Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

kuna jambo linakanganya!! kama unaamin kwamba kuna gharika ilitokea bas huna budi kuamini kuna Mungu. ukiamin juu ya Mungu maana yake unaamini Mungu ni mkuu kuliko huyo Og!! hivyo bas iweje apone na huku lengo la Mungu ni kuangamiza kizazi chote kitakachokua nje ya safina??

lugha rahisi huyu Og alimshinda hadi Mungu. hiyo haiwezekani. ila asante kwa habar yenye kufikirisha
Ndio maana toka mwanzo nikasema hii mada tusiingize mahaba ya dini tufikirie nje ya box mkuu wwe unasema kusupport uwepo wa OG ni kumpinga Mungu?? Je muandishi wa kitabu cha kumbukumbu la torati naye anampinga Mungu??

Kumbukumbu la torati 3:11
11 (Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho je! Hakiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni mikono kenda, na upana wake mikono minne, kwa mfano wa mkono wa mtu

Haya basi tufanye tufanye huyu alidanganya je Vipi kuhusu mstari huu

Mwanzo 6 : 4
4 Wanefili walikuwa duniani siku hizo, na pia baada ya hapo......

Je anaposema wanefili walikuwepo toka enzi hizo na hata baadae alikuwa ana maana gani?? Ina maana naye kapotosha??

Anyway basi tufanye hawa wote walipotosha embu tusaidie basi wanefili mfano wa mfalme OG walirudije duniani kma wote walimalizwa kwenye gharika??? Wana wa aruba,anaki,amoni,wahivi,amori,wayebusi n.k wote walikuwa ni wanefili na joshua anawataja ina maana walirudije duniani if at all wote waliuawa kwenye gharika

Tusaidie hapo ili tujifunze zaidi
 
Nadharia No2 mkuu naipinga japo sio msomaji wa bible vizuri ,ila kibinadamu.

Hata angekuwaje hivi kama inavyosema biblia kuwa maji yalijaa duniani kote mikono kumi na tano (mikono kumi na tano ya wakati huosio sasa) ina maana yalikua maji marefu yenye nguvu unadhani kuna kiumbe kingeweza kabisa kushika safina ili kisiangamie kingali nje ya safina?


Na hio hoja ya kusema kuwa watu wangemvamia.. mkuu maji unayajua nadhani hivi yanavyojua kuwa na nguvu mtu unaweza kumvamia mwenzio? au hata kufikiria kumvamia bila kujiokoa.. Haiwezekani kwakweli.
Tuelimishane vizuri
Hio nadharia ya 3 naweza kuikubali ina make sense mkuu.
1. Ok mikono 15 sio kama ya sasa ina maana kwa vipimo hivo hivo mikono zaidi ya 15 ambao ndio ulikua urefu wa Mfalme ogu nao sio kama wa sasa ikimaanisha bado aliyazidi maji kma alipanda juu ya milima si ndio maana yake???

2. Sijasema wamvamie tu naongelea situation meli imezama alafu wwe unaona kuna boya kweli wote mtamuacha aliye kwenye boya hku mnakufa maji?? Lazma kwenye kutapatapa mtajikuta mnavamia boya lake ili na nyie mjiokoe ssa jiulize dunia nzima inazama alafu unaona boti kubwaaaaa inaelea tu je utakufa bila hata kijaribu kuiparamia ili kujiokoa?? Ssa pata picha lijimtu kma goliath livamie boti si wangeivunjilia mbali!!!

Anyway ni nadharia tu ila zina make sense kwa kiasi chake
 
Sahihi kabisa
Kulikuwa Na mijitu ke Na me!
Lakini kwa kuanza mkuu zitto tambua kuwa mbegu ya giants Bado ipo.
Nimesikia hizi tetesi ila sijawahi kuzikalia chini kuzidadavua..... Embu tupe mbili tatu mkuu
 
Kitu ninachokijua kwa sehemu ndogo tu kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba, Mungu akitaka kufanya jambo lake hashindwi kulifanya, huyo mnefili aliyesalia kwa kufikiri fikiri tu yaweza kuwa alikuwa mimba wakati wa gharika labda.
Kinyume na hapo yaliyobakia yote ni vigumu kukubaliana nayo kwa sababu tangu mvua kunyesha mpaka maji kuanza angalau kupungua ni zaidi ya mwaka! Sasa huyo ni kiumbe gani mwenye mwili ambaye hali wala kunywa kwa mwaka mzima kwenye dharuba nzito namna hiyo?!!!
 
