Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Ok, hv majini yalitokeaje
Majini yameumbwa toka zamani uko na walikuepo kabla yetu hapa dunian wakiishi na wakaja wakaondolewa na kupelekwa baharini baada yakufanya ufisadi hapa aridhini ndipo mungu mungu alipo amrisha waondolewe huku kisha wakapelekwa baharin. Na katika hao majini alikuepo mmoja wao ambae alikuwa mchamungu sana ndipo mungu aliamua kwa makusudi yake mwenyewe amchukue amueke pamoja na malaika na huyo si mwingine bali ni IBIRIS hapo kabla ya kuasi alikua mwema sana na mchamungu kwelikweli mpk akapewa chance yakuwa pamoja na malaika kisha baada ya muda mungu ndo akamuumba baba yetu adam alipo maliza aliwaamrisha malaika pamoja na huyo ibirisi wampe heshma adam. Malaika walimpa heshma adam ila ibirisi alikataa na kwa kibri chake na kumwambia mwenyezi mungu mimi siwezi kukitukuza kiumbe ambacho umekiumba kwa udongo na mimi umeniumba kwa moto na tena umekiumba me nakiona. Hapo ndo mwenyez mungu akakasirika akamlaani yule na kumwambie atoke katika ufalme wake na kumwambie kwanzia leo umeangamia wewe pamoja na wote watakao kufata ibirisi nae kamjibu kwamba atahakikish anafanya kila njia ili ampoteze adam yeye au kizazi chake ili aongie nao motoni.
Nimechoka kuandika bhana ntaendelea badae
 
Naposema Dunia kwa context ya agano la kale ni mashariki ya kati pekee ndio ilikuwa dunia..... Enzi hizo watu waliishi maeneo ya mesopotamia hadi eridu mpaka misri basi na walikuwa hawazidi hata million 5 dunia nzima!!

Enzi za mfalme ogu afrika ilikuwa inaishia libya na misri tu hivyo hakukuwa bado na matishio huku afrika ingawa najua baadae afrika ilikuja kupata watu mashujaa ila all in all huyu Ogu alikuwa ni MWEUSI sababu anatambuliwa kma muamori ambaye ni jamii ya HAMITES ngozi nyeusi kabisa walioishi canaan/palestina-israel ya sasa takriban miaka 6000 iliopita hivyo ni ''mwenzetu'' huyo!!

Hapa naeza pingana na wew kidogo,sidhani kama ni kweli dunia iliishia misri ila tuseme tu maandiko hayakuwa na upana wa kueleza kuihusu Africa kiujumla maana kama wangeliweka uzao wetu lazima tungewahoji vipi sisi mungu alikuwa na lipi juu yetu?

Kama na sisi tungeliandikwa kwenye vitabu vitakatifu wasongelikuwa na uhalali wa kutuaminisha ustarabu ulianzia kwao wakati historia chache zinazopingwa zinaonesha uafrika katika ustarabu wa kwanza!

Ngoja nikwambie chanzo kikuu cha kukizika kitabu cha Enok ni kwa sababu ya kueleza kimapana juu ya dunia na uhalali wa mtu wa kwanza kutokea ukanda wa jangwa la sahara lakini pia kilizungumzia majengo ya pyramid ambayo wanasema hawajui alieyajenga lakini inaelezwa kuwa ni watu wa kabila la Dagon linalopatikana kaskazini ya Niger na nchi ya...(nimesahau) sasa imajini kama pyramid hawajui zilijengwa karne gani na nani watawezaje kukuweka wazi kuhusu uzao wa akina Ogu ambao inasemekana walitokea Afrika au America ya kaskazini ambapo hadi leo kuna baadhi ya michoro na sanamu kubwa,je ziliwekwa na nani ikiwa lile bara halijawahi kukaliwa huko nyuma?na kikubwa zaidi sanamu ni za watu weusi?

