Mzee Emil Lesheya Woiso amefariki leo asubuhi. Msiba upo nyumbani kwake Tegeta karibu na IPTL.
Alikuwa mmiliki wa Tarakea Restaurant pale Mwenge na Cornelius Girls Secondary School pale Tegeta Skanska
natoa faraja kwa wafiwa. kifo kinauma, ukifiwa moyo unaumia, wanahitaji wafarijiwe. hata Yesu alilia pamoja na waliolia.
ila nyote mnaosoma hapa, jiandaeni kwa kifo kwa kumpa Yesu Maisha yenu ili kama mkifa mfe katika Bwana na mkiishi muishi katika Bwana. msidanganywe na mapadre na wachungaji wanaowadanganya kwamba mkifa wataombea maiti zenu au makaburi yenu na huko mliko mtasamehewa. baada ya kifo ni hukumu. hivi ndio vifungo vimewafanya wakatoliki na watu wa dini zingine waogope hata kuondoka,ndio mnyororo na pingu za kuwashikilia kwenye madhehebuhayo yasiyo na Mungu, watu wanaogopa wakiondoka watazikwa na nani? nani atawaombea wakiwa maiti? as if wakiombewa watasamehewa. Kama ingekuwa mtu akifa anaombewa na kusamehewa Mungu asingeelekeza tuache dhambi, si ndugu zangu wangeniombea? unafanya zako dhambi, unakufa, wanakuombea ndugu zako, unaenda mbinguni. ingewezekana kweli?
BIBLIA INASEMA KATIKA UFUNUO 14:13; Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
MANAKE, ukifa matendo yako yatafuatana nawe, yaani yatakufuata ukahukumiwe nayo, pale tu unapokufa, jua ndio itakuwa deadline ya wewe kutengeneza na Mungu kwa kutubia dhambi zako, hatutubu tukiwa tumekufa, opportunity hiyo ni ukiwa hai. na hii mkifunguka itawasaidia kuyakimbia makanisa yasiyohubiri wokovu, hayo yanayohubiri kuomba kwa maria na wafu badala ya Jina la Yesu, hayo yanayohubiri kuombea watu as if wao ndio wenye ticket ya kukufanya uende mbinguni au motoni, wao wenyewe hawana Mungu. kimbieni huko, kimbieniiii.