Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Upo sahihi sanaaa kiongozi
But wachache wanajua A-Z ya ulimwengu huu!
Binafsi kuna WATU walifanikiwa kujua but walizibwa midomo Na wengine waliuliwa
kiukweli mimi huwa najiuliza maswali mengi kuhusu dunia na maisha hadi kichwa kinauma. ila kwa post zako humu inaonyesha kuna kitu unakifahamu kuhusu huu ulimwengu japo kidogo ila sijui ni kwa nini hautaki kukiweka wazi.
 
Duuu imeni inspire ssna hii kitu.
Lakini naamini hata tukiacha hao wanefili....tukiwaangalia akina Adam walikuwa wakubwa.....sio kama sisi
 
Nilikua nataka nisome hadi mwisho lkn umenimaliza poz yani malaika kazaa na mwanadam?? Hii haiko sawa jaman sisi tunaambiwa malaika hanaga jinsia ngoja tu niishie hapa.
Mbona Yesu alizaliwa bila mwanaume kulala na Maria??? Ina maana Roho mtakatifu alikuwa na jinsia hadi apandikize mtoto kwenye kizazi cha maria??

Kama hoja ni sex Majini wanaolala na wanawake wanawezaje?? Hata kma wakiwa ndotoni ila huwa wanaamka asbuhi na kukuta wametumika!!

Kwa ufahamu wangu malaika hawana jinsia ni wakiwa katika mfumo wa kiroho ila wakija hapa duniani huwa lazima wavae mwili ukisoma biblia utaona malaika waliomtembelea Abraham walikuwa wanaonekana ni wanaume!!! Hata waliomtembelea Lutu walionekana ni wanaume na walikula walilala walioga walicheka n.k kma walifanya yote hayo kwanni huamini wanaweza pia kumlala mwanamke/mwanaume???

Tuanzie hapo
 
Mwanzo 7:21 Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu;

mkuu source nyingine sawa, ila bibilia hapana. Vilikufa vyote. labda kama swntensi hiyo niliyoiquote ilimaanisha nini.
Okay nashkuru kwa mchango wako mkuu ila tukijiuliza je wanefili walirudije mkuu baada ya gharika?? Maana Musa anasema wazi kuwa mfalme Ogu ndio mrefai aliebaki sasa alitoka wapi kama walikufa kwenye gharika?? Embu nipe somo hapo

Pia aruba anaki amori amoni hawa wote walikuwa uzao wa wanefili je walitoka wapi au ndio wana wa Mungu walizaa tena na wana wa adamu baada ya gharika???
 
pamoja mkuu. ngoja nitafiti kidogo nitapita kutoa maoni.
maoni yangu yatafungamana na bibilia zaidi.
1:Kama unaamini bibilia ni maandishi sahihi.
2:Kama unaamini Yesu alikuja miaka mingi baada ya gharika ktk umbile la binadamu.
3:Kama unaamini kauli ya Yesu kuwa hata kabla ya Ibrahimu yeye alikuwepo, maana yake hata wakati wa gharika hata kabla ya uumbaji alikuwepo.
4:kama unaamini kama ilivyoandikwa katka kitabu cha waebrania kwamba hakuwahi kitenda dhambi wala kutoa record za uongo.

Hivyo Tunapaswa kuamini maneno ya yesu ya Luka 17:27
Watu waliendelea kula na kunywa, kuoa na kuolewa mpaka wakati ule Noa alipoingia katika safina. Gharika ikatokea na kuwaangamiza wote.

mkui hii inanipa sababu ya kuamini na kuwa hakuna nefili aliyepona. na pili huyo anayetajwa sio nephili wa kiwango cha pre-flood.
inanipa nafasi ya kujifunza.
1:Yawezekana dna za watu wale ziliendelea kuwepo katika ukoo wa nuhu.
2:Yawezekana walikuwa ni watu wakubwa kutokana na vyanzo vingine vya kimabadiliko visivyohusiana na wanefili.
3:Yawezekana Wakawa ni wanadamu wa kawaida ila wenye abdnormal growth mfano goliath na great kali yule mcheza mieleka au Hasheem thabeet.

Fact ya Yesu, kwangu mimi inanifungia mjadala wa kuamini kuna nefili alipona.
ila maelezo yako yananipa changamoto ya kujifunza hao jamaa.

cc
zitto junior
ubarikiwe kwa kutufikirisha mkuu
 
Mbona Yesu alizaliwa bila mwanaume kulala na Maria??? Ina maana Roho mtakatifu alikuwa na jinsia hadi apandikize mtoto kwenye kizazi cha maria??

Kama hoja ni sex Majini wanaolala na wanawake wanawezaje?? Hata kma wakiwa ndotoni ila huwa wanaamka asbuhi na kukuta wametumika!!