So hapo kusema dunia ilianzia misri nakataa sema uzao wetu unafichwa kabisa,haya tuseme sisi makabila mengine ni wakuja tu vipi kuhusu wahdzabe, na wasandawe ambao kimsingi ndio wamiliki wa ukanda huu sema waliponzwa na kuhamahama, na hata baadhi ya vitabu vinasema historia za binadamu wa kwanza kuwa sokwe vinatokana na mwonekano wa jamii hii ya wahadzabe! Je wao hawakuwa na uzao uliotawala? Labda baadhi ya jamii hazikusemwa kwa kuwa hazikuwa zenye uchu wa madaraka hivyo kukimbia Vita basi zinawekwa pembeni

Lakini pia kuna kitabu flan cha nabii wa kike nacho kiliondolewa sababu zikiwa sawa na za kuondolewa kwa kitabu cha Enok huku wakisema vinaushetani

Mzee Afrika ilikuwepo tena enzi na enzi,na ndio maana hata fuvu la mtu wa kale lipo Afrika sema yule Dr nae alipotezewa na fuvu lake hivyo tunaishia tu kusema fuvu la mtu wa kale lipo Afrika basi bila kuhoji zaidi na zaidi

Kuna kitabu flani niliwahi kukiiba kwa mama maana hakutaka kukigawa na hata ufanyeje hakupi,kina mengi sana sema sijui kipo wapi hivi sasa nimekitafuta hapa harakaharaka sijakiona ila hakijapotea kipo nikikipata nitakikopi tujifunze wote

Ila kwa kuwa ni kibiblia zaidi basi tuamini Afrika ilikuwa imeanzia misri.

Jiulizie kwa nini unatajwa mto Nail afu bustani ya Eden haikuandikwa ipo wapi!!
 
Unamaanisha nini kusema hivi?

Louis Seymour Bazett Leakey alituambia kua Mtu wa Zamani/Kale zaidi aliishi Tanzania, na aliigundua hii kitu baada ya kupata Fuvu la Binadamu huyo. Kama unaelewa issue za Zinjanthropus
Baada ya gharika ndio naongelea?? Watu wengi waliishi mashariki ya kati ndio maana Afrika haikusimuliwa sana mpka pale ambapo makabila ya kiafrika yakaendelea kukua na kutapakaa afrika nzima ila hapo kabla ilikuwa nchi za afrika mwisho msiri na libya!!!
 
Kwanza kuna kitu hakileti ukweli katika Biblia maana hapa katika maandiko ya mwanzo kuna mkanganyiko inaonyesha WANEFILI WALIKUWEPO KABLA YA BINADAMU

1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
Mwanzo 6 :1

2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
Mwanzo 6 :2

4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.
Mwanzo 6 :4
 
Mkuu mtu akijiuliza kma seth na cain ndio wana wa Mungu na wana wa adamu je vipi kuhusu watoto wengine wa Adam ambapo hta Cain mwenyewe alienda kuishi kwao huko Nod!! Je wanaangukia upande upi???

Biblia ina mafumbo mengi sana mkuu embu soma huu mstari

Walawi 20:30
11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao

Nadharia hii kupitia definition hii ya kitabu cha walawi inasema Ham alilala na mama yake ndio maana mtoto aliyezaliwa yaani Canaan alilaaniwa na sio Ham..... Na nadharia hii naweza ikubali sababu hata mtoto aliyezaliwa yaani canaan alikua wa ajabu ajabu tu hta kizazi chake walikuwa majitu makubwa ya kutisha hii inaweza tokana na uzao wa ajabu kati ya mwana na mama!!!

Nadharia ya pili inasema alimlaani canaan sababu ndio unabii unaonyesha alikuja kupigwa na waisraeli na kuondolewa kabisa hapo mashariki ya kati hivyo alimtaja canaan sababu ndio atatimiza unabii wa laana ya Ham.... As u know kwenye biblia mtu akitoa laana anamaanisha inaenda hadi kizazi cha nne

Nadharia ya tatu inasema canaan ndio alimuona babu yake yaani Nuhu yupo uchi na akaenda mshtua baba yake yaani ham aone ila Ham akaishia kucheka tu so hasira za Nuhu zikaishia kwa canaan sababu ndio alikua wakwanza kumuona!!

