2. Nadharia ya pili inasema kuwa alikuwa na ukaribu sana na Nuhu hivyo alipewa kazi ya kuiangalia safina kwa nje kuhakikisha haigongi mwamba au mawe makubwa ambayo yangeweza kuipasua safina na hiyo ndio ikawa pona yake!!! Inadaiwa alijishikiza pembeni ya safina ya nuhu ivo hakubebwa na maji ya gharika. Nadharia hii ina mashiko sababu hata baada ya gharika tunaona safina hii ilitua palepale ilipokuwa kabla ya gharika yaani haikuenda mbali kabisa kitu ambacho hakiwezekana kama nguvu ya mafuriko ikizingatiwa lazima boti ingesukumwa maili kadhaa mbele. Kingine kwa akili ya kawaida tu dunia nzima izame alafu ww pekee uwe kwenye boti hivi wanaokufa watakuacha kweli?? Lazima wangetaka kuivamia boti waingia na ukizingatia yalikuwa majitu marefu yangeweza kuipasua pasua ila kwa uwepo wa OG walishindwa maana wangekutana na kipigo cha mbwa mwizi!!
Hii nadharia umesema ndiyo yenye mashiko,sijaelewa ina mashiko kwa nani,kama ni kwako ni sawa...
Kwangu mimi nadharia hii naiona haina mashiko kabisa mkuu.Nasema hivi kwasababu zifuatazo..
1;Suala la yeye "kupewa kazi ya kuiangalia safina ili isigngane na mawe"ni nadharia ya kuchekesha sana maana unataka kumfanya Mungu kama asiyejiweza na kuelewa alilokuwa anafanya.Kwanza ni mawe gani hayo? Maana maji yalifunika milima yote,kuna jiwe kubwa zaidi ya mlima Kilimanjaro kwa mfano?Lakini unapaswa tu uelewe kwamba suala zima la gharika ni suala lilisimamiwa na Mungu,sijuwi kama unaelewa ni nini maana ya Mungu kwa ujumla wake.....
2;Unadaio kuwa "kwa akili ya kawaida dunia nzima izame halafu wewe pekee uwe kwenye boti,hivi waliokufa watakuacha kweli?",yaani hiki nacho ni kichekesho kingine mkuu. Kwanza safina siyo boti,pili safina ilijengwa kwa namna ya ajabu na kwa maelekezo ya Mungu mwenyewe unadhani unaweza ivunja? Kwa kutumia nini? Halafu ukiwa kwenye maji huku ukipigania uhai wako? Are you serious?
Mungu aliwajuwa hao majitu vizuri sana na kwakuwa yeye aliisimamia "shoo"haya unayofikiria ni kama kitu cha kuchekesha sana kwake...
Hii nadharia yako haina mashiko kabisa hata kiduchu....
3. Nadharia ya tatu inasema kipindi cha gharika Ogu alikuwa bado hajazaliwa ila mimba yake ilikuwa imeshatungwa na mama yake aliekuwa mke wa Ham hivyo ham asingeweza kumuacha nyuma ingawa inadaiwa mimba hiyo haikuwa ya Ham bali ya Malaika aliyeitwa shamael!! Hivyo damu ya wanefili ikaweza kuvuka gharika kwa staili hiyo kupitia mtoto aliyezaliwa yaani mflame ogu ama canaan ambae watoto wake kwenye biblia wanatajwa kma majitu makubwa ambayo yaliona wanadamu kma panzi!!! Mfano amori aruba anak hivi gilgal amoni yebusi n.k
Hii nadharia inajaribu kuelezea namna kizazi cha Wanefili kilivyokuja kupatikana baadaye,baada ya gharika.Inawezekana au isiwezekane ukizingatia sababu kuu ya gharika ni hao hao Wanefili na sidhani kama Mungu angeruhusu ikawa hivi japokuwa inaweza ikawezekana pia...
4. Nadharia ya tatu inasema alienda milimani hivyo gharika haikumkuta. Biblia iko wazi kuwa maji yalifunika MILIMA mirefu kwa futi 15 kwenda juu ina maana kma hyu OG alikuwa na futi zaidi ya 13 pengine 28 kama inavyoelezwa kwenye biblia ina maana kama alipanda milima mrefu zaidi basi hakuweza kumalizwa na gharika!! Simple logic
Hii nadhara nayo haifai kabisa.Hii nadharia inataka kumfanya Mungu asiwe Mungu kabisa maana kama tu mtu anaweza kupanda kwenye mlima halafu Mungu atake kumuua na ishindikane kwasababu kapanda kwenye mlima huyo siyo Mungu ni kitu kingine kabisa...
Kumbukumbu la torati 3:11
11 (Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho je! Hakiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni mikono kenda, na upana wake mikono minne, kwa mfano wa mkono wa mtu).
hapa biblia inasema OG NI MREFAI ALIYESALIA tafsiri ya kiingereza inasema LAST OF THE REPHAIMS ikimaanisha ni mnefili pekee aliyesalia baada ya gharika!!!!
Inawezekana lakini swali kubwa ni namna ilivyowezekana....
Hii inaelezwa ndio ilikuwa kasri au jumba la ibada la mfalme ogu na mpaka leo masalia yapo huko golan heights, syria (linakaliwa kimabavu na israel).... Mawe yaliyobaki kwa sasa ni zaidi ya 40,000 yamepangwa hadi futi 15 kwenda juu je kuna mtu wa miaka ile angeweza kupanga mawe mazito kwa urefu wa zaidi ya futi 50 kwa wakati huo kama hakua JITU la mfano wa OGU.
Wanefili wa kabla ya gharika walifikia futi 30 hivyo huyu OGu unayemsema hapa sijaona uajabu wake.Ninachokielewa ni kwamba Wanefili wa baada ya gharika walikuwa na urefu wa futi 10 hadi 18 hivyo walikuwa wadogo kiumbo kuliko wale wa kipindi kile cha kabla ya gharika....
Majengo ya kustaajabisha hayapatikani mashariki ya kati pekee mkuu,yapo dunia nzima kuanzia Puma Punku kule Bolivia hadi Urusi mpaka kwenye kisiwa cha Sardinia kule Italy ambapo baadhi ya watafiti wanasema kwamba inawezekana ilikuwa ni moja ya ground Zero ya Wanefili wa kabla yagharika maana walishafukua mabaki makubwa sana ya hawa Wanefili.Moja ya fuvu lililowashangaza ni lile ambalo waliweza kuingiza kwenye eye socket ylile fuvu,ule upanga refu wenye makali kila upande,upanga maarufu wa vitani na ulizama wote na ulipogota kisogoni sehemu pekee iliyobakia nje ni ile sehemu ya kushikia tu...
Unaweza tu kufikiria lilikuwa ni fuvu kubwa kwa kiwango gani...
Mabaki ya majitu haya yenye urefu wa zaidi ya futi 25 yamefukuliwa maeneo mengi sana America ya kusini,kaskazini,Africa,Ulaya na Asia hivyo huyo unayemsema hakuwa peke yake labda baada ya gharika kama ulivyoelezea hapo juu kwasababu baada ya gharika Wanefili walikuwa wadogo kiumbo...