Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu


Sawa Chief hapo nimekwelewa
 
Umesoma nani anayeongea na wakati gani mkuu
Malaika walifungwa kuzimu nani kasema unajua maana ya agano jipya na la kale su imagino ri agano jipya su la kale ni vitabu vya biblia tu malaika mkuu shetani yuko kuzimu baada ya yesu kufufuka na wangine ndo unasikia wanataabisha watu kabla ya yesu shetani hakuwa kuzimu alikuwa duniani soma uelewebiblia na nyakati na majira ya biblia mkuu unapouliza swali kama hilo nazidi kuona ulivyo lalia vitabu vya miongozo yaani vilivyoongezwa tu
Zaidi ya kuchambua ndani ya Biblia mkuu hakuna malaika aliyekuwa kuzimu na kuzimu kulikuwa na wafu tu
Angalia mwazilishi wa vita na wanadamu alikuwa shetani mwenyewe ndo maana sodoma na gomora ilikuwa hatari mbona Leo Mungu ajawateketeza baadhi watu waovu kama sodoma ujue agano ni nini na linamaanisha nini su nifupishe
Hao malaika walitupwa Wapi baada ya kuasi katika agano la kale weka reference hapa
Au ujue kuwa walioperate mpaka yesu alipofufuka ndo kufungiwa tena aliyefungiwa ni shetani ambaye ni kiongozi wao na jamaa bado wapo ila uwezo wa kuingilia walimwengu umekua tofauti kwa sababu Baba lao lilitupwa kuzimu na limefungwa kwa kunyanganywa mamlaka so hautawaona wanefili tena kipindi hiki
 
Mkuu,kwa namna ninavyoelewa mimi ni kwamba,kwanza suala au dhana ya malaika "kufungwa" kwa upande wangu bado halijakaa sawa....

Nasema hivui kwa sababu sijawahi kuelewa huko "kufungwa" ni kwa namna ipi,lakini pia bado sijaelewa kama walifungwa kweli walifungwa wakati upi. Nasema hivi kwasababu kwenye kitabu cha Ayubu ule ukurasa wa kwanza tu kuna kisa cha Shetani kujumuika na Malaika [Wana wa Mungu] mbinguni huko na alipoulizwa alisema kuwa ametokea duniani alikokuwa anazunguka zunguka. Ukiacha tukio hili kuna tukio la Shetani kufungwa miaka 1000 kwenye kitabu cha Ufunuo baada ya ile dhiki kuu.Hapa inaonekana huyu balaa alikuwa hajafungwa au kuwepo kifungoni...

Ayubu 1:7
7 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.

Ufunuo wa Yohana 20:1-3

1 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.

2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;

3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.




Sasa kwa mantiki hii ni vigumu sana kuhitimisha tu wamefungwa kuzimu na hawatoki humo [kwa maana ya wengi na iliyopelekea kuleta swali uliloniuliza] na kufanya swali la kizazi chao kuwa kuendelea kuwepo kuwa ni gumu zaidi...

Jambo la msingi ambalo wengi hapa wanapaswa walielewe ni kwamba Wanefili walikuwepo hata baada ya Gharika.Waliendelea namna ipi hilo ni jambo la kufanyia utafiti lakini kuna nadharia moja inaeleza kuwa,kwasababu viumbe hawa [Wanefili] walikuwa wanauelewa mkubwa sana wa kanuni za maumbile [physical law] waliweza kupona kwenye gharika kwa namna moja au nyingine au hawakupona lakini malaika wale waliendeleza kizazi kile kwa namna ile ile kwasababu wao gharika haikuwahusu...

Ukiniuliza mimi binafsi naelewaje au kufahamuje viumbe hawa waliwezaje kupatikana baada ya gharika,kama msingi wa swali lako ulivyo ukweli ni kwamba hadi sasa sijapata jibu lenye mashiko au niseme tu kuwa sifahamu ilikuwaje wakaendelea kuwepo lakini nina uhakika kuwa waliendelea kuwepo....

