Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

kiongoz sasa tukienda kwa kubuni tu kuwa wana wa Mungu ndio malaika hapo tutakua tunapotosha

MAANA YA WANA WA MUNGU NA WANA WA WANADAMU
1. WANA WA MUNGU:
a. WANAOITWA WANA WA MUNGU KWA JINSI YA KIMWILI - ni wa uzao wa Adamu kupitia Sethi, walikuwa wa kwanza kuliitia Jina la BWANA. Mwanzo 4:25 Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua. 26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la BWANA.
b. WANAOITWA WANA WA MUNGU KWA JINSI YA KIROHO – Ni wa uzao wa Mungu kwa kwa BWANA YESU KRISTO kupitia ya Roho Mtakatifu; yaani ni wale waliozaliwa mara ya pili kiroho. Yohana 1:9 Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. 10 Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. 11 Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. 12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. Yohana 3:3 YESU akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5 YESU akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. Warumi 8:14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. 15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. 16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. 1Yohana 3:1 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. 3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.


2. JE, MALAIKA NI WANA WA MUNGU?
Tunasoma hivi, katika Waebrania 1:5 Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana? 6 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika wote wa Mungu. 7 Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto. 8 Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. ... 13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? 14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Hivyo hapa tunapata jibu ya kwamba: MALAIKA NI WA TUMISHI TU, ILA WATU HUWAITA WANA WA MIUNGU, kutokana na imani za kale kuhusu uwepo wa miungu mingi ya kipagani, kama ile ya Babeli au hasa ile masimulizi ya kigiriki. Kwa mfano katika Danieli 3: 23 Na watu hao watatu, Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakaanguka, hali wamefungwa, katikati ya ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. 24 Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme. 25 Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.

3. WANA WA WANADAMU
a. WANA WA WANADAMU WA UZAO WA ADAMU KUPITIA KAINI. Mwanzo 4: 16 Kaini akatoka mbele za uso wa BWANA, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni. 17 Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe. 18 Henoko akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli; Mehuyaeli akamzaa Methushaeli; Methushaeli akamzaa Lameki. 19 Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila. 20 Ada akamzaa Yabali; huyo ndiye baba yao wakaao katika hema na kufuga wanyama. 21 Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba yao wapigao kinubi na filimbi. 22 Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na umbu lake Tubal-kaini alikuwa Naama. 23 Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua;
b. WANA WA WANADAMU WA MCHANGANYIKO (Yaani, Machotara au Haibridi)- ni wa uzao wa WANA WA MUNGU AMBAO HAWAKUPANDIKIZWA NGUVU YA UZAO WA MAJITU na wa WANA WA WANADAMU WALIOPANDIKIZWA NGUVU YA UZAO WA MAJITU NDANI YAKE (Hakuna jipya chini ya mbingu! - yaani malaika waovu(mapepo?) yaliwekea baadhi wanaume wa wana wa wanadamu vinasaba (genes, engelic genes; kama wafanyavyo mafundi wa genetical engeneering-ili kuzalisha miili tu iliyo hai(pia wanefili=mijusi, ile iitwayo dinosaurs) kama WANYAMA MWENYE au MIJUSI (DINOSAURS?) YENYE UMBILE LA KIBINADAMU, ambayo kwa macho tunamuona kama ni mwanadamu/mtu-kumbe sivyo, bali NI MIILI AMBAYO HAINA ROHO YA MWANADAMU NDANI YAKE! Ilikuwa ni majitu yanayobaka(na siyo malaika toka mbinguni kama wengine wasemavyo), tena yanatafuna watu kama wanyama wafanyavyo, sehemu nyingine katika biblia yaliitwa majitu kama simba(2Sam.23:20; 1Nya.11:22); ni majitu ambayo hayawezi kamwe kuupokea wokovu wala kuwa na hamu ya kuokoka, kwani si binadamu kabisa! Ni majitu yaliyowafundisha hata wanadamu tabia za kuwaza na kukusudia mabaya tu moyoni siku zote, kiasi kwamba hata yakasababisha Mungu ajute kwa nini amemfanya binadamu, na kuamua atamfutilia mbali asiwepo tena juu ya uso wa nchi, na kupunguziwa umri wa kuishi. Ndiyo maana Mungu aliyafuta makabila na mataifa ya majitu hayo kutoka katika uso wa dunia yasiwepo tena kabisa, kwa kupitia gharika ya Nuhu na vita vya wana wa Israeli – waliambiwa wasiyaache majitu hayo kuishi! Swali, ni kuhusu-artificial insemination? test tube baby? Je, Mungu hutia roho ya mwanadamu anayetengenezwa kwa njia hiyo? Au ndiyo kutengeneza Majitu ambayo Mungu ameyakataa?
Mwanzo 6:1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. 3 BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni mnyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. 4 NAO WANEFILI WALIKUWAKO DUNIANI SIKU ZILE; tena,baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana; hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.