3. Kuhusu wake wa watoto wa Nuhu haielezwi kwenye biblia ila nje ya biblia tunaambiwa ni uzao wa methuselah aliotokana na seth nyingine inadai mke wa Ham alikuwa kitukuu cha cain aliyeitwa neitamuk..... Wengine wanasema walikuwa watoto wa methuselah ila damu ya unefili iliingia kupitia mimba ambayo mke wa Ham alipewa na shamael ambaye ni malaika aliyeasi!!!! Ila hoja hii ina mashiko sababu watoto karibu wote wa Ham walikuwa majitu makubwa kuliko upande wa shem na japhet
But tunaambiwa kuwa sisi weusi ni uzao wa HAM....so it means tuko na shida??
 
mkuu assumptions hizo inabidi na Uhusika wa Mungu kwenye hilo zoezi hilo uwe neglected.
pia baadhi ya commentary zinasema kutumika kwa neno la kiebrania linaloendana na wanefili wa zamani sio lazima awe nefili aliyetoroka kichapo cha mafuriko, bali ni lugha kuwakilisha ufanano wa hilo jitu na majitu ya kale. maana ukiliita hivyo kwa waebrania wataelewa zaidi.

lkn kabla haijatajwa futi 15, fungu la nyuma linasema milima yote ilifunikwa (kufunikwa milima yote, assumption ilikuwa ni grobal flood hata everest yenye zaidi ya futi 20,000, yawezekana hiyo 15 foot ni kwa vimilima ambavyo vilikuwa karibu, ila lile fungu la nyuma lilipozungumzia milima yote sidhani kama huyo jamaa angeweza kusurvive).

Ikiwa ni futi 15 flat worldwide nadhani kuna sehemu zitakuwa hazijafunikwa na maji kama mlima kilimanjaro, kitu ambacho kitakanusha sentesi milima yote ilifunikwa.

Pia nawaza kwa assumption ya uwezekano wa kutoroka kwa huyo jamaa kutokana na umbo lake kuwa kubwa kuliko kimo chake.
mambo kadhaa yataibuka.
1: Mungu ataonekana ni unintelligent being kutoa adhabu ambayo kuimbe wake anaweza kuikwepa. kitu ambacho hakiungani na sifa za Mungu.
2:Mikono 15 ya watu wa enzi za nuhu ni tofauti na mikono ya kipindi hiki. kumbuka kabla ya mafuriko watu walikuwa ni wakubwa sana, na wenda ilichukuliwa reference ya mikono ya hayohayo manefili maana lengo la mafuriko pamoja na yote hao ndio walikuwa walengwa wakuu.
3:Gharika ilidumu juu ya nchi zaidi ya siku arobaini. huyo OG alitakiwa asimame kwenye maji yenye nguvu bila kula siku arobaini. Kumbuka kwao mvua ilkuwa ni mshtukizo japo nuhu alihubiri na kutoa tahadhari miaka 120. hivyo huyo jamaa hakujiandaa kisaikolijia, pia kusema alikula Mizoga kwa wigo wa bibilia watu walianza kula nyama baada ya gharika.
sidhani kama angepata stamina ya kusimama siku zote hizo. Kumbuka nguvu ya maji pia mkuu na huyo kiumbe hajawahi kukutana na hayo mazingira.

4:Mvua ilinyesha Siku 40, maji yakadumu siku 150 siku karibu 200 huyo mdau alikuwa yuko majini. na Mungu akimuangalia tu. Zaidi ya nusu mwaka. mkuu biologically kwa non-aquatic being kuwa hai majini hata kama ni maji ya kiuno?

najaribu kufikiri na kuvaa viatu vya OG napata shida inabidi assumptions nyingi sana ziongezeke, na constants nyingi sana ziondolewe na uwezo wa Mungu na nia yake udogoshwe kabisa awe kama nyampala flani tu ambaye alikiwa anaadhibu vijana wake na baadhi wakamchenga.

nawaza mkuu.
assumption kuu. Yale maji hayakuwa tulivu kama ya kwenye swimming pool hadi mdau apate kusimama raha mstarehe miezi sita, bali yalikuwa ni zaidi ya tsunami kwa maana ya nguvu na vurugu zake.
Mkuu kwanni tusiassume kuwa Mungu alimuacha kwa maksudi yake??? Kama ambavyo aliangusha ukuta wa yeriko ila alimuacha yule kahaba!!! Kama ambavyo alimuamuru Joshua achinje warefai wote ila mwisho wa siku aliwaacha wale wa gaza na hata suleiman alipojaribu kuwaua Mungu alimuadhibu...... Je kwanni tusiangalie possibilities za namna hiyo??? Kwamba Jamaa alipona sio kwa nguvu zake binafsi ila kwa Mkono wa Mungu!!!