Nina dhana nyingi tu ambazo zinajaribu kuelezea hawa majitu waliendeleaje kuwepo na bado naendelea kufuatilia....
Kwanza mkuu nianze kwa kukueleza kuwa ishu ya Yericko ni tofauti sana na hii japokuwa inahusiana pia. ni tofauti kwasababu Rahabu [kama sijakosea] alitoa msaada kwa wapelelezi wa Israeli na wakamuahidi watamuacha hai.Hapa kuna jambo kubwa sana mkuu kwasababu bloodline ya huyu mwanamke ndiyo hii tunayokuja kuipata kwa Yesu.Yaani uzao wa Rahabu ndio blood line ya Yesu. Hili niliache kwa sasa maana kuna mengi hapo,lakini pia unapaswa ukumbuke kuwa maelekezo ya Mungu ya kuwaangamiza Wakanaani ilikuwa ni wanaume wote na wanawake waliomjua mwanaume.Jambo hili linasababishwa na suala hili hili la Wanefili.Hili nalo lina mengi lakini ninachotaka ukione hapa ni kwamba kitendo cha Mungu kuruhusu Rahabu kuendelea kuishi bila kujali alikuwa ni kahaba na kitendo cha kuwa kahaba kina maana kuwa na uwezekano wa kuwa na watoto wenye damu hii ya Wanefili kinaleta maswali mengine magumu sana...

.....sasa basi,kunakuwa na sababu ya kahaba huyo kuachwa hai,je kuna sababu ipi ya Wanefili wa kabla ya gharika kuachwa? [Japokuwa sijasema hawakuachwa] Dhana ya huyu OG kumsaidia nuhu ni ya kufikirika zaidi kwasababu haina ushahidi wa kimaandiko kuwa alimsaidia Nuhu,ni mawazo ya watu tu. Kwa maoni yangu,kama walipona basi huenda ni kwa sababu ambayo huenda hatujaijuwa bado....

Kuhusu Tekinolojia ya wakati huo ni kwamba mimi binafsi ninaamini kuwa wakati ule kulikuwa na maendeleo ya kiteknolojia zaidi ya wakati huu.Ninasema hivi kwasababu nimepitia dicumentary nyingi tu zikielezea maendeleo ya hatari ya wakati huo.Kwa kukuonesha hili nenda katafute documentary moja inaitwa "Technology of the Fallen" utapata mwanga.Maendeleo haya yalitumiwa na binadamu wengine,sisemi kuwa Nuhu aliitumia isipokuwa nataka tu nianze kubadili mtazamo wako kuwa zamani hizo hawakuwa na maendeleo au maendeleo yao yalikuwa duni kuliko leo....

....Mungu kaka alivyo yeye ndiye baba wa teknolojia yote,malaika waasi waliona namna Mungu alivyokuwa anaweka kanuni zote za Physics na vitu vyote kwa ujumla wake na wakaweza kuwa na uelewa mkubwa sana wa kanuni hizo na zingine nyingi.Kumbuka tu ni malaika hao hao waliokuja kuleta maarifa haya kwa binadamu,maarifa ambayo kimsingi binadamu hakupaswa kuyafahamu,maarifa haya yanaitwa "forbiden knowledge".Binadamu hakupaswa kuyaelewa maarifa haya kwasababu hakuumbwa kuyahimili na ndiyo maana walipoyajuwa walianza kuangamizana wao kwa wao na hata leo unaona yanavyotutesa.Sasa kama hawa waliona tu na wakawa na ujuzi huo,vipi Mungu mwenyewe ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa kujengwa safina hadi gharika yenyewe ambaye ndiye mwenye kanuni na ujuzi huo?

Ninachotaka ukielewe hapa ni kwamba,jambo lilalosimamiwa na Mungu mwenyewe weka pembeni yanayowezekana na yasiyowezekana kwa binadamu. Kwa hiyo dhana ya huyo OG "kumsaidia" Nuhu siioni kama ina mashiko kwasababu tu Nuhu "asingeweza" kuijenga mwenyewe....
Hawa Wanefili hawajaisha mkuu,tena nasema hivi kwa uhakika kabisa...

Ni nini kinanipa uhakika mkubwa hivi?

Vipo vingi tu na cha kwanza ni Biblia yenyewe....

Mosi,Biblia yenyewe inakiri Wanefili walikuwepo hata baada ya gharika [mwanzo 6:6],kama walikuwepo baada ya gharika basi watakuwepo hadi leo maana sijaona sababu ya kutokuwepo kwao....

