Zitto junior
Hebu tuanzie hapa kwanza afu tuendelee naimani tutapata kitu
Ogu
BibliaJinaKumbukumbu la Torati
Ogu ni
jina la
mfalme wa
Waamorialiyetawala sehemu za Bashani. Ogu anatajwa katika
Biblia kwenye
vitabuvya
Hesabu 21 na
Kumbukumbu la Torati 3, kwa kifupi pia katika
Zaburi135:11 na 136:20. Inawezekana ya kwamba kutajwa kwa "Mwamori" katika
Amosi 2:9 ni pia kuhusu Ogu.
Ogu katika Biblia
Katika vitabu vya Hesabu na Kumbukumbu la Torati anaonyeshwa kama mfalme ambaye aliyekataa ombi la
Wanaisraeli la kupita katika nchi yake wakitokea
Misri na kuelekea
Kanaani. Ogu alikataa akakusanya
jeshi lake na kuwashambulia Wanaisraeli. Karibu na
mji wa Ederei (leo: Dar'a nchini
Syria) alishindwa. Wanaisraeli waliteka nchi yake ikawa makazi ya
kabila la Manase.
Ogu anakumbukwa katika masimulizi ya Biblia kama jitu akiwa na
kitandachenye
urefu wa
mikono yaani
dhiraa10 sawa na
mita 4-5.
Katika masimulizi ya
Wayahudi sifa hiyo iliendelea kuongezeka; katika
Kitabu cha Amosi 2,9 anatajwa (bila kusema jina) kama "Mwamori" "nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa
mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni".
Ogu katika mapokeo ya Kiyahudi
Wataalamu Wayahudi wa baadaye waliona ya kwamba
vipimo vya Kumb. 3 kuhusu kitanda chake chenye urefu wa mikono yaani
dhiraa 10, sawa na
mita 4-5, vilihusu mkono wa hilo jitu lenyewe, hivyo walimwona mkubwa zaidi tena.
Kwenye
kitabu Berakhot cha
TalmudiOgu anasimuliwa ya kwamba aliweza kuinua
mlima aliotaka kurusha dhidi ya Wanaisraeli, lakini
Mungu alimzuia Katika kitabu cha Nidah katika Talmudi Ogu anasemekana ni mtu aliyeishi kabla ya gharika kuu ya
Nuhu akiwa ni mmoja wa wale ambao walitunzwa.
Ogu nje ya Biblia
Kwa jumla habari haba zilizohifadhiwa juu ya Ogu ziko ndani ya Biblia. Nje yake jina la Ogu linaonekana kwenye
kigae cha mwandiko wa kikabarikutoka
mji wa Biblos
Ogu katika Uislamu
Masimulizi ya Kiyahudi yalipokewa na
Waislamu na kubadilishwa tena. Hapa anajulikana kwa
Kiarabu kama ‘Uj bin Unuq / ‘Anaq عوج بن عنق. Ushahidi uko kwa Al Tabari aliyeandika ya kwamba
maiti ya Udj ilikuwa kama
daraja juu ya
mto Naili, pia wengine.
Kutoka
mapokeo hayo ya Kiislamu jina lilifika pia katika
hekaya za
Waswahilikwa
umbo la
Unju bin Unuk
Kwa msaaada wa mtandao
Asalaam kudo