•••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••

JE, NI KWELI KWAMBA MALAIKA WALIZAA NA WANADAMU?
Hapana! Biblia haisemi hivyo! Ila ni mawazo na maelezo ya watu kutokana na kuitafsiri vibaya mistari katika kitabu cha Mwanzo 6:1-4.
Hapa haina maana kwamba malaika toka mbinguni walifanya tendo la ndoa(uzinzi) na mabinti za wanadamu, (BIBLIA HAISEMI KAMA MALAIKA NDIO WALIOZINI NA BINTI ZA WANADAMU, ILA INASEMA KWAMBA SIKU ZILE WALIKUWEPO WANEFILI AMBAO NI MAJITU SI WANADAMU WA KAWAIDA); bali ni kutokana na mchanganyiko wa kuoana kwa wanadamu wa uzao wa Sethi(WANA WA MUNGU AMBAO HAWAKUPANDIKIZWA NGUVU YA UZAO WA MAJITU) na uzao wa wanadamu (WANA WA WANADAMU WALIOPANDIKIZWA NGUVU YA UZAO WA MAJITU NDANI YAKE); ndipo “wakazaa nao wana; hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.” (AMBAO KIMAUMBILE WALIFANANA NA WANEFILI lakini siyo wanefili).
Umeandika mengi japo nimesoma juu kwa juu!
But Wana wa mungu ni malaika!
 
Grahnman.
Mkuu
Leta maandiko ya hili hapa chini

[Mkuu mbona hata mimi naelewa hivyo kama ulivyosema yaani Wanefili si Malaika ila walitokana na Malaika walioshuka dunian na kuzaa na wanawake]
 
Mkuu mbona hata mimi naelewa hivyo kama ulivyosema yaani Wanefili si Malaika ila walitokana na Malaika walioshuka dunian na kuzaa na wanawake
wana wa Mungu vs Wana wa Wanadamu!!!!!!
japo nje ya mada. mimi naelewa wote hao ni wanadamu.
watu waliomuasi Mungu - wana wa wanadamu.
Watu waliomtii Mungu - wana wa Mungu.

maana hata hao manefili bibilia inawaita ni Watu.
pia bibilia sioni kama inazungumzia kama kuna uwezekano wa viumbe walioumbwa na Moto (malaika) kufanya mapenzi na wanadamu(viumbe wa udongo) ili wazaliane.
Maana tendo la ndoa liliwekwa kwa ajili ya wanadamu na sio malaika. na Yesu alisema mbinguni hakuna kuzaa wala kuzaliana.

maoni.
 
