Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 753
- 1,812
Mfanyabiashara maarufu katika mikoa ya Arusha, Dar na Dodoma Joseph Kalugendo mkazi wa Moshoni jijini Arusha, ameibiwa fedha zake zaidi ya milioni 100 katika benki ya NMB tawi la Clock Tower Arusha na mtumishi wa benki hiyo.
Taarifa ambazo zimethibitishwa na Mfanyabiashara huyo amedai kuwa siku za usoni alienda katika benki hiyo kwa ajili ya kuchukua fedha ndipo alipopigwa na butwaa kukuta kitita hicho hakipo.
Meneja wa benki hiyo Kanda ya Kaskazini Praygod Mphuru alipohojiwa alikiri kuwepo kwa tukio hilo akidai tayari wamemsimamisha kazi mfanyakazi wao Samweli na kwamba suala hilo linafanyiwa kazi na kuomba suala hilo lisitangazwe.
Pia vigogo wa benki hiyo kwa sasa wanahaha kutafuta mchawi aliyetoa taarifa hizo kwa waandishi wa habari na tayari baadhi ya wafanyakazi wameitwa na kuhojiwa juu ya taarifa hizo za ndani kufika kwa wanahabari
Joseph ambaye hufanya biashara za bar na kusambaza vyakula kwenye kambi za jeshi anadaiwa kulundika kiasi hicho cha fedha kwa muda mrefu bila kutoa kiasi, na kwamba mfanyakazi huyo aliona huenda anayeimiliki alishakufa na kuanza kuchomoa kidogo kidogo na kufikia zaidi ya Tsh. Milioni 100.
Hata hivyo baada ya taarifa hizo kubainika uongozi wa benki ulifanya kikao kizito na kubaini kwamba mfanyakazi wao aliyefahamika kwa jina moja la Samweli ndiye aliyehusika na wizi huo kwa kuchomoa fedha hizo kidogo kidogo hadi kufikia hicho cha fedha.
Uongozi wa benki hiyo tayari umemsimamisha kazi lakini suala hilo bado lipo kimya huku Mfanyabiashara huyo akilalamikia hatima ya fedha zake, maana benki hiyo kuwa kimya na haimpi jibu linaloeweka namna ya kurejeshewa.