Mfalme wa Jordan kaenda white house kamuunga mkono Trump kuwahamisha wapalestina, Misri na nchi nyingine kukutana Saudi Arabia kusuka mpango kazi

Mfalme wa Jordan kaenda white house kamuunga mkono Trump kuwahamisha wapalestina, Misri na nchi nyingine kukutana Saudi Arabia kusuka mpango kazi

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Mfalme Abdullah wa Jordan na Mwanawe Wamtembelea Trump Ikulu

Mfalme Abdullah wa Jordan na mwanawe wametembelea Ikulu ya White House kwa mazungumzo na Rais wa Marekani, Donald Trump. Mkutano huo uliangazia juhudi zinazoendelea za kubadilisha mwelekeo wa Mashariki ya Kati, hasa kuhusu uhamishaji wa Wapalestina.

Mfalme Abdullah alegeza msimamo wake

Kauli iliyovutia wengi kutoka kwa Trump ni kwamba ingawa Mfalme Abdullah awali alikataa kuwachukua Wapalestina, sasa amekuwa mmoja wa waasisi wakuu wa mpango huu. Hii inaashiria mabadiliko katika msimamo wa Jordan, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiepuka kuchukua wakimbizi wa Kipalestina.

Trump alieleza kuwa mazungumzo yao yalihusu mipango ya kutafuta maeneo mbadala kwa Wapalestina waliohamishwa, huku Jordan na Misri zikihusishwa kwa karibu. Alihimiza kuwa kuhama kwao kutoka Gaza kungewawezesha kuishi kwa usalama na ustawi mkubwa.

Mfalme abdullah kwa kuonesha Nia kaahidi kuchukua maelfu ya wapalestina kabla ya makubaliano rasmi

Nafasi ya Saudi Arabia na Misri Katika Mpango wa Uhamisho

Mfalme wa Jordan amesema Mwana wa Mfalme wa Saudi arabia Mohammed bin Salman amewaita Jordan na Egypt wakutane Riyadh ili kusuka mpango kazi wa kuunga mkono Plan ya Trump ya kuwahamisha Wapalestina,Lengo likiwa ni kudumisha utulivu katika eneo hilo, King Abdullah kalegeza msimamo wake mkali kama mkate mgumu mbele ya chai yamoto

Mpango wa Kuhamisha Wapalestina kutoka Gaza: Juhudi za Kimataifa


Mada kuu ya mazungumzo ilikuwa maono ya Trump kwa Wapalestina waliopo Gaza. Alisema kwamba Wapalestina wako Gaza kwa sababu hawajawahi kuwa na chaguo jingine, akieleza kuwa "hakuna hata mtu mmoja atakayependa kubaki pale" mara tu atakapopata mbadala mzuri.

Trump alieleza kuwa mataifa mengine pia yameonesha nia ya kusaidia. Mbali na Jordan na Misri, nchi kama Indonesia na Albania pia zimeonyesha utayari wa kushiriki katika juhudi za kuwahamisha Wapalestina. Alisisitiza kuwa kuna nchi nyingi zinazotaka kusaidia kwa sababu kuna "hisia kubwa ya kusaidia Wapalestina."

Trump alifafanua kuwa hali ya sasa ya Gaza haiwezi kudumu na kuwa mpango wa kuhamisha wakazi wake utaleta amani ya muda mrefu. Alisisitiza kuwa eneo hilo litapokea uwekezaji mkubwa wa kiuchumi, na kwa muda, Gaza itabadilika kutoka kuwa eneo la mzozo na kuwa kitovu cha maendeleo.

Gaza kuwa chini ya Marekani

Trump alisema kwamba Marekani itaisimimia Gaza na kuijennga upya kwasabu hali ya sasa ni hatarishi kwa wapalestina kubaki, eneo limechakazwa kwa vita na hali hiyo ina uwezekano wa kujirudia kama wapalestina hawatahamishwa akigusia Hamas walivyoua watu zaidi elf 1 ndani ya Israel siku ya October 7. alisema kuwa Marekani itaichukua na kuishikilia Gaza, kuiendeleza, na kuifanya kuwa sehemu yenye fursa za kiuchumi. Alisisitiza kuwa Gaza itapokea maendeleo makubwa, yakiwemo hoteli, majengo ya ofisi, na makazi, ambayo yatazalisha ajira kwa watu wa Mashariki ya Kati. Trump alitaja kuwa lengo kuu ni kuleta utulivu na amani ya kudumu katika eneo hilo.

Onyo la Trump kwa Hamas: Muda wa Mwisho wa Jumamosi Saa Sita Mchana


Sehemu nyingine muhimu ya mkutano wa Trump ilikuwa onyo kali kwa Hamas, akisisitiza kuwa iwapo mateka hawataachiwa huru ifikapo Jumamosi saa sita mchana, "hakutakuwa na mjadala tena." Alielezea kuwa Hamas italazimika kukabiliana na matokeo makubwa ikiwa hawatazingatia makubaliano.

Trump alikosoa vikali mbinu za Hamas za kuchelewesha kuachia mateka kwa awamu, akisisitiza kuwa Marekani na washirika wake hawataruhusu ucheleweshaji wowote zaidi.