Kingine lazima tujue kuwa hawakupona watu nane tu mfano wakati wa gharika shem alikuwa na miaka 100 na watoto kibao hivyo safina iliweza kubeba watu zaidi ya 70 ingawa tunaambiwa ni 8 ssa kwa mtindo huo kwanni basi tuzichukue statistics za biblia na namba yake kma ni final bila kuangalia possibilities zingine za uwezekano kati ya watu 70 basi Og alikuwa mmoja wao?
 
But tunaambiwa kuwa sisi weusi ni uzao wa HAM....so it means tuko na shida??
Hapana mke wa Ham ndio alikua mweusi Ham hakuwa mweusi alikuwa ni mweupe...... Unless useme tumepata shida sababu ya mke wa ham inayesemakana alikuwa uzao wa Cain labda ndio tutembee na laana ya Cain ila sio eti Ham alikuwa mweusi so ana laana ya Nuhu hapana kwanza alilaaniwa Canaan sio Ham na canaan kizazi chake kilishafutwa toka agano la kale so laana imeishia pale afterall Yesu alishakuja na akasema amefuta laana ya dunia kivp sisi laana ya waafrika iendelee??? Hizo ni kelele za wabaguzi tu ndio maana hta manabii wengi wa agano la kale walikuwa na wake weusi hivyo kma ni laana ilitembea pia kwenye koo zao???
 
Hapa naeza pingana na wew kidogo,sidhani kama ni kweli dunia iliishia misri ila tuseme tu maandiko hayakuwa na upana wa kueleza kuihusu Africa kiujumla maana kama wangeliweka uzao wetu lazima tungewahoji vipi sisi mungu alikuwa na lipi juu yetu?

Kama na sisi tungeliandikwa kwenye vitabu vitakatifu wasongelikuwa na uhalali wa kutuaminisha ustarabu ulianzia kwao wakati historia chache zinazopingwa zinaonesha uafrika katika ustarabu wa kwanza!

Ngoja nikwambie chanzo kikuu cha kukizika kitabu cha Enok ni kwa sababu ya kueleza kimapana juu ya dunia na uhalali wa mtu wa kwanza kutokea ukanda wa jangwa la sahara lakini pia kilizungumzia majengo ya pyramid ambayo wanasema hawajui alieyajenga lakini inaelezwa kuwa ni watu wa kabila la Dagon linalopatikana kaskazini ya Niger na nchi ya...(nimesahau) sasa imajini kama pyramid hawajui zilijengwa karne gani na nani watawezaje kukuweka wazi kuhusu uzao wa akina Ogu ambao inasemekana walitokea Afrika au America ya kaskazini ambapo hadi leo kuna baadhi ya michoro na sanamu kubwa,je ziliwekwa na nani ikiwa lile bara halijawahi kukaliwa huko nyuma?na kikubwa zaidi sanamu ni za watu weusi?

So hapo kusema dunia ilianzia misri nakataa sema uzao wetu unafichwa kabisa,haya tuseme sisi makabila mengine ni wakuja tu vipi kuhusu wahdzabe, na wasandawe ambao kimsingi ndio wamiliki wa ukanda huu sema waliponzwa na kuhamahama, na hata baadhi ya vitabu vinasema historia za binadamu wa kwanza kuwa sokwe vinatokana na mwonekano wa jamii hii ya wahadzabe! Je wao hawakuwa na uzao uliotawala? Labda baadhi ya jamii hazikusemwa kwa kuwa hazikuwa zenye uchu wa madaraka hivyo kukimbia Vita basi zinawekwa pembeni

Lakini pia kuna kitabu flan cha nabii wa kike nacho kiliondolewa sababu zikiwa sawa na za kuondolewa kwa kitabu cha Enok huku wakisema vinaushetani

Mzee Afrika ilikuwepo tena enzi na enzi,na ndio maana hata fuvu la mtu wa kale lipo Afrika sema yule Dr nae alipotezewa na fuvu lake hivyo tunaishia tu kusema fuvu la mtu wa kale lipo Afrika basi bila kuhoji zaidi na zaidi

Kuna kitabu flani niliwahi kukiiba kwa mama maana hakutaka kukigawa na hata ufanyeje hakupi,kina mengi sana sema sijui kipo wapi hivi sasa nimekitafuta hapa harakaharaka sijakiona ila hakijapotea kipo nikikipata nitakikopi tujifunze wote

Ila kwa kuwa ni kibiblia zaidi basi tuamini Afrika ilikuwa imeanzia misri.