Kwa ufahamu wangu malaika hawana jinsia ni wakiwa katika mfumo wa kiroho ila wakija hapa duniani huwa lazima wavae mwili ukisoma biblia utaona malaika waliomtembelea Abraham walikuwa wanaonekana ni wanaume!!! Hata waliomtembelea Lutu walionekana ni wanaume na walikula walilala walioga walicheka n.k kma walifanya yote hayo kwanni huamini wanaweza pia kumlala mwanamke/mwanaume???

Tuanzie hapo
Nakushauri ukasome tena mkuu kwa maana tunaambiwa malaika ambao walimtembelea Ibrahim walienda tu kwa umbile la mwanadam na waliondoka wakaelekea katika kijiji cha sadum kwa lut na walivyofika walikaribishwa na lut hakujua kama hao wageni wake ni malaika kutoka mbinguni wakakaa na wakatengewa chakula wakakaribishwa kula na walikataa na hapo ndipo walimwambia lut kwamba sisi ni malaika kutoka mbinguni tumetumwa kwako ili kukuokoa hivyo unatakiwa ujiandae ucku huu pamoja na watu wako muondoke zenu katika kijiji hiki cz tunataka kukiangamiza. Hakuna hata sehem moja ya andiko inayosema malaika kazaa na mwanadam acheni kupotosha watu bhana.
 
Halafu msipende kuwafananisha malaika na majini jaman ni viumbe wawili tofauti kabisa jaman majini ni kama sisi tu wanadam baadhi ya sifa zao na zetu zinafanana
 
Kitu ninachokijua kwa sehemu ndogo tu kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba, Mungu akitaka kufanya jambo lake hashindwi kulifanya, huyo mnefili aliyesalia kwa kufikiri fikiri tu yaweza kuwa alikuwa mimba wakati wa gharika labda.
Kinyume na hapo yaliyobakia yote ni vigumu kukubaliana nayo kwa sababu tangu mvua kunyesha mpaka maji kuanza angalau kupungua ni zaidi ya mwaka! Sasa huyo ni kiumbe gani mwenye mwili ambaye hali wala kunywa kwa mwaka mzima kwenye dharuba nzito namna hiyo?!!!
Okay mkuu lakini unachotakiwa kujua ni kwamba kama maji yalifika juu ya mlima kwa mikono 15 na huyu jamaa ni mara mbili ya hizo ina maana mpaka mwaka unaisha angeweza kuishi juu ya milima na chakula angeweza kula mizoga ya wanyama ama samaki pia waliofurumushwa na mafuriko kutoka baharini

Kuna kitabu nmesoma ambayo ni true story ya wanajeshi wa marekani walifurumushwa na mabomu ya wajapani na ndege zao kuanguka pacific

Wale jamaa walikuwa 4 walisurvive kwenye BOYA kwa miezi miwili..... Ndio miezi miwili na hawakuwa na chakula ivo walikuwa wanabahatisha samaki wanaoelea juu wanakula wabichi na sometimes kulala njaa ila walimaliza miezi miwili ndio sembuse LIJIMTU kma MFALME OGU ambalo linaweza kamata nyangumi kwa kiganja???
 
Duh
 
Halafu msipende kuwafananisha malaika na majini jaman ni viumbe wawili tofauti kabisa jaman majini ni kama sisi tu wanadam baadhi ya sifa zao na zetu zinafanana
Hakuna anayewafananisha tunatoa tu hoja kwamba kwakuwa wote ni ROHO basi kuna characters watashabihiana tofauti kabisa na mwanadamu ambaye ni mwili tu

Mfano kwenye biblia malaika walikula,walilala,walipigana na yakobo!!,walioga n.k wakiwa hapa duniani je kwanni kumlala mwanamke washindwe??

Kwenye story ya lutu tunaona kuna majamaa waliwatamani malaika sababu ya uzuri wao hadi wakataka kulala nao ikimaanisha walikuwa na maungo kma tu ya binadamu wengine hapa duniani sasa kivp kusex ndio washindwe??

Kama issue ni uzao Yesu alipandikizwa kwenye tumbo la maria bila mtu kusex na maria why malaika wengine washindwe??

