Mfalme Zumaridi, Mama huyu ni nani na kwanini Serikali imemuacha tu?

Mfalme Zumaridi, Mama huyu ni nani na kwanini Serikali imemuacha tu?

Angekuwa mzungu au mwarabu huenda mngeamini. Walau naye kaanzisha dhehebu la waafrika maana waafrika tu ndiyo tulikana madhehebu yetu na kuanza kufuata ya weupe na ndiyo maana ni bara maskini kuliko yote. Waindi wana madhehebu yao, waarabu pia, wachina, wazungu sisi ni wazee wa kucopy na tunajifanya tunaujua Ukristo na Uislam kuliko hata waanzilishi.
Go Zumaridi japo mimi siwezi kuwa muumini wako
😂😂😂😂😂Huoni Kama kanisa mkuu. Ila hili wameliupgrade
 
Mfalme Zumaridi

Kipindi cha nyuma kidogo niliwahi kuishi Nyegezi stendi mtaa wa Nyamanzobe kwa hiyo bili ya maji nilikuwa ninaenda kulipia Iseni ofisi ndogo ya Idara ya Maji.

Kanisa la Mfalme Zumaridi liko karibu sana sana na Idara ya Maji (jirani). Kipindi cha nyuma niliwahi kuwa na rafaki yangu ambaye alikuwa anasali kanisani kwa Mfalme Zumaridi, rafiki yangu alivutika kanisani baada ya Star tv kulipoti eti kuna wachawi wameshikwa kanisani kwa huyu mama kipindi hicho. Kanisa lake liko bohari chini kidogo ya iseni kwa hiyo kipindi hicho alipata sana waumini mno.

Kwanza kabisa ukisikia Mfalme Zumaridi elewa kabisa huyu ndio Mungu wao na ukienda kanisani kwao na ukasema "MUNGU" tu bila kuweka zumaridi waumini wanaweza kukuombea hadi ukafa.

Yaani kanisani kwao nenda muda wowote kuna watu na sio wachache wengi sana cha ajabu wanaume ndio wengi sana. Huyu mama hana mume kuna muda hasa Jumapili kwenye ibada kubwa huwa anasalimia salamu zao baada ya hapo anasema ana ujumbe kutoka kwa baba Mfalme Zumaridi then anasema "Jana usiku mungu wa Zumaridi kaniotesha nimepata mume kanisani".

Baada ya hapo waumini wanakaa na kusubiri kuona nani bahati imemwangukia ya kupendwa na Mfalme Zumaridi
Akibahatika hapo hapo huyo mama anajifungisha ndoa fast baada ya muda ndoa hakuna anachangua mwengine.

Iseni iko karibu sana na kambi ya jeshi ya nyegezi kona kwa hiyo huyu mama huwa anawashika sana wanajeshi hasa wale ambao wanakaribia kustaafu huyu anawafanya watenge familia zao kabisa.

Mama huyu kuna tax nyeupe huwa anapenda kutembelea alinunuliwa na mwanajeshi mmoja ambaye alikuwa ametoka kuchukua pesa zake za mafao hakurudi alizipeleka kanisani mama akazibariki hakurudi tena nyumbani hadi pale mke wange alichukua watoto na kuwapeleka pale kanisani na kuanza kulia sana ndio yule mama alimwachia mzee yule ambaye alirudi nyumbani bila senti hata moja.

Pia mama anachapa sana waumini wake fimbo.

Ni hayo machache kuhusu hili kanisa
 
Kwa kujiita tu mfalme wakati ni Ke unaona hamna kitu hapo

Ni kweli mkuu. Mungu atusaidie sana kutuelekeza wapi panakweli.! Mie najiulizaga kwanini mambo kama haya yanatokea kama yapo kinyume naye kwanini aruhusu watu wake waangamie kama anatupenda kweli? Ilipaswa unapotokea ujinga au upotoshaji wowote juu yake angewawajibisha ili watu wamheshimu lakini Mungu anaangalia tu [emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
 
2 Timotheo 4:1-4
1 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;

2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.

3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;

4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
 
Ni kweli mkuu. Mungu atusaidie sana kutuelekeza wapi panakweli.! Mie najiulizaga kwanini mambo kama haya yanatokea kama yapo kinyume naye kwanini aruhusu watu wake waangamie kama anatupenda kweli? Ilipaswa unapotokea ujinga au upotoshaji wowote juu yake angewawajibisha ili watu wamheshimu lakini Mungu anaangalia tu [emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
Mungu wetu ni Mungu wa uhuru asiyeingilia uchaguzi wetu binafsi ametupa uwezo wa sisi kuamua mambo yetu binafsi, alichofanya ni kutoa muongozo kupitia neno lake ili tufahamu lipi jema na lipi ni baya lakini halazimishi utende yoyote kati ya hayo

Hawa nao huachwa ili kama vile ambavyo alimuacha shetani aendelee kuwepo pamoja na kuwa ndiye muanzilishi wa dhambi ili kuonyesha siyo dikteta anayetaka tu watu wafuate anachokitaka so hawa wataendelea kuwepo ila alishanena hbr zao ktk sura ya 24 ya Mathayo kuwa wataibuka manabii wa uongo siku za mwisho sisi tunaowaona leo ni kuwapima kama ni wa kweli au uongo maana anasema msiziamini kila Roho maana nyingine zinatoka kwa ibilisi
 
Back
Top Bottom