Ushahidi upo mkuu wa kisayansi na kihistoria kuprove kuwa dunia at some point ilikaliwa na maji..... Kasome the canopic theory na ilivyozaa ice age baada ya kuanguka kutoka angani na kujaza dunia nzima na maji ya mafuriko mwishowe ikaganda!!!!

Nliwahi kuweka hapa full documentary ya canopic theory nafkiri kwenye uzi wa kuhusu GIANTS..... Ngoja niitafute niicopy hapa ila gharika is real hata kma halikua la Noah ama hizo 15 myths
Fanya hivyo mzee may be I can change my view cause a critical thinker always changes his view when presented with better argument
 
Kwanza kuna kitu hakileti ukweli katika Biblia maana hapa katika maandiko ya mwanzo kuna mkanganyiko inaonyesha WANEFILI WALIKUWEPO KABLA YA BINADAMU

1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
Mwanzo 6 :1

2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
Mwanzo 6 :2

4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.
Mwanzo 6 :4
Wewe ndo unachanganya huoni amekwambia walijitwalia mabinti? Sasa unaposema Wanefili walikuwepo kabla ya binadamu una maanisha nini?
 
Nilikua nataka nisome hadi mwisho lkn umenimaliza poz yani malaika kazaa na mwanadam?? Hii haiko sawa jaman sisi tunaambiwa malaika hanaga jinsia ngoja tu niishie hapa.
 
Grahnman. Sasa mkuu hapo nimechanganya wapi?
Wana wa Mungu waliwaona wana wa binadamu ya kuwa ni wazuri je wana wa Mungu walikuwa wapi?

Rejea hapa 4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
Mwanzo 3 :4

5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Mwanzo 3 :5

Huyu nyoka alitoka wapi?
Je jamii hii ya wanefili si unaona wamekuwa na ustaarabu kabla ya wanadamu
 
Grahnman. Sasa mkuu hapo nimechanganya wapi?
Wana wa Mungu waliwaona wana wa binadamu ya kuwa ni wazuri je wana wa Mungu walikuwa wapi?

Rejea hapa 4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
Mwanzo 3 :4

5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Mwanzo 3 :5

Huyu nyoka alitoka wapi?
Je jamii hii ya wanefili si unaona wamekuwa na ustaarabu kabla ya wanadamu
Mkuu wana wa Mungu si anamaanisha hao Malaika walioshuka kuja kulala na hao wanawake mkuu
 
Najua kufikia hapa wengi mtasema ni upotoshaji na kwamba ni stori za kijiweni ila hoja hii inapata mashiko kupitia biblia kuwa mfalme OGU alikuwa ndio mnefili pekee aliyepona gharika.
Mwanzo 7:21 Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu;

mkuu source nyingine sawa, ila bibilia hapana. Vilikufa vyote. labda kama swntensi hiyo niliyoiquote ilimaanisha nini.
 
Grahnman. Sasa mkuu hapo nimechanganya wapi?
Wana wa Mungu waliwaona wana wa binadamu ya kuwa ni wazuri je wana wa Mungu walikuwa wapi?

Rejea hapa 4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
Mwanzo 3 :4

5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Mwanzo 3 :5

Huyu nyoka alitoka wapi?
Je jamii hii ya wanefili si unaona wamekuwa na ustaarabu kabla ya wanadamu

Mkuu Point yako ipo sahihi kiasi chake maana hatuna ushahidi wa moja kwa moja lakini inasemekana binadamu alikuwepo kabla ya uumbwaji wa Adamu

Nitarudi ili tusaidiane katika kulifahamu hili ningojee kidoogo
Naja
 
Back
Top Bottom