Mfanyabiashara kijana aandaa kaburi lake baada ya kukiuka masharti ya Mganga

Mfanyabiashara kijana aandaa kaburi lake baada ya kukiuka masharti ya Mganga

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Mfanyabiashara Kijana wa Nakonde nchini Zambia mwenye umri wa miaka 29 ameanza kuandaa kaburi lake baada ya kuambiwa na Mganga wake wa Sumbawanga kuwa atakufa hivi karibuni kwa kukiuka masharti ya utajiri wake.

Grigory Siame ambaye alikuwa maskini sana hadi alipoenda kuonana na mganga miaka 8 iliyopita, anasemekana kukiuka masharti baada ya kuabiri moja ya magari yake 5 mapya aliyonunua.

Bw Siame anasemekana kumiliki saloon za kisasa za kiume 89 na vibanda vya simu za njiani BoothTelephone) 240 huko Nakonde na Tunduma ambapo hukusanya ZMK28,000 sawa na TSH 3,975,000 kwa siku.

Pamoja na kumsihi sangoma huyo amsamehe au kumbadilishia adhabu, Lakini juhudi zake hizo ziligonga mwamba.

Kwa sasa tajiri huyo mtoto anajiandaa kufa hata ukimwangalia anaonekana Kuwa ni mtu aliyekata tamaa.

Ukipenda hembu sema neno la faraja kwake.

Screenshot_20220720_000720.jpg
 
Siame ni ukoo wa machifu wa wanyamwanga Sumbawanga
Au hilo jina alifoji? Ukoo wa Siame hawana tabia ya kudhulumu mtu au kwenda kutafuta utajiri wa kishirikina

Huyo sio ukoo wa Siame wacha yamkute kafoji Jina la watu ukoo wa kichifu halafu anaenda kishirikina wakati ukoo huo wa Siame ushirikina kwao mwiko.Afe tu
 
Siame ni ukoo wa machifu wa wanyamwanga Sumbawanga
Au hilo jina alifoji? Ukoo wa Siame hawana tabia ya kudhulumu mtu au kwenda kutafuta utajiri wa kishirikina

Huyo sio ukoo wa Siame wacha yamkute kafoji Jina la watu ukoo wa kichifu halafu anaenda kishirikina wakati ukoo.huo wa Siame ushirikina kwao mwiko.Afe tu
Hivi kuna tofauti kati ya chifu na mchawi,mwanga kigagu,mshirikina?
 
Back
Top Bottom