Jiulizie kwa nini unatajwa mto Nail afu bustani ya Eden haikuandikwa ipo wapi!!
Mkuu nmekuelewa hoja yako na nikiri kweli kwa kiasi kikubwa historia ya afrika inapotoshwa na ndio maana mwanzoni wa hoja yangu nimesema KWA CONTEXT YA AGANO LA KALE...... Sababu kibiblia tokea dunia iumbwe mpaka gharika tunaona population kubwa ikiwa concentrated mashariki ya kati enzi hizo bado dunia ni bara moja tu hakuna mabara na hapo ndio ilikuwa katikati ya dunia na ndio maana enzi hizo ukicontrol middle east inahesabika umetawala dunia sababu hiyo hata Nimrod aliitwa mtawala wa dunia simply alitawala sumeria iliokuwa ndio utawala mkubwa mashariki ya kati ingawa kweli nakubali lazima afrika kulikuwa na watu ila kibiblia haitaji inaishia misri kwa sana

Baada ya gharika ndio tunaona mabara yanagawanyika na watu wanasambaa dunia nzima na hata afrika tunaanza kutajwa humo watu kma nimrod na canaan wanatajwa humo kma watu waliokuwa na nguvu sana na ushawishi katika ulimwengu wa kale so kwa muktadha huu gharika lingepiga mashariki ya kati wakati wa Nuhu ina maana wangeweza kusummarise kuwa gharika limepiga dunia nzima sababu ndio limit ya makazi ya watu !!!

All in all waafrika tujilaumu kwa kutokuandika na kutunza historia zetu mwisho wa siku wazungu ndio wanatuandkiia historia yetu iliopotoshwa..... Mpaka Yesu wanaonyesha ni mzungu ilihali alizaliwa kwenye lineage ya mke wa suleiman aliyekuwa mweusi tii anayezungumziwa kwenye wimbo ulio bora !! Funny
 
Hapa naeza pingana na wew kidogo,sidhani kama ni kweli dunia iliishia misri ila tuseme tu maandiko hayakuwa na upana wa kueleza kuihusu Africa kiujumla maana kama wangeliweka uzao wetu lazima tungewahoji vipi sisi mungu alikuwa na lipi juu yetu?

Kama na sisi tungeliandikwa kwenye vitabu vitakatifu wasongelikuwa na uhalali wa kutuaminisha ustarabu ulianzia kwao wakati historia chache zinazopingwa zinaonesha uafrika katika ustarabu wa kwanza!

Ngoja nikwambie chanzo kikuu cha kukizika kitabu cha Enok ni kwa sababu ya kueleza kimapana juu ya dunia na uhalali wa mtu wa kwanza kutokea ukanda wa jangwa la sahara lakini pia kilizungumzia majengo ya pyramid ambayo wanasema hawajui alieyajenga lakini inaelezwa kuwa ni watu wa kabila la Dagon linalopatikana kaskazini ya Niger na nchi ya...(nimesahau) sasa imajini kama pyramid hawajui zilijengwa karne gani na nani watawezaje kukuweka wazi kuhusu uzao wa akina Ogu ambao inasemekana walitokea Afrika au America ya kaskazini ambapo hadi leo kuna baadhi ya michoro na sanamu kubwa,je ziliwekwa na nani ikiwa lile bara halijawahi kukaliwa huko nyuma?na kikubwa zaidi sanamu ni za watu weusi?

