Mfalme Zumaridi, Mama huyu ni nani na kwanini Serikali imemuacha tu?

yupo wrong from the beginning,Hairuhusiwi mwanamke kuwa mchungaji,muhubiri,muinjiristi wala shemasi hawajawahi kuwepo kwenye biblia,kwa lugha nyingine mwanamke haruhusiwi kusimama madhabahuni na akawafundisha wanaume,wanawake sababu yeye si kichwa,yeye alidanganywa mwanzo
 
Mfalme wa kike. Hapo tu jua unapigwa.
Manabii waliokuwepo,walikuja kwa ajili ya kuutambulisha ulimwengu juu ya uwepo wa Mungu.Walimaliza kazi yao na walirudi kwenye ufalme wa Mungu.Hakuna tena unabii mwingine.Hawa manabii wote wa sasa ni wapiga dili tu,wala siyo wachamungu.Ukiwafuatilia mambo yao utapatwa mshangao wa hali ya juu.
 
mfalme wavkike na nabii wa kike sio manabii wa kike. kuwa makini mkuu utaliwa
 
Kwa hiyo hayupo mwenye habari zake, za hata kule alikoanzia? Kuna mwingine Nyamanoro anajiita Nabii Rhoda
 
Akili za walokole wanazijua wenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani huyo mungu mtu ameolewa?
Kwenu wapi weye? Mfalme tena mwanamume wa wanaume aolewe tena!!! Labda uliza hivi; Ameoa?? Mke wa mfalme huitwa "Malkia". Hata yule wa nyuki huitwa malkia ndo maana hutaga mayai baada ya kupandwa na madume nyuki. Sasa weye wataka "Mfalme" aoulewe?? Maajabu gani unatuletea.
 
Habari kutoka kanda ya ziwa kutoka Kanisa la huyu mama Nabii Zumaridi lililopo Mkuyuni mkoani Mwanza

Inaelezwa kwamba Nabii Zumaridi ameamua kuchukua mamlaka ya Mungu chini ya jua, kwamba anajiita Mungu, hali hiyo iliyopelekea kufikia hatua kwa Waumini wake pamoja na wafuasi wake kumwabudu, kumtukuza na kumsujudia.

Anavyofanya huyu mama si sawa kabisa, ifike mahala Serikali ichukue hatua kwa mambo kama haya ya upotoshaji huu.

Na kwanini wahanga wengi wa mambo kama haya ni wanawake..!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…