Ni muda kwa nchi za kiarabu kuonyesha mapenzi ya dhati kwa Palestina kwa Vitendo, kwa muda mrefu nchi za kiarabu zimekuwa haziwataki Wapalestina walio chini ya utawala wa kimabavu wa Hamas, FREE GAZA !


View: https://www.youtube.com/watch?v=uubzgf1UiTI
 
Mfalme wa Jordan kaenda Ikulu ya Marekani (White House) Pamoja na mtoto wake wamemuunga mkono Rais wa Marekani Donald Trump kwa mpango wa kuwahamisha wapalestina.

Kuonyesha nia kabla ya makubaliano rasmi, Mfalme atawachukua watoto 2,000

Kuna kikao kimeshaandaliwa Saudi Arabia kwa nchi kadhaa za mashariki ya kati akiwemo Misri kusuka mpango kazi wa kuwasaidia wapalestina wanaoishi kwa taabu huko Gaza kwa kuwatafutia maeneo ndani ya nchi zao

Aidha Trump kawakumbusha Hamas, Deadline ya kuwaachia watu wote waliotekwa ni Jumamosi lasivyo Hell will break loose

Super Power ikiwa na Super Leader ni kolabo la kukaa nalo mbali


View: https://www.youtube.com/watch?v=uubzgf1UiTI


View: https://youtu.be/3_8_fbJcKug?si=O_-KOcucEfwsUGxp
 
Kuonyesha nia kabla ya makubaliano rasmi, Mfalme atawachukua watoto 2,000

Kuna kikao kimeshaandaliwa Saudi Arabia kwa nchi kadhaa za mashariki ya kati akiwemo Misri kusuka mpango kazi wa kuwasaidia wapalestina wanaoishi kwa taabu huko Gaza kwa kuwatafutia maeneo ndani ya nchi zao
Hamas wa Vingunguti wanashirikishwa kwenye huu mpango?
 
Mfalme wa Jordan kaenda Ikulu ya Marekani (White House) Pamoja na mtoto wake wamemuunga mkono Rais wa Marekani Donald Trump kwa mpango wa kuwahamisha wapalestina.

Kuonyesha nia kabla ya makubaliano rasmi, Mfalme atawachukua watoto 2,000

Kuna kikao kimeshaandaliwa Saudi Arabia kwa nchi kadhaa za mashariki ya kati akiwemo Misri kusuka mpango kazi wa kuwasaidia wapalestina wanaoishi kwa taabu huko Gaza kwa kuwatafutia maeneo ndani ya nchi zao

Aidha Trump kawakumbusha Hamas, Deadline ya kuwaachia watu wote waliotekwa ni Jumamosi lasivyo Hell will break loose

Super Power ikiwa na Super Leader ni kolabo la kukaa nalo mbali


View: https://www.youtube.com/watch?v=uubzgf1UiTI


Mkuu round kick! Imeshingaza na kunistusha! Sikutegemea kuna nchi ya Kiarabu hata moja inaweza kukaribisha wazo hilo! Nimeona nguvu ya US behind the scene! Nchi kama Jordan zinasimama kwa msaada wa Marekani! Unapochukua watu 2000, maana ni familia za watu 2000! Nilijua toka Trump alipotoa wazo la kuwaondoa Wapelestina Gaza, hata baadhi ya Wapelestina watataka kuondoka! Nimesoma mahali kuna baadhi ya Wapelestina wanasema Waarabu wenzetu sio kama wanatupenda wakitaka tubaki Gaza, bali hawataki tuenda nchi zao!

Trump yuko very calm, anasema hata Saudia na nchi za kiarabu zitakubali proposal yake! Kila siku kuna mpya middl east!
 
USA Haiwezi shindwa, lile ni Taifa kubwa

Azarel, ukweli ndio huo hata kama wengi hawataki kukubali! Pressure behind the scene, nchi kama Jordan, kuanzia babake aliwekwa na Waingereza, ni vigumu mno kuikatalia Marekani!
 
Hii habari mwenzetu uneitoa wapi?

Nimeiona kwenye live, Fox News! In short nilisthtuka sana, sikutegemea kabisa kuna nchi ya kiarabu inaweza kubadili msimamo wao! Unajua wazi pressure ya Trump behind the scene, halafu miaka yote Utawala wa Jordan uko kwa support kubwa ya US!
 
Mkuu nchi za kiarabu kizitoa support tu, that is end of Gaza!
Sikiliza ile video clip ya ile meeting kati ya Trump na King Abdullah, the King amesema akirudi Mwanawa Mfalme wa Saudi arabia amewaita Riyadh Jordan na Egypt ili wakakamilishe namna wataunga mkono Trump plan. Pale tu kwenye kikao King Abdullah kalegeza msimamo wake mkali
 
Huyo Mfalme kama kachoka kukaa Ikulu afanye huo ujinga, analindwa na Israel na USA lakini yuko wapi Assad aliyekuwa analindwa na Russia
 
Ndio kakuambia kaenda kuuza Palestina!!! nyie subilieni Dodo kwenye Mwarubaini huu mwaka uyo Puto wenu Tramp anaenda kuchezea kichapo kikali zaid ajiandae na mavikwazo yake ndio kimbilio lake lkn Kijesh !!!! Wauni Wamechoka ujinga wa Marekan!!i atazika vijana wake uyo Puto mwisho atakimbila kwenye vikwazo!!! Vita Marekani aziwez,
 
Back
Top Bottom