Tuanzie hapo
 
Okay mkuu lakini unachotakiwa kujua ni kwamba kama maji yalifika juu ya mlima kwa mikono 15 na huyu jamaa ni mara mbili ya hizo ina maana mpaka mwaka unaisha angeweza kuishi juu ya milima na chakula angeweza kula mizoga ya wanyama ama samaki pia waliofurumushwa na mafuriko kutoka baharini

Kuna kitabu nmesoma ambayo ni true story ya wanajeshi wa marekani walifurumushwa na mabomu ya wajapani na ndege zao kuanguka pacific

Wale jamaa walikuwa 4 walisurvive kwenye BOYA kwa miezi miwili..... Ndio miezi miwili na hawakuwa na chakula ivo walikuwa wanabahatisha samaki wanaoelea juu wanakula wabichi na sometimes kulala njaa ila walimaliza miezi miwili ndio sembuse LIJIMTU kma MFALME OGU ambalo linaweza kamata nyangumi kwa kiganja???
assumption kuwa jamaa alikuwepo:
turudi kwenye situation ya maji yaliyosemwa katika mwanzo.

kama ilivyovigumu kusimama kwenye mafuriko ya maji ya mto msimbazi. Atawezaje kusimama kwenye maji ambayo sio tu yanatoka juu bali ardhi ilikuwa pia ikitoa maji.
Pili lengo la Mungu lilikuwa ni kuwaangamiza wanadamu wote kwa staili ile, je atawezaje kiruhusu aina ya maangamizi ambayo yatampa fursa mmojawapo kutoroka?

Yale maji yalikuwa ni combination ya "Fountain of the deep" na "product ya Windows of heaven"

maelezo yako bado kama yanatoa nafasi finyu hau haipo kabisa kwa huyo kiumbe kuescape ikiwa unakubaliana na complications za yale mafuriko kama yanavyoelezwa hapo mwanzo.
 
mwanzo 7:21
Viumbe wote hai katika nchi wakafa. Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama wa porini, makundi ya viumbe wote katika nchi kavu na wanadamu wote; 22naam, kila kiumbe hai katika nchi kavu kilikufa.
 
Zitto junior

Hebu tuanzie hapa kwanza afu tuendelee naimani tutapata kitu

Ogu
BibliaJinaKumbukumbu la Torati

640px-Ostjordanische_Amoriterreiche.png

Ogu ni jina la mfalme wa Waamorialiyetawala sehemu za Bashani. Ogu anatajwa katika Biblia kwenye vitabuvya Hesabu 21 na Kumbukumbu la Torati 3, kwa kifupi pia katika Zaburi135:11 na 136:20. Inawezekana ya kwamba kutajwa kwa "Mwamori" katika Amosi 2:9 ni pia kuhusu Ogu.

Ogu katika Biblia
Katika vitabu vya Hesabu na Kumbukumbu la Torati anaonyeshwa kama mfalme ambaye aliyekataa ombi la Wanaisraeli la kupita katika nchi yake wakitokea Misri na kuelekea Kanaani. Ogu alikataa akakusanya jeshi lake na kuwashambulia Wanaisraeli. Karibu na mji wa Ederei (leo: Dar'a nchini Syria) alishindwa. Wanaisraeli waliteka nchi yake ikawa makazi ya kabila la Manase.

Ogu anakumbukwa katika masimulizi ya Biblia kama jitu akiwa na kitandachenye urefu wa mikono yaani dhiraa10 sawa na mita 4-5.

Katika masimulizi ya Wayahudi sifa hiyo iliendelea kuongezeka; katika Kitabu cha Amosi 2,9 anatajwa (bila kusema jina) kama "Mwamori" "nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni".

Ogu katika mapokeo ya Kiyahudi
Wataalamu Wayahudi wa baadaye waliona ya kwamba vipimo vya Kumb. 3 kuhusu kitanda chake chenye urefu wa mikono yaani dhiraa 10, sawa na mita 4-5, vilihusu mkono wa hilo jitu lenyewe, hivyo walimwona mkubwa zaidi tena.

Kwenye kitabu Berakhot cha TalmudiOgu anasimuliwa ya kwamba aliweza kuinua mlima aliotaka kurusha dhidi ya Wanaisraeli, lakini Mungu alimzuia Katika kitabu cha Nidah katika Talmudi Ogu anasemekana ni mtu aliyeishi kabla ya gharika kuu ya Nuhu akiwa ni mmoja wa wale ambao walitunzwa.

Ogu nje ya Biblia
Kwa jumla habari haba zilizohifadhiwa juu ya Ogu ziko ndani ya Biblia. Nje yake jina la Ogu linaonekana kwenye kigae cha mwandiko wa kikabarikutoka mji wa Biblos

Ogu katika Uislamu
Masimulizi ya Kiyahudi yalipokewa na Waislamu na kubadilishwa tena. Hapa anajulikana kwa Kiarabu kama ‘Uj bin Unuq / ‘Anaq عوج بن عنق. Ushahidi uko kwa Al Tabari aliyeandika ya kwamba maiti ya Udj ilikuwa kama daraja juu ya mto Naili, pia wengine.

Kutoka mapokeo hayo ya Kiislamu jina lilifika pia katika hekaya za Waswahilikwa umbo la Unju bin Unuk

Kwa msaaada wa mtandao

Asalaam kudo
 
Back
Top Bottom