So hapo kusema dunia ilianzia misri nakataa sema uzao wetu unafichwa kabisa,haya tuseme sisi makabila mengine ni wakuja tu vipi kuhusu wahdzabe, na wasandawe ambao kimsingi ndio wamiliki wa ukanda huu sema waliponzwa na kuhamahama, na hata baadhi ya vitabu vinasema historia za binadamu wa kwanza kuwa sokwe vinatokana na mwonekano wa jamii hii ya wahadzabe! Je wao hawakuwa na uzao uliotawala? Labda baadhi ya jamii hazikusemwa kwa kuwa hazikuwa zenye uchu wa madaraka hivyo kukimbia Vita basi zinawekwa pembeni

Lakini pia kuna kitabu flan cha nabii wa kike nacho kiliondolewa sababu zikiwa sawa na za kuondolewa kwa kitabu cha Enok huku wakisema vinaushetani

Mzee Afrika ilikuwepo tena enzi na enzi,na ndio maana hata fuvu la mtu wa kale lipo Afrika sema yule Dr nae alipotezewa na fuvu lake hivyo tunaishia tu kusema fuvu la mtu wa kale lipo Afrika basi bila kuhoji zaidi na zaidi

Kuna kitabu flani niliwahi kukiiba kwa mama maana hakutaka kukigawa na hata ufanyeje hakupi,kina mengi sana sema sijui kipo wapi hivi sasa nimekitafuta hapa harakaharaka sijakiona ila hakijapotea kipo nikikipata nitakikopi tujifunze wote

Ila kwa kuwa ni kibiblia zaidi basi tuamini Afrika ilikuwa imeanzia misri.

Jiulizie kwa nini unatajwa mto Nail afu bustani ya Eden haikuandikwa ipo wapi!!
Aisee hongera kwa uchambuzi yakinifu.

Huwa najiuliza sana wanaposema fuvu la mtu wa kwanza lilipatikana Africa lakini cha kushangaza wanasahau hilo
 
Majini yameumbwa toka zamani uko na walikuepo kabla yetu hapa dunian wakiishi na wakaja wakaondolewa na kupelekwa baharini baada yakufanya ufisadi hapa aridhini ndipo mungu mungu alipo amrisha waondolewe huku kisha wakapelekwa baharin. Na katika hao majini alikuepo mmoja wao ambae alikuwa mchamungu sana ndipo mungu aliamua kwa makusudi yake mwenyewe amchukue amueke pamoja na malaika na huyo si mwingine bali ni IBIRIS hapo kabla ya kuasi alikua mwema sana na mchamungu kwelikweli mpk akapewa chance yakuwa pamoja na malaika kisha baada ya muda mungu ndo akamuumba baba yetu adam alipo maliza aliwaamrisha malaika pamoja na huyo ibirisi wampe heshma adam. Malaika walimpa heshma adam ila ibirisi alikataa na kwa kibri chake na kumwambia mwenyezi mungu mimi siwezi kukitukuza kiumbe ambacho umekiumba kwa udongo na mimi umeniumba kwa moto na tena umekiumba me nakiona. Hapo ndo mwenyez mungu akakasirika akamlaani yule na kumwambie atoke katika ufalme wake na kumwambie kwanzia leo umeangamia wewe pamoja na wote watakao kufata ibirisi nae kamjibu kwamba atahakikish anafanya kila njia ili ampoteze adam yeye au kizazi chake ili aongie nao motoni.
Nimechoka kuandika bhana ntaendelea badae
Mkuu kitabu gani umesoma kupata hicho unachokiandika nami nikitafute ili twende sambamba coz nahic km unanivuruga hivi.

Eti Mungu alimwamurisha shetani amuhesimu Adamu? Fafanua

Na ni ufisadi gani waliufanya hao majini mpk kupewa adhabu ya kuishi majini si kwingineko

Mwanzoni ulisema majini na binadamu ni ndugu mbona hapo tyr unaonekana uadui?

Na je unaweza kuniambia kiuhalisia muonekano wa shetani kiumbe alieumbwa kwa moto kwa mujibu maelezo yako?
 
Hii siyo nadharia ya kwenye Biblia, hakuna sehemu kwenye Biblia ambapo haya yameandikwa. Haya ni maandishi ya baadhi ya Wayahudi na Waarabu.

