napata mawazo kadhaa...
1:ni vizuri tujue kusudi la Mungu kumuacha makusudi wakati Lengo lilikuwa ni Kuangamiza dunia yote kwa Maji. Waliopona walipata neema kwa Mungu na Mungu akawaweka wazi. Ingekuwa kuna Mwovu mwingine anapata rehema tungefahamishwa. Na kujua kama hakuwepo, mara baada ya gharika uendelezo wa vizazi haumuonyeshi wala uzao wake.
2:Rahabu alipata rehema, alafu ile adhabu ilikuwa ni regional sio grobal hata ile ya wakaanani. Lengo na hili la nuhu ni tofauti. Mwanzo Mungu anataka kufuta wanadamu wote, hapo case nyingine anataka kufuta baadhi ya watu waovu katika eneo flani tu, huku maeneo mengine ya dunia uovu unaendelea kama kawaida, hivyo muovu mmoja au wachache kupata rehema, au wajumbe wa Mungu kukengeuka na kitotimiza agizo walilopewa kukomesha regional uovu ni tofauti na sidhani kama ni sawa kutumia mifano hiyo.
3: Rahabu ulikuwa mpango wa Mungu. Na kupitia rahabu na Malaya wengine kama Tamari Yesu alizaliwa. na kuna typology nyingi tunapata kwa rahabu na wokovu wa mwanadamu, pamoja na ile kamba nyekundu iliyowaokoa wanadamu. Assumption Mungu aruhusu hybrid ya uovu, ambayo ndiyo ilikuwa lengo lake kuiangamiza hicho kizazi ambacho wewe unataka kiokolewe.
4:Watu sabini kuingia kwenye safina hiyo assumption ni sahihi kwa vitabu na maarifa nje ya bibilia. lkn hiyo hoja tukiijenga kwenye bibilia inaleta ukakasi mwingi.
*Mwanzo 7:7 wanaoingia wanatajwa. Nuhu, wanawe, mke wa nuhu na wake za wanawe. Mungu anawafahamu wana wa wana na huko nyuma kwenye geneology wametajwa lkn hapa hawakutajwa, na imerudiwa zaidi ya mara moja bila kutajwa, sidhani kama kunausahaulifu ila yawezekana ndivyo ilivykuwa.
*Mwanzo 7:13 Wanatajwa hado majina Shemu,hamu na yafethi na wake zao. Nuhu na Mke waku.
*Mwanzo 8:15,16
Wanatoka kwenye safina, Nuhu, mkewe, wanawe na wake za wanawe.
*Mwanzo 9:1 Mungu anawapa amri kama aliyowapa adamu na hawa kabla hawajapata watoto. Zaeni mkaongezeka mkaijaze nchi. Maana yake walikuwa hawana watoto.
*Mwanzo 9:18,19 wanatajwa wana wa nuhu hao watatu, na anapigilia msurmari mstari wa 19, "HAWA WATATU WALIKUWA WANA WA NUHU NA KWA HAWA WATATU NCHI YOTE IKAENEA WATU"
* Mwanzo 10:1 watoto wa hawa jamaa wanaozungumziwa ni Baada ya Gharika, baada ya kuambiwa na Mungu zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi.
5:Katika gharika Umesema Shem Alikuwa na miaka 100. hivyo anatakiwa awe ameshapata watoto.
Mwanzo 7:6, wakati mtoto wa kwanza anaingia na miaka 100, Baba mtu alikiwa na miaka 900.
hapo utaona Nuhu alipata mtoto akiwa na Miaka 800. kwa ratio hiyo tukiihamishia kwenye kizazi chetu au ukitoa sufuri Nuhu aliingia anamiaka 90, mtoto wake akiwa na Miaka 10.
kwa umri wa kabla ya gharika miaka mia ni kama teeneger. Ila kwa ukomavu wao walikuwa wameoa. yawezekana walikiwa hawajaoana muda mrefu au kwa ratio ya baba na watoto, watoto hawakuwa tayari wameshapata watoto.
mkuu nafikili kibibiliabibilia zaidi.