Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Hatujaambiwa walikuwa jinsia gani so huenda kulikuwa na wanefili wa kiume na wakike. Ila uzao wao upo mfano huyu mfalme ogu alikuwa anatawala MAJIJI 60 kwenye himaya ya jamii yake ikimaanisha aliweza kuwa na uzao ingawa hatujaelezwa huyo mke wake alikuwa wa aina gani kma naye ni alikua mnefili ama lah ila kwa kujibu swali lako tuamini tu kuwa kulikuwa na wanawake wanefili pia hivyo walilala nao hao hao
Sahihi kabisa
Kulikuwa Na mijitu ke Na me!
Lakini kwa kuanza mkuu zitto tambua kuwa mbegu ya giants Bado ipo.
 
Hawa wanefili ni matokeo ya malaika kuzaa na binadamu na inasemekana waliangamia na hawapo tena
Kwanini hawa malaika waliozaa na binadamu huwa hawashuki tena duniani na kuja kuzaa na mabinti wengine baada ya gharika hadi mpaka sasa?
Nini kimewazuia
Hapana kiongozi
Hawa wanefili uzao wao Bado upo Na unaendelea Ku exist katika Dunia ya Leo!
Malaika waaasi baada ya kushuka Na kuzini Na dada zetu!
Walitimuliwa mbinguni Na wapo Na adhabu yao siku ya mwisho
Also tambua kuwa Super Natural aliamua kuangamiza Hawa majitu coz ya kulinda utaratibu !Na mfumo wa ulimwengu!
 
Kwanza kuna kitu hakileti ukweli katika Biblia maana hapa katika maandiko ya mwanzo kuna mkanganyiko inaonyesha WANEFILI WALIKUWEPO KABLA YA BINADAMU

1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
Mwanzo 6 :1

2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
Mwanzo 6 :2

4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.
Mwanzo 6 :4
Hapana mkanganyiko hapo kiongozi
Natural Power iliamua Ku balance ulimwengu!
Kumbuka hiyo mijitu Bado Ina exist Na inacontrol Dunia kwa njia zingine
 
zitto junior. Kuna vitu tumefichwa lakini ukweli ni kuwa Mungu alimuumba mwanadamu kukiwa kuna maisha ya viumbe kama binadamu tayali.
Na sijui kwanini Mungu aliamua kutupunguzia maisha wakati viumbe wake waliotutangulia ndio wametufanya tuingie katika majaribu ya kutuhadaa

Ushahidi wa viumbe waliokuwepo kwa mjibu wa Biblia

5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Mwanzo 3 :5

Hapa Mungu anatufananisha na viumbe waliotangulia hapa kuna kitu ukitafakari unapata jibu la kuwepo maisha yaliyoendelea

3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
Mwanzo 6 :3
Kwanini Mungu atupunguzie umri ili hali yeye ndiye katuumbia vitu vya kutupotosha?

Kwanini Mungu asingetupeleka sayari nyingine tuanze maisha yetu yasiyo na mchanganyiko wowote?

Kwanini Mungu asinge tupeleka hata kwenye nyota (jua) proxima century mbali na hapa tukawa mbali na wanefili?

Maana wanefili bado wanaishi ila Mungu kawapunguzia uwezo wa nguvu lakini ndiyo jamii zenye ushawishi na nguvu kiuchumi kuindesha Dunia ndio wazungu wenye macho njano.

Kwa picha hii ni uthibitisho tosha kuwa wapo ila hawana nguvu za mwili ila wamebaki kiakili
Soma maandiko kwa kuelewa
Ni kweli wanefili Bado wapo
Usifananishe hiyo pics Na mijitu
 
Hakuna malaika maana biblia inatuambia walikuwepo wana wa Mungu
Soma hapo chini

2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
Mwanzo 6 :2

4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.
Mwanzo 6 :4
Impongo unakuwa Na pupa ndiyo maana unajikanganya
 
View attachment 758692
Mfalme OG anatajwa kwenye vitabu vya dini kuu tatu za mashariki ya kati i.e uislam,ukristo na uyahudi....

Inaelezwa alikuwa ni mfalme aliyetawala eneo la Canaan (palestina/israel ama jordan ya sasa )katika ulimwengu wa kale takriban miaka zaidi ya 6000 iliopita.... Na inaelezwa ndio mwanadamu aliyeishi zaidi kutokana na kuwa na mwili mkubwa sana aliishi zaidi ya miaka 3500!!! Alikuwa ni mfalme aliyeogopeka sana mashariki ya kati maana alikuwa jitu lenye nguvu na mrefu zaidi ya minazi kama anavyoelezwa na Nabii Amos

Amos 2:9
9 Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini.

Umaarufu wa Mfalme Ogu wa bashan umekuja baada ya historia kubainisha kwamba ndio binadam pekee aliyesalia kwenye gharika nje ya Nuhu na familia yake!!

JE ALIPONAJE GHARIKA

1. Nadharia ya kwanza inasema alikuwa mrefu sana kiasi kwamba maji ya gharika yalimfikia kiunoni!!!!

2. Nadharia ya pili inasema kuwa alikuwa na ukaribu sana na Nuhu hivyo alipewa kazi ya kuiangalia safina kwa nje kuhakikisha haigongi mwamba au mawe makubwa ambayo yangeweza kuipasua safina na hiyo ndio ikawa pona yake!!! Inadaiwa alijishikiza pembeni ya safina ya nuhu ivo hakubebwa na maji ya gharika. Nadharia hii ina mashiko sababu hata baada ya gharika tunaona safina hii ilitua palepale ilipokuwa kabla ya gharika yaani haikuenda mbali kabisa kitu ambacho hakiwezekana kama nguvu ya mafuriko ikizingatiwa lazima boti ingesukumwa maili kadhaa mbele. Kingine kwa akili ya kawaida tu dunia nzima izame alafu ww pekee uwe kwenye boti hivi wanaokufa watakuacha kweli?? Lazima wangetaka kuivamia boti waingia na ukizingatia yalikuwa majitu marefu yangeweza kuipasua pasua ila kwa uwepo wa OG walishindwa maana wangekutana na kipigo cha mbwa mwizi!!

3. Nadharia ya tatu inasema kipindi cha gharika Ogu alikuwa bado hajazaliwa ila mimba yake ilikuwa imeshatungwa na mama yake aliekuwa mke wa Ham hivyo ham asingeweza kumuacha nyuma ingawa inadaiwa mimba hiyo haikuwa ya Ham bali ya Malaika aliyeitwa shamael!! Hivyo damu ya wanefili ikaweza kuvuka gharika kwa staili hiyo kupitia mtoto aliyezaliwa yaani mflame ogu ama canaan ambae watoto wake kwenye biblia wanatajwa kma majitu makubwa ambayo yaliona wanadamu kma panzi!!! Mfano amori aruba anak hivi gilgal amoni yebusi n.k

4. Nadharia ya tatu inasema alienda milimani hivyo gharika haikumkuta. Biblia iko wazi kuwa maji yalifunika MILIMA mirefu kwa futi 15 kwenda juu ina maana kma hyu OG alikuwa na futi zaidi ya 13 pengine 28 kama inavyoelezwa kwenye biblia ina maana kama alipanda milima mrefu zaidi basi hakuweza kumalizwa na gharika!! Simple logic

Mwanzo 7
20 Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano.

Najua kufikia hapa wengi mtasema ni upotoshaji na kwamba ni stori za kijiweni ila hoja hii inapata mashiko kupitia biblia kuwa mfalme OGU alikuwa ndio mnefili pekee aliyepona gharika.

Kumbukumbu la torati 3:11
11 (Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho je! Hakiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni mikono kenda, na upana wake mikono minne, kwa mfano wa mkono wa mtu).

hapa biblia inasema OG NI MREFAI ALIYESALIA tafsiri ya kiingereza inasema LAST OF THE REPHAIMS ikimaanisha ni mnefili pekee aliyesalia baada ya gharika!!!!

BAADA YA GHARIKA
Kupitia vitabu vya dini na kihistoria tunaelezwa kuwa baada ya gharika aliendelea kutawala maeneo ya mashariki ya kati eneo la bashan huko Canaan walipoishi majitu mengine kma wayebusi waamori waamaleki wagilgashite n.k na inasemekana aliishi miaka 3500!! Yaani alikuwepo toka kizazi cha adam hadi kipindi wana wa israel wanarudi canaan !!

MWISHO WAKE
Vitabu vya kidini na historia vinasema mfalme OG au UJ BIN ANAQ kiarabu.... Alipambana na waisraeli waliokuwa wametoka misri kuelekea canaan na katika vita hiyo inaelezwa mfalme Og aliweza kunyanyua mlima mzima!!!! Na kutaka kuutupa kwenye kambi ya waisraeli lakini Inadaiwa kwa bahati mbaya au nzuri mlima ukavunjika katikati hivyo ukamnyima balance akaangukiwa na kipande cha mlima hivo kuumia vibaya na ndipo musa akapata fursa ya kumchoma na mkuki na vita ikawa kma imemalizwa na wanajeshi wake kwa hofu wakakimbia huku na kule na waliobaki wakamalizwa na waisraeli

Kumbukumbu la torati 3
1 Ndipo tukageuka, tukakwea njia ya Bashani; na Ogu, mfalme wa Bashani, akatutokea juu yetu, yeye na watu wake wote, kuja kupigana huko Edrei.
2 BWANA akaniambia, Usimwogope; kwa kuwa nimemtia mkononi mwako, yeye na watu wake wote na nchi yake; nawe utamtenda mfano wa ulivyomtenda Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni.
3 Basi BWANA, Mungu wetu, akamtia mikononi mwetu na Ogu mfalme wa Bashani, na watu wake wote; tukampiga, asisaziwe cho chote.
4 Tukatwaa miji yake yote wakati huo; hapakuwa na mji tusiotwaa kwao miji sitini, nchi yote ya Argobu, ndio ufalme wa Ogu ulio katika Bashani.


