Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 43,960
- 77,533
Wanataka wale na vya madhabahuni?Wale vya CRO.😂😂😂Ajiongeze sasa,kwani police huwa wanataka nini.Asipojiongeza ataoza. Jela ni kwa ajili yetu masikini.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanataka wale na vya madhabahuni?Wale vya CRO.😂😂😂Ajiongeze sasa,kwani police huwa wanataka nini.Asipojiongeza ataoza. Jela ni kwa ajili yetu masikini.
Hatari sana, ile miuno minginyu minginyu sijui ataifanyia wapi...Mfalme apelekewe vipodozi vyake huko mahabusu....waumini watamsahau .
uno atakatia huko huko mahabusu 😁😁Hatari sana, ile miuno minginyu minginyu sijui ataifanyia wapi...
Ila serikali ikikuamulia aisee...
Diana Bundala maarufu kama 'Mfalme Zumaridi' na wenzake 83 leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali ya mashtaka yanayowakabili.
Zumaridi na wenzake wanakabiliwa na makosa matatu ikiwamo ya usafirishaji haramu wa binadamu, shambulio la kudhuru mwili na kuzuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu wao.
Wakati wa kuwasili ndani ya chumba cha Mahakama Zumaridi ameonekana akiwa amejifunika na kitenge wakati wote kisha akalazimika kukiondoa baada ya kupanda kizimbani kusomewa maelezo hayo.
Hata hivyo, washtakiwa hao hawakusomewa maelezo ya awali ya mashtaka yanayowakabili kutokana na Hakimu Mkazi mwandamizi, Monica Ndyekobora ambaye ndiyo mwenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kutokuwepo leo mahakamani jambo lililosababisha mashauri hayo kusikilizwa na Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Stela Kiama.
Washtakiwa baada ya kufikishwa mahakamani wamesomewa mashtaka yanayowakabili na wakili wa Serikali Mwandamizi anayeendesha mashtaka hayo, Emmanuel Luvinga akishirikina na Gisela Bantulaki.
Katika shauri hilo, kuna mashtaka matatu yanayowakabili washtakiwa hao ambayo ni kesi ya jinai namba 11/2022 ambayo ni usafirishaji haramu wa binadamu inayomkabili mfalme Zumaridi peke yake, kesi ya jinai namba 10/2022 ambayo ni kufanya shambulio la kudhuru mwili kwa lengo la kuzuia maofisa wa serikali kutimiza wajibu wao linalomkabili Zumaridi na wenzake 8.
Nyingine ni kesi ya jinai namba 12/2022 inayomkabili mhubiri huyo na wenzake 83 ambayo ni kufanya kusanyiko lisilo rasmi.
Baada ya Washtakiwa kusomewa mashtaka hayo, wakili wa utetezi, Erick Mutta aliwasilisha maombi ya dhamana kwa washtakiwa wanane wanaoendelea kusota rumande na mhubiri huyo ambayo yalikubaliwa na mahakama hiyo baada ya washtakiwa kukidhiri vigezo na masharti ya dhamana.
Kwa upande wake, Mfalme Zumaridi kutokana na kukabiliwa na kesi ya usafirishaji haramu wa binadamu isiyo na dhamana anaendelea kusota rumande na washtakiwa wenzake nane ambao hawajakidhi vigezo vya kupewa dhamana.
Shauri hilo limeahirishwa hadi Aprili 4, mwaka huu litakapoitwa kwa ajili ya kusomwa maelezo ya awali kwa washtakiwa.
Katika hatua nyingine, wakili wa utetezi Erick Mutta ameiambia mahakama hiyo kwamba, mshtakiwa namba 67 (Elias Joseph) ameshindwa kufika mahakamani hapo kutokana na maofisa kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kufika ofisi kwake kwa ajili ya kumfanyia ukaguzi.
Amesema mshtakiwa namba 38 (Maria Joseph) ameshindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando akipatiwa matibabu ya majeraha aliyopata wakati wa ukatamaji uliofanywa na maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani humo.
Pia amesema mshtakiwa namba 84 (Kanyangi Mary) na 68 wameshindwa kuhudhuria shauri hilo kutokana na kuhudhuria matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure.
Chanzo: Mwananchi
Hatimaye anayejiita MUNGU mahakamani,hata hivyo huu upuuzi uliachwa muda Sana!

Sawa, ila bado tuko jamii inayotoa nafasi kwa baadhi ya watu kutoa hukumu kabla hukumu ili kutesana tu.Kuna mengi yanayoweza nyima mtuhumiwa zamana
1.kama akiwa nje asije ingilia upelelez
2.asije tokomea kusiko julikana
Wabongo tuache ujuaji kidogo, maelezo yanasema kesi yake ya jinai haina dhamana wewe unataka apewe dhamana.Ni upumbavu pili mtuhumiwa ana mali nyingi tena zisizohamishika kwann zisitumike kama dhamana.
Pili hili la hakimu husika kutokuwepo siku ya kesi husika, kwann asiwepo nani anabeba hii Dhamana ya mtu kupigwa tarehe tena hadi hakimu awepo.
Sasa wewe unaona hizo kesi tatu zina point za kumtia hatiani?Wabongo tuache ujuaji kidogo, maelezo yanasema kesi yake ya jinai haina dhamana wewe unataka apewe dhamana.
Labda icho unachokiomba ulishawahi kukisikia kinafanyika wapi? Mtu anakesi ya jinai alafu anapewa dhamana.
Sisi kilakitu nikulalamika tu, angepewa dhamana tungelalamika kwanini apewe dhamana kwa kesi ya jinai, amenyiwa bado tunalalamika vilevile
Kwa uelewa wangu ni kuwa kesi yake itaendelea kusikilizwa akitokea rumande kwa sababu haina dhamana.Sasa wewe unaona hizo kesi tatu zina point za kumtia hatiani?
Hio ya usafirishaji haramu si hadi wapatikane ushahidi
MunguWengi tunaamini mafundisho yake yanapingana na Mungu lakini tuwe waangalifu tusijipe kazi ya Mungu ya kumhukumu kutumia sheria zetu za Duniani.
Kama kumweka mtu rumande kwenye mrundikano wa watu na maisha mabovu kama ya mifugo sio lazima, basi huo ni uonevu ambao hata huyo Mungu hapendi.
Ni uonevu lakini,mbona waganga wa kienyeji waharibu Sana Maisha ya watu na hata ukienda kwenye majumba yao watu wamekusanyika bila kibali,wao mbona awakamatwiKwa uelewa wangu ni kuwa kesi yake itaendelea kusikilizwa akitokea rumande kwa sababu haina dhamana.
Endapo ushahidi usipothibitisha anayo hatia basi ataachiwa huru. Ila kesi kesi yake haitosikilizwa akitokea nyumbani haina dhamana, labda wamfutie ilo shitaka la jinai abaki na hayo mengine
Wenzako waligeuka makerubi, hawasikii maumivu wala amri walikuwa wanamlinda Mungu wao Zumaridi!! Wajinga ndio waliwao!!Naona watuhumiwa wapigwa sana sasa hao ni kina mama uwe mwanaume ni kuvunjana miguu kma yule wa mauaji ya msuya.
3.Ananyimwa dhamana kwa ajili ya usalama wake mwenyewe.Kuna mengi yanayoweza nyima mtuhumiwa zamana
1.kama akiwa nje asije ingilia upelelez
2.asije tokomea kusiko julikana