Alichosena mkuu zitto junior hapa ni nadharia "theory" ambayo kazi zetu wasomaji ni kupima, kuchambua na kutafuta ushahidi ili tupate ukweli. Kubwa ziaidi hii ni nadharia ya kidini na siyo ya kisayansi, hivyo tutakuwa tunakosea sana kama tunazipinga kwa kutumia sayansi.

Yote tisa kama unashangaa hili dogo, utaelezaje lile la Nabii Joshua kugandisha jua siku nzima ili Wahebrania wapigane vita. Au lile la Yona kukaa tumboni mwa nyangumi kwa siku tatu bila kufa...???

Je huyu aliekufa na kujifufua mwenyewe na kupaa utasemaje
Zen rekebisha futa kauli Joshua hakusimamiasha jua alisimamisha dunia isizunguke jua
 
Katika vitu ambavyo huwa nashangaa ni kumkuta mtu mzima akiamini hizi story za bible na vitabu vyengine vya dini..! [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Katika vitu ambavyo huwa nashangaa ni kumkuta mtu mzima akiamini hizi story za bible na vitabu vyengine vya dini..! [emoji1][emoji1][emoji1]
Wewe unaamini zipi ? Au bado ni mtoto?
 
2. Nadharia ya pili inasema kuwa alikuwa na ukaribu sana na Nuhu hivyo alipewa kazi ya kuiangalia safina kwa nje kuhakikisha haigongi mwamba au mawe makubwa ambayo yangeweza kuipasua safina na hiyo ndio ikawa pona yake!!! Inadaiwa alijishikiza pembeni ya safina ya nuhu ivo hakubebwa na maji ya gharika. Nadharia hii ina mashiko sababu hata baada ya gharika tunaona safina hii ilitua palepale ilipokuwa kabla ya gharika yaani haikuenda mbali kabisa kitu ambacho hakiwezekana kama nguvu ya mafuriko ikizingatiwa lazima boti ingesukumwa maili kadhaa mbele. Kingine kwa akili ya kawaida tu dunia nzima izame alafu ww pekee uwe kwenye boti hivi wanaokufa watakuacha kweli?? Lazima wangetaka kuivamia boti waingia na ukizingatia yalikuwa majitu marefu yangeweza kuipasua pasua ila kwa uwepo wa OG walishindwa maana wangekutana na kipigo cha mbwa mwizi!!
Hii nadharia umesema ndiyo yenye mashiko,sijaelewa ina mashiko kwa nani,kama ni kwako ni sawa...

Kwangu mimi nadharia hii naiona haina mashiko kabisa mkuu.Nasema hivi kwasababu zifuatazo..

1;Suala la yeye "kupewa kazi ya kuiangalia safina ili isigngane na mawe"ni nadharia ya kuchekesha sana maana unataka kumfanya Mungu kama asiyejiweza na kuelewa alilokuwa anafanya.Kwanza ni mawe gani hayo? Maana maji yalifunika milima yote,kuna jiwe kubwa zaidi ya mlima Kilimanjaro kwa mfano?Lakini unapaswa tu uelewe kwamba suala zima la gharika ni suala lilisimamiwa na Mungu,sijuwi kama unaelewa ni nini maana ya Mungu kwa ujumla wake.....

2;Unadaio kuwa "kwa akili ya kawaida dunia nzima izame halafu wewe pekee uwe kwenye boti,hivi waliokufa watakuacha kweli?",yaani hiki nacho ni kichekesho kingine mkuu. Kwanza safina siyo boti,pili safina ilijengwa kwa namna ya ajabu na kwa maelekezo ya Mungu mwenyewe unadhani unaweza ivunja? Kwa kutumia nini? Halafu ukiwa kwenye maji huku ukipigania uhai wako? Are you serious?

Mungu aliwajuwa hao majitu vizuri sana na kwakuwa yeye aliisimamia "shoo"haya unayofikiria ni kama kitu cha kuchekesha sana kwake...