NB:kwenye vitabu vya kiyahudi vinadai Mungu wao Israel yaani YHWH alishusha nzige/nyuki wakaula ule mlima kutokea katikati ndio ukagawanyika nusu ila najiuliza nyuki waule mlima ndani ya dakika??? Aseee!!!

Anyway hicho ndio kifo cha mfalme huyu aliyetikisa dunia kwa miaka yake na mpaka leo waisraeli wanatambua ushindi ule kma mkubwa kabisa kwenye historia ya taifa lao!! Hata amos na mfalme daudi huwa wanakikumbuka kisa hiko miaka zaidi ya 600 baadae!!!

Amos 2:9
9 Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini.

Zaburi 135:
10 Aliwapiga mataifa mengi,Akawaua wafalme wenye nguvu;
11 Sihoni, mfalme wa Waamori,Na Ogu, mfalme wa Bashani,Na falme zote za Kanaani


USHAHIDI WA KISAYANSI/KIHISTORIA

Rujm-El hiri or Circle of the rephaites
View attachment 758680
Hii inaelezwa ndio ilikuwa kasri au jumba la ibada la mfalme ogu na mpaka leo masalia yapo huko golan heights, syria (linakaliwa kimabavu na israel).... Mawe yaliyobaki kwa sasa ni zaidi ya 40,000 yamepangwa hadi futi 15 kwenda juu je kuna mtu wa miaka ile angeweza kupanga mawe mazito kwa urefu wa zaidi ya futi 50 kwa wakati huo kama hakua JITU la mfano wa OGU.

2. Karne ya 20 mwanzoni watafiti wa kijerumani waligundua makaburi makubwa ya mawe ambayo yanafanana na hesabu zilizopigwa kuhusu urefu wa mfalme ogu kwenye kitabu cha kumbukumbu la torati..... Kaburi hilo lilipatikana eneo la mto Jabbok, Bashan ambako ndipo mfalme ogu alifia. Na kwa hesabu zao kaburi hilo lina umri wa zaidi ya miaka 6000!!! Muda ambao ndio inasemekana og aliishi hapa duniani
View attachment 758687

3. Mfalme ogu pia alifanikiwa kuandika kitabu chenye sura 7 ambacho kilipatikana takriban miaka 1400 kabla ya kristo ila kilifichwa huko maktaba ya vatican kuaniza karne ya 5 ila baadae kilivujishwa je huu ni ushahidi mwingine kuwa JITU hili liliexist kweli na kuutesa ulimwengu!!!

Karibuni wanajukwaa kwa michango
Naomba kuwasilisha

View attachment 758716
duuuuuu jamaa alikuwa c mchezo kupona ktika gharika walah mtihan mzito
 
Nadharia No2 mkuu naipinga japo sio msomaji wa bible vizuri ,ila kibinadamu.

Hii siyo nadharia ya kwenye Biblia, hakuna sehemu kwenye Biblia ambapo haya yameandikwa. Haya ni maandishi ya baadhi ya Wayahudi na Waarabu.

Alichosena mkuu zitto junior hapa ni nadharia "theory" ambayo kazi zetu wasomaji ni kupima, kuchambua na kutafuta ushahidi ili tupate ukweli. Kubwa ziaidi hii ni nadharia ya kidini na siyo ya kisayansi, hivyo tutakuwa tunakosea sana kama tunazipinga kwa kutumia sayansi.

Yote tisa kama unashangaa hili dogo, utaelezaje lile la Nabii Joshua kugandisha jua siku nzima ili Wahebrania wapigane vita. Au lile la Yona kukaa tumboni mwa nyangumi kwa siku tatu bila kufa...???
 
The so called Great Flood is a myth. There was no such a thing like Great Flood. And for your information kuna visa zaidi ya kumi na tano vinavyo fanana na kisa cha nuhu ambavyo vilitokea maelfu ya miaka kabla ya kutokea kwa kile kinacho itwa Gharika kuu....15 FLOOD MYTHS SIMILAR TO THE STORY OF NOAH
Ushahidi upo mkuu wa kisayansi na kihistoria kuprove kuwa dunia at some point ilikaliwa na maji..... Kasome the canopic theory na ilivyozaa ice age baada ya kuanguka kutoka angani na kujaza dunia nzima na maji ya mafuriko mwishowe ikaganda!!!!

Nliwahi kuweka hapa full documentary ya canopic theory nafkiri kwenye uzi wa kuhusu GIANTS..... Ngoja niitafute niicopy hapa ila gharika is real hata kma halikua la Noah ama hizo 15 myths
 
Back
Top Bottom