DOKEZO Mfanyabiashara maarufu Arusha aibiwa Tsh. Milioni 100 kwenye akaunti ya Benki ya NMB

DOKEZO Mfanyabiashara maarufu Arusha aibiwa Tsh. Milioni 100 kwenye akaunti ya Benki ya NMB

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Haya mambo NMB ni kawaida ina wafanyakazi wezi wezi wanaajiriana kwa madili.. siwezi kuweka pesa yangu NMB hata juzi nimetoka kuweka mil 700 Exim bank coz nawaamini, hata balays toka mwaka juzi wamanitunzia bil 2 kiuaminifu kabisa. Bil 2 ni fedha ndogo ndio maana nimeitunza tu
 
Haya mambo NMB ni kawaida ina wafanyakazi wezi wezi wanaajiriana kwa madili.. siwezi kuweka pesa yangu NMB hata juzi nimetoka kuweka mil 700 Exim bank coz nawaamini, hata balays toka mwaka juzi wamanitunzia bil 2 kiuaminifu kabisa. Bil 2 ni fedha ndogo ndio maana nimeitunza tu
Kweli kabisa hutwo tubilioni tuwili ni tuela twa mboga tu! (joke).
 
Huwa hawafanyi hivyo.

Wanajifanya mteja mwenye account alikuja kuomba atm card mpya. Wanamjazisha fomu kisha wanatengeneza card mpya . Kisha anajifanya tena mteja alikuja kufata card yake na amemkabidhi hiyo card mpya.

Kumbe card hiyo anayo yeye mwenyewe mfanyakazi wa bank

Hapo ndipo anaanza ku draw pole pole via ATM kwa kutumia hiyo card yenye jina la mteja mwenye account
Huna unachokijua khusu ATM CARD.....tulia hivyohivyoooo
 
Ni kweli. Kuna kesi nyingi za warithi kudhulumiwa na kudanganywa kuhusu kiasi cha fedha kilichokuwa kwenye account ya marehemu.

Binafsi mzee wangu alikuwa anafanya shughuli zake na alikuwa anaweka fedha benki pia Alikuwa mstaafu so alikuwa analipwa Pension yake via NMB. Mwaka ambao mzee alifariki, alivuna mpunga na akauza gunia zaidi ya 500 ambazo alipeleka benki. Baada ya kufariki na tulikaa muda mrefu kupata utaratibu wa mirathi kwenda benki tunaambiwa mzee alikuwa na laki saba tu benki.
Ungeomba statement ya bank
 
Japokuwa me ni member wa hizi harakati

Black panther
Civil rights movement
Back to africa movement


Lakini linapokuja swala la kumuamini mtu mweusi najivua hayo magamba kwa muda.
Nimecheka balaaa hadi machozi yamenitoka. Nigga ni mtu moja hovyo sana mchafu siyo honest. Bure kabisa.
14729.png
 
Na utakuta huyo Samweli hizo pesa kaenda kuhonga malaya na sasa anajuta sana.
Ajiangalie yeye na wezi wenzake watapakatwa veri suni.
 
Mfanyabiashara maarufu katika mikoa ya Arusha, Dar na Dodoma Joseph Kalugendo mkazi wa Moshoni jijini Arusha, ameibiwa fedha zake zaidi ya milioni 100 katika benki ya NMB tawi la Clock Tower Arusha na mtumishi wa benki hiyo.

Taarifa ambazo zimethibitishwa na Mfanyabiashara huyo amedai kuwa siku za usoni alienda katika benki hiyo kwa ajili ya kuchukua fedha ndipo alipopigwa na butwaa kukuta kitita hicho hakipo.

Meneja wa benki hiyo Kanda ya Kaskazini Praygod Mphuru alipohojiwa alikiri kuwepo kwa tukio hilo akidai tayari wamemsimamisha kazi mfanyakazi wao Samweli na kwamba suala hilo linafanyiwa kazi na kuomba suala hilo lisitangazwe.

Pia vigogo wa benki hiyo kwa sasa wanahaha kutafuta mchawi aliyetoa taarifa hizo kwa waandishi wa habari na tayari baadhi ya wafanyakazi wameitwa na kuhojiwa juu ya taarifa hizo za ndani kufika kwa wanahabari

Joseph ambaye hufanya biashara za bar na kusambaza vyakula kwenye kambi za jeshi anadaiwa kulundika kiasi hicho cha fedha kwa muda mrefu bila kutoa kiasi, na kwamba mfanyakazi huyo aliona huenda anayeimiliki alishakufa na kuanza kuchomoa kidogo kidogo na kufikia zaidi ya Tsh. Milioni 100.

Hata hivyo baada ya taarifa hizo kubainika uongozi wa benki ulifanya kikao kizito na kubaini kwamba mfanyakazi wao aliyefahamika kwa jina moja la Samweli ndiye aliyehusika na wizi huo kwa kuchomoa fedha hizo kidogo kidogo hadi kufikia hicho cha fedha.

Uongozi wa benki hiyo tayari umemsimamisha kazi lakini suala hilo bado lipo kimya huku Mfanyabiashara huyo akilalamikia hatima ya fedha zake, maana benki hiyo kuwa kimya na haimpi jibu linaloeweka namna ya kurejeshewa.

Miaka minne niliacha million 3 kcb ,ATM card ilivunjika nikakosa muda wa kuingia counter ,gafla scholarship hii hapa,nikaeda masomoni nimerudi nikaenda counter mzigo umeongezeka Laki kadhaa ,imefanya niipende hii bank
 
Alijiaminisha vipi mwenye pesa zake kafa. So stupid and incompetent. Ila Joseph ana hela bwana. Mpaka akazisahau hizi 100M. Sijui matako bar bado ipo? Ilijua kumpatia pesa ndefu 🙌🏾🙌🏾
Hivi Matako bar ni ya huyu mhaya?? Nasikia Angelo Mwoleka pia alikuwa mmiliki ila siku hizi imefubaa
 
Inakuwaje pesa zichomolewe asipewe taarifa kwa ujumbe mfupi? Au huyo jamaa alifanya yake zikitolewa asipate taarifa?

shirikisha akili vizuri utapata majibu, ni uchaguzi kupata hizo taarifa, sio lazima!
 
Back
Top Bottom