Pili,Yesu mwenyewe alisema "kama ilivyokuwa nyakati za Nuhu ndivyo itakavyokuwa wakati wa kuja kwake mwana wa Adamu" hii inamaana kuwa,moja ya alama za kurudi Yesu mara ya pili ni uwepo wa mambo kama ya nyakati za Nuhu na moja ya mambo ya wakati ule ni uwepo wa Wanefili...

Tatu,utafiti ambao umeshafanywa na watu wengi sana unaonesha kuwa Majitu haya yapo hadi leo hivyo sina sababu ya kupinga na nimeshaangalia video moja kutoka kwa mtu aliyeshuhudia kuona majitu haya kwenye D.A.M.Bs [Deep Underground Military Bases] zilizoko karibu dunia nzima chini ardhini na yanachapa kazi kabisa. Kilichoko huku juu ni mfano wa kilichoko huko chini.Majiji unayoyaona huku juu ni madogo sana kwa size ya majiji yaliyoko huko chini ardhini ma majiji yote yameunganishwa kwa barabara zilizojengwa kwa viwango vya hali ya juu kiteknolojia,ngoja niishie hapa kwenye hili...

Nadhani swali litakalofuatia hapa ni kuhusu sababu za majitu haya kufichwa au kujificha.Sababu namba moja iliyofanya haya ni udanganyifu....

Ni udanganyifu namna gani?

Kwanza kabisa baada ya gharika Shetani aliamua kutengeneza namna mpya ya kukabiliana na Mungu na njia hiyo ni udanganyifu. Udanganyifu wa kwanza kabisa ni kuhakikisha kile ambacho Mungu anawaeleza binadamu kionekane ni uwongo.Mojawapo wa mfano wa jambo hili ni suala hili la uwepo Mjitu haya.Shetani aliamua kuendesha harakati zake mafichoni huko na siyo wazi maana kama ikiwa siyo mafichoni watu wataona majitu haya na kuverify maelezo ya kwenye Biblia kuwa ni kweli yalikuwepo majitu na hili lina madhara makubwa sana kwao maana kuna mtaalam mmoja wa masuala ya Evolution alisema kuwa kama itaonekana ni kweli kulikuwepo Wanefili basi evolution inakufa kifo cha kibudu.Kuna aina nyingi sana za udanganyifu haswa kwenye historia ambako ndiko kwenye msingi mkubwa sana wa kuona Mungu anasema kweli namna ipi kwenye kwenye Biblia na maeneo mengine.

Hii ndio sababu moja na ndogo sana na zipo nyingi sana na nadhani hii inatosha kwa hapa....

Ni kweli kuwa viongozi wa dunia wengi ni bloodline isiyokuwa na asili ya binadamu,Moja ya damu inayosadikiwa haina asili ya binadamu inaitwa RH-Negative,nakupa kazi mkuu kafukue ufahamu mengi kuhusu group hili la damu....

Kuna namna ambayo unaweza kuwa na bloodline ya Wanefili na hutakuwa na umbo kubwa na hili linaratibiwa kwenye DNA yako na hiki ndicho alichokifanya shetani ili kuendelea kufanya kazi yake kwa kutumia kizazi chake.Kwa namna hii hata leo tuna "Wanefili" lakini hawaonekani kwa namna inayotarajiwa na wengi kuwa Mnefili ni mwenye umbo kubwa...

Hii siyo ajabu kwasababu ukiwafuatilia marais wa Marekani kwa mfano unaona kabisa ni bloodline moja na inakwenda kuungana na bloodline ya Royal Family kule UK.Brad Pit naye ni blood line hii,ukiangalia hakuzaa na Angelina Jolie kwa bahati mbaya maana naye pia ni bloodline hii hii...

Nadhani kuna mtu anaweza hoji juu ya Barack Obama na bloodline yake,ninachotaka kusema hapa ni kwamba kuna mengi ukiyajuwa kuhusu mtu huyo unaweza baki mdomo wazi...

Acha niishie hapo kwa leo mkuu....

Mungu akubariki sana..

Tuombe uzima tuendelee kupeana kiduchu kiduchu namna hii....
 
Ufunuo 20:1-3
1 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.

2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;

3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.




Hapa Shetani alifungwa kuzimu na hii ni baada ya kufufuka Yesu.....