Mchawi Mkuu. Tusaidie unavyo amini haya huenda tukapata mwanga zaidi.
Kwanza binafsi sifahamu mungu ni Nani?
Najua kuna SUPER NATURAL POWER ambayo Ina control universe
Inshu ya hao majitu Na fallen angel
Na ishu ya Seth Na Cain
Mimi naijua tofaut Na wengi humu!
 
wana wa Mungu vs Wana wa Wanadamu!!!!!!
japo nje ya mada. mimi naelewa wote hao ni wanadamu.
watu waliomuasi Mungu - wana wa wanadamu.
Watu waliomtii Mungu - wana wa Mungu.

maana hata hao manefili bibilia inawaita ni Watu.
pia bibilia sioni kama inazungumzia kama kuna uwezekano wa viumbe walioumbwa na Moto (malaika) kufanya mapenzi na wanadamu(viumbe wa udongo) ili wazaliane.
Maana tendo la ndoa liliwekwa kwa ajili ya wanadamu na sio malaika. na Yesu alisema mbinguni hakuna kuzaa wala kuzaliana.

maoni.
tunaanza kuongea lugha moja sasa.
mchawi
ztto jr
 
wana wa Mungu vs Wana wa Wanadamu!!!!!!
japo nje ya mada. mimi naelewa wote hao ni wanadamu.
watu waliomuasi Mungu - wana wa wanadamu.
Watu waliomtii Mungu - wana wa Mungu.

maana hata hao manefili bibilia inawaita ni Watu.
pia bibilia sioni kama inazungumzia kama kuna uwezekano wa viumbe walioumbwa na Moto (malaika) kufanya mapenzi na wanadamu(viumbe wa udongo) ili wazaliane.
Maana tendo la ndoa liliwekwa kwa ajili ya wanadamu na sio malaika. na Yesu alisema mbinguni hakuna kuzaa wala kuzaliana.

maoni.
Lkn si unakubali uwepo wa Wanefili je wakitokea wapi?
 
Hatujaambiwa walikuwa jinsia gani so huenda kulikuwa na wanefili wa kiume na wakike. Ila uzao wao upo mfano huyu mfalme ogu alikuwa anatawala MAJIJI 60 kwenye himaya ya jamii yake ikimaanisha aliweza kuwa na uzao ingawa hatujaelezwa huyo mke wake alikuwa wa aina gani kma naye ni alikua mnefili ama lah ila kwa kujibu swali lako tuamini tu kuwa kulikuwa na wanawake wanefili pia hivyo walilala nao hao hao

labda walikuwa na mwili mkubwa lakini wana vibamia vilivyowawezesha kulala na wanawake wa kawaida!!!samahani lakini nimekuletea story za vibamia hadi huku
 
Mchawi Mkuu. Tusaidie unavyo amini haya huenda tukapata mwanga zaidi.
Kwanza binafsi sifahamu mungu ni Nani?
Najua kuna SUPER NATURAL POWER ambayo Ina control universe
Inshu ya hao majitu Na fallen angel
Na ishu ya Seth Na Cain
Mimi naijua tofaut Na wengi humu!
Mkuu now sipo sawa kuongelea hilo swala!
 
Jamani haya yanawezekana maana hata toothpick walizokuwa wanatumie enzi hizo ni kubwa sana kwa sasa unaweza kuzifananisha na nguzo ya umeme.
Duh... punguza fix kidogo we mrembo... dah!
 
Hawa wanefili ni matokeo ya malaika kuzaa na binadamu na inasemekana waliangamia na hawapo tena
Kwanini hawa malaika waliozaa na binadamu huwa hawashuki tena duniani na kuja kuzaa na mabinti wengine baada ya gharika hadi mpaka sasa?
Nini kimewazuia

kwahiyo hao malaika wana maumbo makubwa au watoto wakizaliwa ndio wanakuja kuwa na maumbo makubwa???
 
Grahnman.
[Lkn si unakubali uwepo wa Wanefili je wakitokea wapi]

Jibu ni kuwa wanefili walikuwepo kabla ya wanadamu.
 
Wewe mjamaa!
Inshu ni kwamba
Wewe unasema wanefili n product ya Wana wa mungu ambao ni uzao wa Seth
But me nasema hao majitu ni uzao wa malaika waasi mbona history Na vitu vipo wazi
hilo bandiko nimelitoa mahali kuleta mtazamo mpya juu ga wanao sema wana wa Mungu ndio malaika. Nimeomba ushahidi wa wapi ktk biblia unaonesha wana wa Mungu ndio malaika waasi sijapata mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom