Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Nimesikiliza sehemu ya mahojiano kati ya mkuu wa mkoa wa Arusha Makonda na waandishi wa habari. Jambo mojawapo aliloulizwa ni tuhuma dhidi yake za ukiukwaji wa haki za binadamu, majibu yake yameniacha hoi kwa mshangao.
Makonda anasema yeye ni mtetezi mkubwa wa haki za binadamu, mifano aliyoitoa ni kuhusu kushughulikia waliotapeliwa na Mr. Manguruwe pamoja kesi fulani ya mgogoro wa deni kati ya mdaiwa mmoja anayedai alikopeshwa milioni 3 akanyang'anywa nyumba ya milioni 50.
Hivi kweli mtu anayeongoza jiji kubwa la Arusha hajui hata maana ya haki za binadamu na mifano yake sahihi?! Yani kesi za madai na watu wengine ambao wametapeliwa huenda tena kwa ushamba wao tu yeye ndio anaona mifano sahihi ya kumtambulisha kama mtetezi mkubwa wa haki za binadamu kwa tuhuma nzito anazoshutumiwa nazo!
Hivi hakika ni vituko vitupu.