Dhana na kuwa malaika wamefungwa kwa maana physical huwa ina matatizo mengi sana.Ukiangalia kinachoendeleaduniani leo ni ngumu sana kuona kuwa ni kweli kafungwa kwa namna mnayoisema ninyi....

Ninaamini maandiko yalikuwa yanamaanisha kitu kingine kabisa yaliposema "wamefungwa"...
 
Kwangu mimi hao wanaoitwa Wayahudi siyo Wayahudi watoto wa Yakobo....
 
Aiseeee.... Mkuu Eiyer indeed wewe ni true great thinker maana umenipa material zaidi ya niliohitaji na nimegundua sifahamu hata 2% ya mambo ya sirini ya dunia hii ila umenipa mwanga nitatafiti hayo ulionitonya ili niongeze maarifa na kupata majibu ya maswali ninayojiuliza.

Once again nashkuru kwa kuja kutupa darasa murua kabisa ila usiende mbali sana kuna mada nyingine nimeipandisha ila mods hawajaiachia na nategemea utakuja kutupa darasa tena

Kudos!
 
Hakuna ukweli wowote hapa na hizo nadharia zako pitia maandiko matakatifu then njoo tena
Nilipitia ndio uwezo wangu ukaishia hapo ndio maana nikafungua thread so nategemea wasomaji kma ww ndio mtusaidie kupata majibu so karibu utuambie ukweli ni upi

Ahsante
 
Tuko pamojakiongozi...

Tunachojuwa ni kama punje moja ya mchanga wa bahari,ni kama hatujuwi kabisa...

Tuendelee kuombeana uzima tuendelee kujuzana kadiri ya tunavyowezeshwa na Mungu wetu...

Barikiwa sana mkuu...
 
Rudi kwenye siasa,maana siasa ndo huhitaji kurembesha unachoongea,biblia haina kutembesha wala kukoleza,ni black inatamkwa black white inatamkwa white,hakuna sehemu ya biblia inayotamka hayo aliyoyamka na unayolazimisha wewe kuwa huyo mtu aliyafanya,narudia aliyafanya siyo kutajwa kwake jina,nnachoamini binafsi ni simulizi za biblia na siyo simulizi za mtaani,na nnaongelea kile nnachokisoma,km unajua na siyo kukarilishwa,nipe mstari ama sura ama ukurasa unaoongelea hayo juu ya mtu hyu,
Mngeongelea kadri ya hadithi zenu za vijiweni na siyo kuamunisha watu kuwa matendo yote mlomjazia jamaa yamenenwa ktk biblia,
Usiumie na mm kusema haya,
Acha blah blaha,
 
Tatizo lako unataka kulazimisha mambo na uelewa wako ukawa sahihi,
Nnachokataa Mimi ni kuisingizia biblia,
Unapoongea jambo bainisha kipi kimesemwa na biblia na kipi hakijasemwa ila umekipata kwingine,
Rudia kusoma mafungu aliyotoa,halafu wianisha na matendo yaliyohadithiwa kwa kukolezwa juu ya mtu huyu,
Narudia kuongea hadithi kwa mujibu wa biblia juu ya mtu huyu hazipo hivyo,kwa hiyo tunapo ongelea jambo tubainishe kuwa hili ni la chanzo cha biblia na hii ni la vyanzo vingine km hadithi za mtaani ama kwenye kahawa ama vitabu vingine,usisingizie vyanzo ili kutaka kuaminika,
 
Nianze na fungu ulilotoa,
Nioneshe wapi amosi kasema jamaa alitaka kuinua mlima,
Lkn nikusihi usisome biblia kimbumbumbu,usisome biblia km style anayotumia bata kula,
Usimeze vizima vizima,cheua,
Biblia inapofananisha mtu na kiumbe kingine haiwianishi kwa vigezo unavyodhania ww,biblia hutamka sifa hizo km mifano ya sifa ktk kuwafahamisha watu juu ya jambo siyo uwiano wa jambo km lilivyotajwa,(vivumishi)
Mf.biblia ilipomuita Petro mwamba unataka kusema ilimaanisha petro kaumbwa kwa lava km mwamba?,ama mwili wake unaugumu na tabia na hali sawa na mwamba? Kiasi ambacho hata uzito na uimara wa mwili wa petro ulifanana na mwamba?
Jiulize hili na utafakari,
Mf.mwingine ni km biblia ilipotaja 666,haikumaanisha namba zenye umbile huo tajwa,lilikuwa ni neno la kumteta ama kumzungumzia adui yao kimafumbo japo mbumbumbu wa biblia wanalimeza na kulitafsiri zimazima wanapotoka,
Biblia imewafananisha watu na tabia za vitu vingi sana,
Mf.mwingine,Yesu anaitwa mwanakondoo,inamaana anamanyoya km kondoo,alikuwa na kimo umbile na nguvu km kondoo?
Yesu anaitwa pia simba wa yuda inamaana alikuwa physically km simba?
Ili ujue kilichowianishwa kwa huyo mtu siyo kimo sahihi cha mti ila ni muonekano wake awapo ktk kundi la watu nijuze km miti yooote ya aina tajwa ina height sawa na uliyosema,
Acheni blah blah
Na msichukie kuambiwamnaongea na kutafsiri kipotofu,
Wapo watu walifananishwa na tai si kwamba wanaruka km tai,
 


Kuwa mpole Chief huko tushatoka tangu Jana na kuendeleza mjadala uliofungwa ni kujirudisha utoto

Tuache utoto tungojee thread nyingine iliozuiliwa na Mods

Watu kama nyinyi hata darasani walikuwepo,hawakupenda kushea mambo wanayoyajua na wengine na hata kama hawajui hawakutaka kuonekana hawajui

Chief maandiko yoote na vifungu watu wameweka kweli wewe hujaona hata kimoja? Chenye kukupa uchangamsho wa fikira! Japo ili angalau uje hapa utufunze na sisi wenye simulizi za vijiweni ?

Chief umeshindwa kuja kutuelimisha na mandiko ya biblia kuhusu upotoshaji wa simulizi zetu za vijiweni kweli?

Hebu jipange hata kwa nusu saa tu pengine waeza rudi na nondo nzuri zaidi ukatushawishi kuanza upya mjadala
 
Definetly
Wasoma vijarida vya sani wamegeuka wataalamu wa maneno yaMungu,
 
Ulichoongea saa hizi ni tofauti na ulichoongea awali hadi ukatuletea actual height ya huo mti ili tu kutulinganishia urefu,
Nadhani umegundua kuwa ulipotoka ktk ufahamu wako wa jambo hili na umeshindwa kukiri ulipotoka sasa unaamua kujitutumua kuwa ulimaanisha hili,
Kili ulipotoka
NB.hatupingi kuwa hakuwepo
Hatupingi kuwa hakuwa na nguvu zaidi ya binadamu wa kawaida
Hatupingi kuwa hakuwa na kimo zaidi ya binadamu wa kawaida,
Tunapinga chumvi za mtaani,
Tunapinga ulinganishaji wa kimbumbumbu
 
Unaposema utoto unajitambulisha ulivyo km kipofu aliyepata nafasi ya kuona na akaona punda hivyo kila kitu ukimuambia anawianisha na punda,
Unataka kunambia huwa ktk mijadala hakuna nyongeza,
Huwa hakuna kujibu ulichoulizwa Jana,
Walioongea wameingelea ufahamu wao,Na mm niliyenukuliwa napaswa kujibu ufahamu wangu maana mm ndo nilinukuliwa,
Tabia yako ya kushinda humu sababu ya kukosa majukumu mengine siyo kipimo cha usahihi wa namna tunavyopaswa kuenenda ktk mijadala ya humu,
Muda ww unapokuwa humu fulltime mm nakuwa nakuandalieni ada na mengineyo,
 
Mkuu utawezaje kujua kama Padre Titus Amigu ndo Zitto Junior ama ndo Mitale na Midimu?
Duuh hapo sasa ila yatupasa kuwa tunawatafuta hawa watu physically kwa majina yao halisi kuliko haya ya bandia
 

Ahsante Chief mungu awe nawe kwa kila jambo utendalo na akusamehe makosa yako maana hujui utendalo

Enenda katika imani ya bwana na yafanye matendo yako yawe nguzo njema ya maisha yako bila kumchukiza muumba wako

Bwana awe nawe na ninamwomba mungu amfanye ndugu yangu Da'vinsi asipite huku maana shetani anaweza kuijaribu imani yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…