Hii nadharia yako haina mashiko kabisa hata kiduchu....
3. Nadharia ya tatu inasema kipindi cha gharika Ogu alikuwa bado hajazaliwa ila mimba yake ilikuwa imeshatungwa na mama yake aliekuwa mke wa Ham hivyo ham asingeweza kumuacha nyuma ingawa inadaiwa mimba hiyo haikuwa ya Ham bali ya Malaika aliyeitwa shamael!! Hivyo damu ya wanefili ikaweza kuvuka gharika kwa staili hiyo kupitia mtoto aliyezaliwa yaani mflame ogu ama canaan ambae watoto wake kwenye biblia wanatajwa kma majitu makubwa ambayo yaliona wanadamu kma panzi!!! Mfano amori aruba anak hivi gilgal amoni yebusi n.k
Hii nadharia inajaribu kuelezea namna kizazi cha Wanefili kilivyokuja kupatikana baadaye,baada ya gharika.Inawezekana au isiwezekane ukizingatia sababu kuu ya gharika ni hao hao Wanefili na sidhani kama Mungu angeruhusu ikawa hivi japokuwa inaweza ikawezekana pia...
4. Nadharia ya tatu inasema alienda milimani hivyo gharika haikumkuta. Biblia iko wazi kuwa maji yalifunika MILIMA mirefu kwa futi 15 kwenda juu ina maana kma hyu OG alikuwa na futi zaidi ya 13 pengine 28 kama inavyoelezwa kwenye biblia ina maana kama alipanda milima mrefu zaidi basi hakuweza kumalizwa na gharika!! Simple logic
Hii nadhara nayo haifai kabisa.Hii nadharia inataka kumfanya Mungu asiwe Mungu kabisa maana kama tu mtu anaweza kupanda kwenye mlima halafu Mungu atake kumuua na ishindikane kwasababu kapanda kwenye mlima huyo siyo Mungu ni kitu kingine kabisa...
Kumbukumbu la torati 3:11
11 (Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho je! Hakiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni mikono kenda, na upana wake mikono minne, kwa mfano wa mkono wa mtu).

hapa biblia inasema OG NI MREFAI ALIYESALIA tafsiri ya kiingereza inasema LAST OF THE REPHAIMS ikimaanisha ni mnefili pekee aliyesalia baada ya gharika!!!!
Inawezekana lakini swali kubwa ni namna ilivyowezekana....
Hii inaelezwa ndio ilikuwa kasri au jumba la ibada la mfalme ogu na mpaka leo masalia yapo huko golan heights, syria (linakaliwa kimabavu na israel).... Mawe yaliyobaki kwa sasa ni zaidi ya 40,000 yamepangwa hadi futi 15 kwenda juu je kuna mtu wa miaka ile angeweza kupanga mawe mazito kwa urefu wa zaidi ya futi 50 kwa wakati huo kama hakua JITU la mfano wa OGU.
Wanefili wa kabla ya gharika walifikia futi 30 hivyo huyu OGu unayemsema hapa sijaona uajabu wake.Ninachokielewa ni kwamba Wanefili wa baada ya gharika walikuwa na urefu wa futi 10 hadi 18 hivyo walikuwa wadogo kiumbo kuliko wale wa kipindi kile cha kabla ya gharika....

Majengo ya kustaajabisha hayapatikani mashariki ya kati pekee mkuu,yapo dunia nzima kuanzia Puma Punku kule Bolivia hadi Urusi mpaka kwenye kisiwa cha Sardinia kule Italy ambapo baadhi ya watafiti wanasema kwamba inawezekana ilikuwa ni moja ya ground Zero ya Wanefili wa kabla yagharika maana walishafukua mabaki makubwa sana ya hawa Wanefili.Moja ya fuvu lililowashangaza ni lile ambalo waliweza kuingiza kwenye eye socket ylile fuvu,ule upanga refu wenye makali kila upande,upanga maarufu wa vitani na ulizama wote na ulipogota kisogoni sehemu pekee iliyobakia nje ni ile sehemu ya kushikia tu...

Unaweza tu kufikiria lilikuwa ni fuvu kubwa kwa kiwango gani...

Mabaki ya majitu haya yenye urefu wa zaidi ya futi 25 yamefukuliwa maeneo mengi sana America ya kusini,kaskazini,Africa,Ulaya na Asia hivyo huyo unayemsema hakuwa peke yake labda baada ya gharika kama ulivyoelezea hapo juu kwasababu baada ya gharika Wanefili walikuwa wadogo kiumbo...
 
Back
Top Bottom