwepo kabla ya gharika ila tusaidie wwe je wanefili walirudije baada ya gharika??? Maana Mungu alitaka kuwaangamiza wanadamu wote kasoro Nuhu ambaye hakuwa na damu ya kinefili sasa basi kama mnakataa OGU ndio alivusha damu hiyo je nani basi alivusha damu ya wanefili hadi isipotee kwenye gharika

Maana gharika limeisha tu utagundua wanefili tayari walishakuwa na nchi yao wanaishi na wanapigana hadi vita na falme zingine soma mwanzo 14 je walitoka wapi hawa wanefili ilihali gharika liliwamaliza??

Kingine nimrod hakuzaa waamori.... Waamori walitokana na canaan mtoto wa mwisho wa ham. Na hao waamori walikuwa wanajinaisibisha na mfalme Ogu je swali linarudi waamori walitoa wapi unefili ilihali wanefili walimalizwa kwenye gharika??
 
Mkuu Nuhu alikuwa uzao wa SETH yaani mwana wa Mungu na kitabu cha jasher ambacho kinatambuliwa na waandishi wa biblia yaani Nabii musa.... Kinasema mabinti wa methuselah ndio waliolewa na wana wa Nuhu je hiyo damu ya UNEFILI itoke wapi wakati ilikuja baada ya WANA WA MUNGU kuzaa na WANA ADAMU whatever au SETH kuzaa na CAIN

Sioni mahala damu ya cain ilipenya kuendana na official biblical records...... Je wametoka wapi wanefili hao
 
Unaarudi tu mama mno unaijua sifa ya mwamori utaelewa mnefili katoka Wapi
 
Mwanzo 6
1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
3 BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.


Ukisoma kwa umakini utagundua mstari wa pili ndipo walipoanza kuzaliana.... Na hao wanefili wamekuja kutajwa mstari wa 4 ikimaanisha ni zao la mstari wa 2.....

Kuhusu neno WANA WA MUNGU WA KWELI labda muandishi alitaka aweke tu msisitizo ila bado maana ni ile ile kuwa ni WANA WA MUNGU haijalishi alimaanisha wana wa Mungu yaani malaika ama alimaanisha wana wa Mungu yani watu waliokuwa wanamuabudu ila naona hiyo WA KWELI kama msisitizo tu wa sentensi kuonyesha utofauti wa hao wana wa Mungu wa kweli kulinganisha na wanadamu wengine ambao walikuwa hawamuabudu Mungu au vilevile alitaka kuweka msisitizo juu ya Mungu anaeongelea kuwa ni YHWH na sii mwingine

Che mittoga SALA NA KAZI
 
Unaarudi tu mama mno unaijua sifa ya mwamori utaelewa mnefili katoka Wapi
Mkuu swali ni hili naona hatuelewani

Mnefili alikuwepo kabla ya gharika..... Akawepo baada ya gharika je iliwezekanaje ilihali Mungu alishaapa kuwafuta wote kasoro Nuhu ambaye hakuwa ameoa WANADAMU yaani watoto wa CAIN

Hapa tu nisaidie
 
Aisee umenisaidia kuanza kusoma biblia
 
Asante mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…