Mfalme wa Jordan kaenda white house kamuunga mkono Trump kuwahamisha wapalestina, Misri na nchi nyingine kukutana Saudi Arabia kusuka mpango kazi

Mfalme wa Jordan kaenda white house kamuunga mkono Trump kuwahamisha wapalestina, Misri na nchi nyingine kukutana Saudi Arabia kusuka mpango kazi

Huyo Mfalme kama kachoka kukaa Ikulu afanye huo ujinga, analindwa na Israel na USA lakini yuko wapi Assad aliyekuwa analindwa na Russia
Mbona tayari kakubali sasa.Kuanzia atachukua watoto na badae utaratibu mwingine utafuata(Arabs can't be trusted).Kikubwa tulieni tu maana Misri hana kauli kwa Marekani ,huyo mwana wa mfalme wa Saudia ndio kabisa kwa Trump hawezi kunyanyua mdomo
 
Hao wakazi wa Gaza ina maana hawatafaidika na lolote na hiyo Gaza mpya??
Yaani mnatimuliwa kabisa aisee.

Wacha tusubiri .
 
Mfalme Abdullah wa Jordan na Mwanawe Wamtembelea Trump Ikulu

Mfalme Abdullah wa Jordan na mwanawe wametembelea Ikulu ya White House kwa mazungumzo na Rais wa Marekani, Donald Trump. Mkutano huo uliangazia juhudi zinazoendelea za kubadilisha mwelekeo wa Mashariki ya Kati, hasa kuhusu uhamishaji wa Wapalestina.

Mfalme Abdullah alegeza msimamo wake

Kauli iliyovutia wengi kutoka kwa Trump ni kwamba ingawa Mfalme Abdullah awali alikataa kuwachukua Wapalestina, sasa amekuwa mmoja wa waasisi wakuu wa mpango huu. Hii inaashiria mabadiliko katika msimamo wa Jordan, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiepuka kuchukua wakimbizi wa Kipalestina.

Trump alieleza kuwa mazungumzo yao yalihusu mipango ya kutafuta maeneo mbadala kwa Wapalestina waliohamishwa, huku Jordan na Misri zikihusishwa kwa karibu. Alihimiza kuwa kuhama kwao kutoka Gaza kungewawezesha kuishi kwa usalama na ustawi mkubwa.

Mfalme abdullah kwa kuonesha Nia kaahidi kuchukua maelfu ya wapalestina kabla ya makubaliano rasmi

Nafasi ya Saudi Arabia na Misri Katika Mpango wa Uhamisho

Mfalme wa Jordan amesema Mwana wa Mfalme wa Saudi arabia Mohammed bin Salman amewaita Jordan na Egypt wakutane Riyadh ili kusuka mpango kazi wa kuunga mkono Plan ya Trump ya kuwahamisha Wapalestina,Lengo likiwa ni kudumisha utulivu katika eneo hilo, King Abdullah kalegeza msimamo wake mkali kama mkate mgumu mbele ya chai yamoto

Mpango wa Kuhamisha Wapalestina kutoka Gaza: Juhudi za Kimataifa


Mada kuu ya mazungumzo ilikuwa maono ya Trump kwa Wapalestina waliopo Gaza. Alisema kwamba Wapalestina wako Gaza kwa sababu hawajawahi kuwa na chaguo jingine, akieleza kuwa "hakuna hata mtu mmoja atakayependa kubaki pale" mara tu atakapopata mbadala mzuri.

Trump alieleza kuwa mataifa mengine pia yameonesha nia ya kusaidia. Mbali na Jordan na Misri, nchi kama Indonesia na Albania pia zimeonyesha utayari wa kushiriki katika juhudi za kuwahamisha Wapalestina. Alisisitiza kuwa kuna nchi nyingi zinazotaka kusaidia kwa sababu kuna "hisia kubwa ya kusaidia Wapalestina."

Trump alifafanua kuwa hali ya sasa ya Gaza haiwezi kudumu na kuwa mpango wa kuhamisha wakazi wake utaleta amani ya muda mrefu. Alisisitiza kuwa eneo hilo litapokea uwekezaji mkubwa wa kiuchumi, na kwa muda, Gaza itabadilika kutoka kuwa eneo la mzozo na kuwa kitovu cha maendeleo.

Gaza kuwa chini ya Marekani

Trump alisema kwamba Marekani itaisimimia Gaza na kuijennga upya kwasabu hali ya sasa ni hatarishi kwa wapalestina kubaki, eneo limechakazwa kwa vita na hali hiyo ina uwezekano wa kujirudia kama wapalestina hawatahamishwa akigusia Hamas walivyoua watu zaidi elf 1 ndani ya Israel siku ya October 7. alisema kuwa Marekani itaichukua na kuishikilia Gaza, kuiendeleza, na kuifanya kuwa sehemu yenye fursa za kiuchumi. Alisisitiza kuwa Gaza itapokea maendeleo makubwa, yakiwemo hoteli, majengo ya ofisi, na makazi, ambayo yatazalisha ajira kwa watu wa Mashariki ya Kati. Trump alitaja kuwa lengo kuu ni kuleta utulivu na amani ya kudumu katika eneo hilo.

Onyo la Trump kwa Hamas: Muda wa Mwisho wa Jumamosi Saa Sita Mchana


Sehemu nyingine muhimu ya mkutano wa Trump ilikuwa onyo kali kwa Hamas, akisisitiza kuwa iwapo mateka hawataachiwa huru ifikapo Jumamosi saa sita mchana, "hakutakuwa na mjadala tena." Alielezea kuwa Hamas italazimika kukabiliana na matokeo makubwa ikiwa hawatazingatia makubaliano.

Trump alikosoa vikali mbinu za Hamas za kuchelewesha kuachia mateka kwa awamu, akisisitiza kuwa Marekani na washirika wake hawataruhusu ucheleweshaji wowote zaidi.

Ni muda kwa nchi za kiarabu kuonyesha mapenzi ya dhati kwa Palestina kwa Vitendo, kwa muda mrefu nchi za kiarabu zimekuwa haziwataki Wapalestina walio chini ya utawala wa kimabavu wa Hamas, FREE GAZA !


View: https://www.youtube.com/watch?v=uubzgf1UiTI

Trump ndo mtu sahihi wa kuimalizia usa
 
Ila waarabu bhana 😁dah,Yani mgeni kutoka mbali anakuja kukubwekea nyumbani kwako na kukupangia Cha kufanya
 
Back
Top Bottom